Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
Kweli kabisa. Moja ya maamuzi ya kipuuzi kutokea katika Bunge la Tanzania, ni lile la kuondoa Wabunge kuitwa 'ndugu' na kubadilishwa na 'mheshimiwa'. Katika nchi inayojaribu kuleta usawa na kupambana na ulevi wa madaraka, kitendo hiki kimechangia kwa Wabunge wengi, Spika wa sasa, kujiona Mungu-mtu. Uheshimiwa ni sifa ya mtu anayejistahi, mwenye hekima na sera njema.
Anayefanya kazi kwa kujitolea zaidi akiangalia maslahi ya watu na si binafsi, mpinga rushwa, ubadhirifu.... ni wangapi katika bunge hivi sasa?
Kama nikiwa kiongozi, nitaamuru wote serikalini na mihimili mingine waitwe 'mtumishi'. Bwana mtumishi kadhaa, bibi mtumishi kadhaa. Hii itatia dhana katika vichwa vyao kuwa wananchi ndiyo maboss wao, na siyo kama sasa ambapo wengi wanadhani wanatutendea 'fadhila' na kwamba mmoja wao akifa au akiondoka maisha yetu yataingia dosari!