Mzee Warioba: Wabunge huchaguliwa kwa misingi ya Ukabila na Bahasha

Siasa za Tanzania kuna vitu vya kuchekesha sana,
Mtu ameishi Dar es Salaam utu uzima wake wote halafu wakati wa uchaguzi anaenda kugombea Kasulu au Kilosa!
Mbunge ambaye ni mwakilishi wa watu wake anatakiwa mtu anayeishi hilo eneo muda wote na anayeishi na wananchi wake, sio mtu anagombea tu kwa sababu kuna babu na bibi yake hapo.
Wakati mwengine mzee anazungumza vitu vinavyoibua maswali sana. Hivi kuna sehemu Tanzania ambako kuna jimbo la kabila au dini flani wakati tumechanganywa kama taifa tangu enzi za Mwalimu? Hizi ni fikra za udini na ukabila.

Halafu mtu lazima akagombee anakotoka ili ajue Rural sociology ya hilo jimbo na wananchi wamjue . Point ya rushwa tunaweza kukubaliana ktk baadhi ya maeneo siyo general kama alivyoongea mzee. Yaani kila jimbo kuna rushwa? Hii ni fallacy generalization.[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Hapa hakuna cha kubisha. Mzee kasema ukweli lakini ingependeza zaidi kama angekuja na ways za kuondoa hiyo situation katika taifa letu. Unless otherwise ni kutafuta popularity tu.
Warioba atafute umaarufu wakati huu! Mbona alifanya vizuri sana kwenye maoni ya katiba mpya ambayo ilitokea kuwa tishio kwa CCM na hakutafuta umaarufu kama alivyofanya Polepole.
 
Siasa za Tanzania kuna vitu vya kuchekesha sana,
Mtu ameishi Dar es Salaam utu uzima wake wote halafu wakati wa uchaguzi anaenda kugombea Kasulu au Kilosa!
Mbunge ambaye ni mwakilishi wa watu wake anatakiwa mtu anayeishi hilo eneo muda wote na anayeishi na wananchi wake, sio mtu anagombea tu kwa sababu kuna babu na bibi yake hapo.
Ndio ukabila huo!
 
Jaji Warioba amesema Siasa za Tanzania zinaendeshwa mikanda, kikabila na kidini na hili liko wazi kabisa

Warioba amesema mfano rahisi ni Wabunge wa Bunge la JMT ambao huenda kugombea vijijini kwao ili wachaguliwe na watu wa makabila yao wakipozwa na " Bahasha"

Source ITV habari
Duh !! Mzee katema nyongo !! Huyu mzee anazeeka vizuri sana !!Anaendelea kutumia akili yake vizuri sana !! Mungu ambariki sana. !
 
UKabila Bado upo s'na tu, ni vile hauongelewi kma Kenya. We nenda kagombee ubunge au udiwan sehemu usiyo na nasaba Nayo!! UOne utapta hyo nafasi Ukiacha maeneo machache ya mjini..
Kweli kabisa !!
 
Siasa za Tanzania kuna vitu vya kuchekesha sana,
Mtu ameishi Dar es Salaam utu uzima wake wote halafu wakati wa uchaguzi anaenda kugombea Kasulu au Kilosa!
Mbunge ambaye ni mwakilishi wa watu wake anatakiwa mtu anayeishi hilo eneo muda wote na anayeishi na wananchi wake, sio mtu anagombea tu kwa sababu kuna babu na bibi yake hapo.
Hakika !!
 
Ubaguzi na uonevu kwa misingi ya kisiasa ni hatari zaidi kuliko ukabila,ukanda na udini.
 
Hapa hakuna cha kubisha. Mzee kasema ukweli lakini ingependeza zaidi kama angekuja na ways za kuondoa hiyo situation katika taifa letu. Unless otherwise ni kutafuta popularity tu.
Alikuja na Rasmi ya Katiba Mpya Makonda Alimpiga Makofi
Bunge la KATIBA lilipovunjika Walimnyanganya gari Dodoma yeye na Wajumbe wenzake walidharirishwa sana
 
Ukabila sio tatizo kama kelele nyingi zinavyopigwa, tatizo kubwa ni akili ndogo za Waafrika wengi ambao hupelekea kudhulumiana na kuuana kwa sababu ya ukabila au udini.

Huwezi kusema uchaguzi sio huru na haki eti kwasababu;

Wamasai wamemchagua Mmasai mwenzao kwa kuamini anaweza kuwakilisha na kutetea maslahi yao vizuri zaidi bungeni.

Waislamu wamemchagua Muislamu kwa kuamini atawapa mahakama ya kadhi kama wanaitaka na ndio kipaumbele chao.

