Mzee Warioba: Wabunge huchaguliwa kwa misingi ya Ukabila na Bahasha

Huyu mzee bwana, kaenjoy system weeeeee na mpaka saivi anakula 80% ya mshahara wa PM aliyepo afu anajikuta mzalendo.

Wanazingua sana hawa wazee!
 
wabunge wetu hutumia nguvu kubwa sana kuingia madarakani kuna jambo
 
Waliokuja kutafuta D'Salaam wanaelewa zaidi changamoto za Daslamu kwa sababu hapa ndipo wanapofanya sehemu kubwa ya maisha, wanaweza kuwa wawakilishi wazuri zaidi wa hapa kuliko kule walipotoka.

Tatizo linaenda mbali zaidi na kuwa kubwa sana kwa sababu unakuta hao wabunge wengi wa huko mikoani wanaishi Dar hata wakiwa wabunge badala ya kuishi kwenye majimbo yao na wale waliowachagua.
 
Sidhani kama ulimaanisha matabaka maana kwenye jamii yoyote ile huwa kuna makundi tofauti ya watu na huwa yana maslahi tofauti, Wafanyakazi wana maslahi yao, wakulima wana yao, Wafanyabiashara wana yao, wafugaji wana yao, wavuvi wana yao, Waislamu wana yao, Wakristo wana yao n.k

Katika demokrasia halisi mshindi hupatikana kwa kuweza kuwashawishi wapiga kura wengi kutoka makundi/matabaka mengi zaidi au makubwa yamchague. Huo ndio uhalisia.
 
Kwa nini Nyerere na wenzake walikuwa na chuki sana na makabila ya watu? Mpaka akataka Watanzania wajichanganye, wasiyazungumzie makabila yao. Makabila yalimkosea nini Nyerere mpaka ayapige vita kiasi kile?
Umevamia jf nenda fb
 
Kwa nini Nyerere na wenzake walikuwa na chuki sana na makabila ya watu? Mpaka akataka Watanzania wajichanganye, wasiyazungumzie makabila yao. Makabila yalimkosea nini Nyerere mpaka ayapige vita kiasi kile?
Umevamia jf nenda fb
 
Hapa hakuna cha kubisha. Mzee kasema ukweli lakini ingependeza zaidi kama angekuja na ways za kuondoa hiyo situation katika taifa letu. Unless otherwise ni kutafuta popularity tu.
Humjui mzee warioba ama hujui maana ya popularity?
Umevamia jf nenda fb
 
Bado sioni sababu kwanini pawepo na makundi ili kuchaguana, kwasababu haya makundi yanakuwa na interest tofauti, huwezi kusema namchagua huyu wa kundi langu/mwenzetu ili atujengee kitu chetu, hapa tayari mnakuwa mmewatenga wengine wasio wa kundi lenu, na hii kwangu sio demokrasia, ni kuchaguana kwa upendeleo.

Labda nikupe mfano, kwanini pasiwepo na matukio kama lile la Magufuli kuchangisha pesa za kujengea msikiti kanisani? hii kwangu naamini inasaidia kuondoa utengano, na inazidisha mshikamano baina ya makundi tofauti, na hapa ndipo demokrasia huchanua.
 
Sijaelewa vizuri
 
Magufuli alikuwa mkabila wa hovyo sana
 
Sasa utamchaguaje mtu ambaye hawajui/hajui matatizo ya watu kiundani kabisa,au ikitokea kuna jambo limetokea kwenye Jimbo husika, mzawa wa Jimbo husika ndio anaweza kulielezea kwa ufasaha akizingatia Mila na desturi ya Jimbo husika. Warioba hayupo sahihi kwa kauli hii ya ukabila.
Udini haupo katika kuchagua wabunge,kuna maeneo ambayo yana waislamu wengi,Ila mbunge ni mkristo,mfano Tabora. Pia kuna maeneo ambayo kuna wakristo wengi,Ila mbunge ni muislamu.
 
Interests za Mmasai anayehitaji eneo la mifugo yake, maji, na malisho haziwezi kuwa sawa na za mafanyabiashara wa Kariakoo anayejali zaidi masuala ya kodi na ufanisi wa bandari kwa mizigo yake, pia interests za hao wawili ni tofauti na interests za mfanyakazi anayetegemea kupandishwa mshahara kila mwaka.

Magufuli kuchangisha pesa za kujenga msikiti wala haina uhusiano na demokrasia. Tanzania haina utengeno au ubaguzi wa kidini au kikabila na sio rahisi uje kuwepo tena kwa sababu nyingi sana.
 
Mbunge anawakilisha wananchi wa hilo jimbo..

Sasa mnataka mzaramo akawe mbunge wa Iramba.

Hao wananchi wa vijijini iramba watamueleza shida zao kwa lugha gani? .
maisha ya vijijini kuna watu wanajua lugha asili tu ya kwao. Ndio maana wanachagua mtu wao.. hata kampeni huwa zinafanywa kwa kilugha chao
 
Ndio sababu nimekupa mfano wa Mbowe
 
Halafu tunawakomalia Wakenya. Nani kweli haoni kundule. Cheo pekee ambacho Watanzania hatuchagui kikanda ama kikabila ni cha Rais tu. Na hiyo ni kwa sababu number zetu kikabila hazisupport hiyo. Otherwise, sisi na Kenya ni sawasawa tu.
 
Kwa maana hiyo mhehe anayezungumza kisukuma anaweza kuchaguliwa Misungwi au Geita....!!?
 
Kenya wana uchaguzi huru na haki.
Halafu tunawakomalia Wakenya. Nani kweli haoni kundule. Cheo pekee ambacho Watanzania hatuchagui kikanda ama kikabila ni cha Rais tu. Na hiyo ni kwa sababu number zetu kikabila hazisupport hiyo. Otherwise, sisi na Kenya ni sawasawa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…