Mzee Warioba: Wabunge huchaguliwa kwa misingi ya Ukabila na Bahasha

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Jaji Warioba amesema Siasa za Tanzania zinaendeshwa mikanda, kikabila na kidini na hili liko wazi kabisa

Warioba amesema mfano rahisi ni Wabunge wa Bunge la JMT ambao huenda kugombea vijijini kwao ili wachaguliwe na watu wa makabila yao wakipozwa na " Bahasha"

Source ITV habari
 
Ni kweli BILA hela ya kahawa kwa wanyamwezi HUKO unafikiri Protas na ntimizi wangekuwa WABUNGE!!?

Full umafia !Ndio màana nataka;-

"Rasimu ya Warioba irudi mezani Sasa owe latina Mpya!
 
Sio tu,bahasha na kahawa,upo ule umafia wa kuteka wagombea wengine na kuwapora fomu Ili kupitia bila kupingwa au kuwaweka pingamizi uchwara 🤔
 
Kuna clip moja nimeiona jana humu JF Magufuli anamdismiss Mbunge wa Upinzani huku akimtetea nadhani alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri maeneo ya Mara huko. Magufuli mwisho akasema "kwanza huyu siyo mtu wa huku anatokea huko Morogoro sijui kuja kuwavuruga hapa".
 
Ukabila ulikuwa upo ila haukuwa na nguvu until kipind chake aka amplify hiyo kitu.
 
Mwambie Hakuna tatizo zikiendeshwa hivyo kama viongozi wanachaguliwa katika uchaguzi huru na wa haki na sio kupitia teuzi. Siasa duniani kote huwa zinaendeshwa kwa namna hiyo, watu wanamchagua mtu wanayemtaka. Wakifanya hivyo kwa sababu ya dini yake, kanda au kabila ni sawa tu.
Jaji Warioba amesema Siasa za Tanzania zinaendeshwa mikanda, kikabila na kidini na hili liko wazi kabisa

Warioba amesema mfano rahisi ni Wabunge wa Bunge la JMT ambao huenda kugombea vijijini kwao ili wachaguliwe na watu wa makabila yao wakipozwa na " Bahasha"

Source ITV habari
 
Kasema ukweli kabisa.ukanda umekithiri sana awamu hii.kama wewe siyo mzenji au mpwani teuzi utazisikia redioni tu
 
Jaji Warioba amesema Siasa za Tanzania zinaendeshwa mikanda, kikabila na kidini na hili liko wazi kabisa

Warioba amesema mfano rahisi ni Wabunge wa Bunge la JMT ambao huenda kugombea vijijini kwao ili wachaguliwe na watu wa makabila yao wakipozwa na " Bahasha"

Source ITV habari
wewe si ndo unayeshabikia hayo mambo humu ndani?alichosena ndo uhalisia wenyewe.hakuna alipopindisha hata kidogo hata mwalimu aliishaliongelea hilo sana ktk hotuba zake mbali mbali.ccm imejaa rushwa ya kila aina.
 
Mwambie Hakuna tatizo zikiendeshwa hivyo kama viongozi wanachaguliwa katika uchaguzi huru na wa haki na sio kupitia teuzi. Siasa duniani kote huwa zinaendeshwa kwa namna hiyo, watu wanamchagua mtu wanayemtaka. Wakifanya hivyo kwa sababu ya dini yake, kanda au kabila ni sawa tu.
Uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki tena kama unakiri mgombea anachaguliwa kwa vigezo vya dini, na kabila lake.

Kwa sababu wale wasio wa dini au kabila hilo, hawapati uwanja sawa na yule wa kabila na eneo alipotoka, hata kama ana sifa za ziada kiutendaji.
 
Wakati mwengine mzee anazungumza vitu vinavyoibua maswali sana. Hivi kuna sehemu Tanzania ambako kuna jimbo la kabila au dini flani wakati tumechanganywa kama taifa tangu enzi za Mwalimu? Hizi ni fikra za udini na ukabila.

Halafu mtu lazima akagombee anakotoka ili ajue Rural sociology ya hilo jimbo na wananchi wamjue . Point ya rushwa tunaweza kukubaliana ktk baadhi ya maeneo siyo general kama alivyoongea mzee. Yaani kila jimbo kuna rushwa? Hii ni fallacy generalization.🙏🙏🙏
 
Kwa mfano Mbowe anagombea Hai kwa sababu za ukabila vinginevyo angegombea Kawe anakojulikana miaka yote
 
Wakati mwengine mzee anazungumza vitu vinavyoibua maswali sana. Hivi kuna sehemu Tanzania ambako kuna jimbo la kabila au dini flani wakati tumechanganywa kama taifa tangu enzi za Mwalimu? Hizi ni fikra za udini na ukabila.

Halafu mtu lazima akagombee anakotoka ili ajue Rural sociology ya hilo jimbo na wananchi wamjue . Point ya rushwa tunaweza kukubaliana ktk baadhi ya maeneo siyo general kama alivyoongea mzee. Yaani kila jimbo kuna rushwa? Hii ni fallacy generalization.🙏🙏🙏

Kwa nini Nyerere na wenzake walikuwa na chuki sana na makabila ya watu? Mpaka akataka Watanzania wajichanganye, wasiyazungumzie makabila yao. Makabila yalimkosea nini Nyerere mpaka ayapige vita kiasi kile?
 
Back
Top Bottom