Umesimama vyema kabisa katika kupigania maslahi ya taifa hili kila mara, lakini umepuuzwa na kudharauliwa na hao hao wanaotaka sasa uwe dodoki la kufuta uchafu.
Umekuwa ni sauti pekee iliyosalia ikisikika kushauri na kuonya juu ya mwelekeo mbaya linakoelekezwa taifa hili bila ya kukata tamaa.
Umepuuzwa na kutengwa na kuwa wewe ndiye adui wa taifa hili.
Sasa baada ya kupuuzwa huko, na watawala kutimiza malengo yao ya kuchukuwa uongozi wa nchi kwa mabavu na kusababisha upotevu wa maisha ya waTanzania; watu hao hao wanageuka nyuma na kutaka wakutumie wewe kuhalalisha uovu wao na kuwasafisha.
Utawala uliopo ni HARAMU; huwezi kushiriki katika kuponya taifa wakati waliodharau maonyo yako wakiendelea kushika madaraka ya uongozi.
Utaanzia wapi kushughulikia Katiba Mpya chini ya maelekezo ya watu ambao tayari wamekudharau na kuwadharau waTanzania?
Hiyo kazi ya mchakato wa Katiba Mpya, pamoja na umuhimu wake ulivyo; tafadhali, usikubali kusimamia kazi hiyo chini ya serikali HARAMU hii; na wakati ambapo maswala mengi ya uovu uliofanyika bado hayajapata suluhisho.
Njia pekee ya wewe kujihusisha na kazi hiyo tukufu kwa taifa letu ni hapo hawa watawala watakapokuwa nje ya uongozi wa serikali haramu; na wafungwa wote wa kisiasa wakisha achiwa huru.
Kamwe usikubali kutumika kama kikaratasi cha kufutia uchafu.