Wakristo wamemchagua mtu wanayeamini atawapa nafuu za kisera na kodi kwenye shule, hospitali na vyuo vyao vya kidini.

Marekani, Wakristo wa Msimamo mkali wanaopinga Utoaji mimba na Ushoga walimchagua kwa wingi Trump dhidi ya Clinton na akashinda kwa haki kabisa huku Clinton akikubali matokeo. Walifanya hivyo tena dhidi ya Biden ila Wa Democrats ilibidi wafanye kazi ya ziada kuhamasisha watu wao wapige kura kwa wingi zaidi jambo ambalo liliwapa ushindi.
Simply haya mawazo yako naona yanachochea matabaka kwenye jamii, jambo ambalo sio zuri kwa upande wangu.

Hatuwezi kuwa na jamii inayochagua watu kwa sababu ya dini yao ili wakatimize yaliyoandikwa kwenye vitabu vyao, wakati jamii tunamoishi ni mchanganyiko.
 
Hapa hakuna cha kubisha. Mzee kasema ukweli lakini ingependeza zaidi kama angekuja na ways za kuondoa hiyo situation katika taifa letu. Unless otherwise ni kutafuta popularity tu.
Katiba mpya
 
Siasa za Tanzania kuna vitu vya kuchekesha sana,
Mtu ameishi Dar es Salaam utu uzima wake wote halafu wakati wa uchaguzi anaenda kugombea Kasulu au Kilosa!
Mbunge ambaye ni mwakilishi wa watu wake anatakiwa mtu anayeishi hilo eneo muda wote na anayeishi na wananchi wake, sio mtu anagombea tu kwa sababu kuna babu na bibi yake hapo.

..kuna baadhi ambao wamekuja D'Salaam kwa ajili ya kutafuta tu, lakini mioyo na mapenzi yao yako vijijini walikozaliwa.

..Na pamoja na kuishi kwa muda mrefu D'Salaam bado wanajihusisha kwa ukaribu na masuala ya kijamii na kisiasa ya vjijini ambako ndiko chimbuko na asili yao.

..lakini hawa ninaowazungumzia hapa, watoto wao waliowazaa D'Salaam hawajihisi kama ni watu wa kutoka kule ambako ni chimbuko la wazazi wao.

..Mfano mzuri ni Mzee Joseph Warioba. Yeye aliishi D'Salaam kikazi lakini akaenda kugombea ubunge kwao Bunda. Mwanae Warioba, ambaye anaitwa Kippi alizaliwa mjini na amegombea ubunge jimbo la Kawe zaidi ya mara moja.

..Binafsi sikubaliani na Mzee Warioba kwamba kuna ukabila.
 
Tatizo namba moja Tanzania hii ni CCM,haya mengine ni blaa blaa tu.
 
Njia pekee ya kupunguza na kuondoa hilo, ni kutumia mfumo wa uwakilishi wenye uwiano(proportional representation) kwenye kuchagua wabunge, madiwani etc. Hii inasaidia sana hata makundi madogo madogo, kwenye jamii au eneo fulani kupata uwakilishi kwenye vyombo hivyo. Pia inasaidia vyama vidogo kuchipuka na kukomaa. Sio bunge linakuwa la chama kimoja au viwili tu.
 
Hana cha kupoteza kama kula ameshakula na kusaza basi kama mbwai mbwai tu.
 
..kuna baadhi ambao wamekuja D'Salaam kwa ajili ya kutafuta tu, lakini mioyo na mapenzi yao yako vijijini walikozaliwa.

..Na pamoja na kuishi kwa muda mrefu D'Salaam bado wanajihusisha kwa ukaribu na masuala ya kijamii na kisiasa ya vjijini ambako ndiko chimbuko na asili yao.

..lakini hawa ninaowazungumzia hapa, watoto wao waliowazaa D'Salaam hawajihisi kama ni watu wa kutoka kule ambako ni chimbuko la wazazi wao.

..Mfano mzuri ni Mzee Joseph Warioba. Yeye aliishi D'Salaam kikazi lakini akaenda kugombea ubunge kwao Bunda. Mwanae Warioba, ambaye anaitwa Kippi alizaliwa mjini na amegombea ubunge jimbo la Kawe zaidi ya mara moja.

..Binafsi sikubaliani na Mzee Warioba kwamba kuna ukabila.
Mara ya mwisho Kipi amegombea umamani pale Moshi
 
Hapa hakuna cha kubisha. Mzee kasema ukweli lakini ingependeza zaidi kama angekuja na ways za kuondoa hiyo situation katika taifa letu. Unless otherwise ni kutafuta popularity tu.
Kusema mzee warioba anatafuta popularity ni tusi kubwa bora ungenitukana mimi tu mkuu
 
Back
Top Bottom