Mzee Warioba: Wabunge huchaguliwa kwa misingi ya Ukabila na Bahasha

Siasa za Tanzania kuna vitu vya kuchekesha sana,
Mtu ameishi Dar es Salaam utu uzima wake wote halafu wakati wa uchaguzi anaenda kugombea Kasulu au Kilosa!
Mbunge ambaye ni mwakilishi wa watu wake anatakiwa mtu anayeishi hilo eneo muda wote na anayeishi na wananchi wake, sio mtu anagombea tu kwa sababu kuna babu na bibi yake hapo.
 
Hapa hakuna cha kubisha. Mzee kasema ukweli lakini ingependeza zaidi kama angekuja na ways za kuondoa hiyo situation katika taifa letu. Unless otherwise ni kutafuta popularity tu.
Warioba atafute umaarufu wakati huu! Mbona alifanya vizuri sana kwenye maoni ya katiba mpya ambayo ilitokea kuwa tishio kwa CCM na hakutafuta umaarufu kama alivyofanya Polepole.
 
Ndio ukabila huo!
 
Duh !! Mzee katema nyongo !! Huyu mzee anazeeka vizuri sana !!Anaendelea kutumia akili yake vizuri sana !! Mungu ambariki sana. !
 
UKabila Bado upo s'na tu, ni vile hauongelewi kma Kenya. We nenda kagombee ubunge au udiwan sehemu usiyo na nasaba Nayo!! UOne utapta hyo nafasi Ukiacha maeneo machache ya mjini..
Kweli kabisa !!
 
Hakika !!
 
Ubaguzi na uonevu kwa misingi ya kisiasa ni hatari zaidi kuliko ukabila,ukanda na udini.
 
Hapa hakuna cha kubisha. Mzee kasema ukweli lakini ingependeza zaidi kama angekuja na ways za kuondoa hiyo situation katika taifa letu. Unless otherwise ni kutafuta popularity tu.
Alikuja na Rasmi ya Katiba Mpya Makonda Alimpiga Makofi
Bunge la KATIBA lilipovunjika Walimnyanganya gari Dodoma yeye na Wajumbe wenzake walidharirishwa sana
 
Simply haya mawazo yako naona yanachochea matabaka kwenye jamii, jambo ambalo sio zuri kwa upande wangu.

Hatuwezi kuwa na jamii inayochagua watu kwa sababu ya dini yao ili wakatimize yaliyoandikwa kwenye vitabu vyao, wakati jamii tunamoishi ni mchanganyiko.
 
Hapa hakuna cha kubisha. Mzee kasema ukweli lakini ingependeza zaidi kama angekuja na ways za kuondoa hiyo situation katika taifa letu. Unless otherwise ni kutafuta popularity tu.
Katiba mpya
 

..kuna baadhi ambao wamekuja D'Salaam kwa ajili ya kutafuta tu, lakini mioyo na mapenzi yao yako vijijini walikozaliwa.

..Na pamoja na kuishi kwa muda mrefu D'Salaam bado wanajihusisha kwa ukaribu na masuala ya kijamii na kisiasa ya vjijini ambako ndiko chimbuko na asili yao.

..lakini hawa ninaowazungumzia hapa, watoto wao waliowazaa D'Salaam hawajihisi kama ni watu wa kutoka kule ambako ni chimbuko la wazazi wao.

..Mfano mzuri ni Mzee Joseph Warioba. Yeye aliishi D'Salaam kikazi lakini akaenda kugombea ubunge kwao Bunda. Mwanae Warioba, ambaye anaitwa Kippi alizaliwa mjini na amegombea ubunge jimbo la Kawe zaidi ya mara moja.

..Binafsi sikubaliani na Mzee Warioba kwamba kuna ukabila.
 
Tatizo namba moja Tanzania hii ni CCM,haya mengine ni blaa blaa tu.
 
Njia pekee ya kupunguza na kuondoa hilo, ni kutumia mfumo wa uwakilishi wenye uwiano(proportional representation) kwenye kuchagua wabunge, madiwani etc. Hii inasaidia sana hata makundi madogo madogo, kwenye jamii au eneo fulani kupata uwakilishi kwenye vyombo hivyo. Pia inasaidia vyama vidogo kuchipuka na kukomaa. Sio bunge linakuwa la chama kimoja au viwili tu.
 
Hana cha kupoteza kama kula ameshakula na kusaza basi kama mbwai mbwai tu.
 
Mara ya mwisho Kipi amegombea umamani pale Moshi
 
Hapa hakuna cha kubisha. Mzee kasema ukweli lakini ingependeza zaidi kama angekuja na ways za kuondoa hiyo situation katika taifa letu. Unless otherwise ni kutafuta popularity tu.
Kusema mzee warioba anatafuta popularity ni tusi kubwa bora ungenitukana mimi tu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…