Mzee Warioba, Tahadhari: Huwezi Kugeuzwa kuwa Jiwe la Chumvi

Kalamu

Platinum Member
Joined
Nov 26, 2006
Posts
22,898
Reaction score
33,309
Umesimama vyema kabisa katika kupigania maslahi ya taifa hili kila mara, lakini umepuuzwa na kudharauliwa na hao hao wanaotaka sasa uwe dodoki la kufuta uchafu.

Umekuwa ni sauti pekee iliyosalia ikisikika kushauri na kuonya juu ya mwelekeo mbaya linakoelekezwa taifa hili bila ya kukata tamaa.

Umepuuzwa na kutengwa na kuwa wewe ndiye adui wa taifa hili.

Sasa baada ya kupuuzwa huko, na watawala kutimiza malengo yao ya kuchukuwa uongozi wa nchi kwa mabavu na kusababisha upotevu wa maisha ya waTanzania; watu hao hao wanageuka nyuma na kutaka wakutumie wewe kuhalalisha uovu wao na kuwasafisha.

Utawala uliopo ni HARAMU; huwezi kushiriki katika kuponya taifa wakati waliodharau maonyo yako wakiendelea kushika madaraka ya uongozi.

Utaanzia wapi kushughulikia Katiba Mpya chini ya maelekezo ya watu ambao tayari wamekudharau na kuwadharau waTanzania?

Hiyo kazi ya mchakato wa Katiba Mpya, pamoja na umuhimu wake ulivyo; tafadhali, usikubali kusimamia kazi hiyo chini ya serikali HARAMU hii; na wakati ambapo maswala mengi ya uovu uliofanyika bado hayajapata suluhisho.

Njia pekee ya wewe kujihusisha na kazi hiyo tukufu kwa taifa letu ni hapo hawa watawala watakapokuwa nje ya uongozi wa serikali haramu; na wafungwa wote wa kisiasa wakisha achiwa huru.

Kamwe usikubali kutumika kama kikaratasi cha kufutia uchafu.
 
Hapana, hakuna ugumu wowote kama sisi wenyewe tukidhamiria kuiweka sawa nchi yetu.
Hii ni kazi yetu; hatuwezi kumtegemea mtu mwingine yeyote aifanye kwa niaba yetu.
tatizo SMG na AK47
 
Warioba siyo Mjinga
Naamini kabisa kuwa Mzee Warioba siyo mjinga.
Maana yangu ya kumpa tahadhari ni huu ulaghai mwingi unaotumiwa na huyu mwanamke shetani kabisa.

Wakati huu atatumia sababu ya kuponya taifa; na umuhimu wa kuwa na hiyo Katiba Mpya; ili kumfanya mzee wa watu ashawishike kuisimamia kazi hiyo muhimu.

Naelewa mzalendo yeyote atashawishika kama kazi anayo ombwa kuisimamiaina umuhimu kama ilivyo hii ya Katiba Mpya.
Ninachomtahadharisha mzee Warioba, ni kutumiwa kwa lengo la kuwasaidia kukaa madarakani hawa waovu, wakati uwepo wao huo ukiwa ni haramu.
 
Chezea kibuyu cha asali ww 😂
Wewe tayari umekwisha toa hukumu? Kuna wazalendo wasiotetereshwa na hivyo vibuyu vya aslai uchwara.
Hakuna "kibuyu cha asali" kinachoizidi utamu ilionao nchi yetu hii Tanzania. Hiku pekee, ndicho kibuyu cha asali cha uhakika.

Nenda kamuulize Tundu Lissu kama huamini ninayokwambia mimi.
 
Na sisi tutazipata tu, maana juzi hizo ndio tulizikosa. Kama wao wanakaa kwa silaha za moto, basi watatoka kwa silaha hizo hizo za moto.
Sasa hivi hizo ndizo pekee wanazozitegemea kuwa madarakani; wanaozishikilia kwa niaba yetu na wao karibuni watageuka na kuwa upande wetu. Hawa wengi wao ni waTanzania tu kama tulivyo wengi wetu.
 
