Nyerere hakuwa na chuki na makabila ya watu ila huenda aliangalia migogoro na mauji yaliyokiwa yanaendelea Rwanda, Congo, Burundi, Uganda, Zimbabwe, Nigeria n.k ambayo kwa sehemu kubwa ilitokana na ukabila. Kwa kipindi kile alikuwa sahihi ila baadaye waka overdo walipoifanya hii kuwa ajenda ya kudumu. Zaidi sana sio rahisi hata kidogo kuwa na ukabila Tanzania, sio rahisi kuwa na kabila moja linalo dominate na kukandamiza makabila mengine.
Jambo la kushangaza dini imetumika kwa ubaguzi, ukandamizaji na kama kichocheo kimojwapo cha vurugu na vita sehemu kadhaa duniani ila haikupuuzwa au watu hawahamasishwi kuipuuza mpaka leo! Kumekuwepo na Jihads na Crusades, migogoro ya Msumbiji, Somalia, Nigeria, Rwanda, Mnymar, vita vya Iraq-Iran, vita vya Israel-Palestina, Sudan, Yugoslavia, Vietnam, Afrika Kusini, Kashmir n.k dini zimehusika pakubwa sana.