Umesimama vyema kabisa katika kupigania maslahi ya taifa hili kila mara, lakini umepuuzwa na kudharauliwa na hao hao wanaotaka sasa uwe dodoki la kufuta uchafu.

Umekuwa ni sauti pekee iliyosalia ikisikika kushauri na kuonya juu ya mwelekeo mbaya linakoelekezwa taifa hili bila ya kukata tamaa.

Umepuuzwa na kutengwa na kuwa wewe ndiye adui wa taifa hili.

Sasa baada ya kupuuzwa huko, na watawala kutimiza malengo yao ya kuchukuwa uongozi wa nchi kwa mabavu na kusababisha upotevu wa maisha ya waTanzania; watu hao hao wanageuka nyuma na kutaka wakutumie wewe kuhalalisha uovu wao na kuwasafisha.

Utawala uliopo ni HARAMU; huwezi kushiriki katika kuponya taifa wakati waliodharau maonyo yako wakiendelea kushika madaraka ya uongozi.

Utaanzia wapi kushughulikia Katiba Mpya chini ya maelekezo ya watu ambao tayari wamekudharau na kuwadharau waTanzania?

Hiyo kazi ya mchakato wa Katiba Mpya, pamoja na umuhimu wake ulivyo; tafadhali, usikubali kusimamia kazi hiyo chini ya serikali HARAMU hii; na wakati ambapo maswala mengi ya uovu uliofanyika bado hayajapata suluhisho.

Njia pekee ya wewe kujihusisha na kazi hiyo tukufu kwa taifa letu ni hapo hawa watawala watakapokuwa nje ya uongozi wa serikali haramu; na wafungwa wote wa kisiasa wakisha achiwa huru.

Kamwe usikubali kutumika kama kikaratasi cha kufutia uchafu.
Wewe nani wa kumshauri Jaji Warioba? Ungekuwa mawazo yako yanahitajika ungeitwa wewe. Kazi kujipa umaarufu usiokuwa nao.

Yaani upande wewe ni mhamasisha maandamano, halafu wewe leo ndiyo uwe na mawazo ya kumshauri Warioba?? Nyie wachoma nchi bama, hatuwataki kwendeni zenu
 
Unanijibu wewe ukiwa kama nani, nguruwe wa Samia?
Kwa hiyo sasa hivi mnamwona huyo mzee kuwa wa maana kwenu baada ya dharau na madhalilisho mengi mliyompa kwa kuwapa ushauri mzuri tu; ili msimwage damu ya waTanzania!

Sasa mmekwishatimiza lengo lenu; na kuchafuka hovyo kabisa, mnataka kumrudia tena ili awasaidie kuendelea kuwa madarakani?.

Kama unaniweka kwenye uhamasishaji wa maandamano; nipe sababu ya kutofanya hivyo ili kuondokana na ushenzi wenu huu mliouleta kwenye taifa letu.

Ndiyo, nitahamasisha maandamano, kama ndiyo njia pekee iliyobaki kuondoa takataka nyie madarakani.
 
Tunaamini amempa stahiki yake na za uso za kutosha......alichokitegemea ...sicho alichopata jana......yule Butiku ni mnafiki hana IQ ya Warioba yule ni chawa tu hana uwezo huo ndio maana amekubali kununuliwa 1b.....mpuuzii
 
Muache mzee na yeye apige hela unafikiri yeye ni mjinga
Leo unakubali mwenyewe kuwa unahangaika sana humu JF kwa sababu ya "kupiga hela"?

Butiku anapiga hela; Wasira anapiga hela. Mzee Warioba angekuwa ni mpiga hela wakati huu usingemsikia tena akitajwa tajwa na yeyote. Mzee wa watu amenyanyasika sana kwa msimamo wake usioyumba juu ya hatma ya taifa hili..
 
Mimi najitolea mkuu na sio mwanasiasa na sina chama
 
Back
Top Bottom