Pre GE2025 Mzee Wasira: Wananchi wana njaa, hawawezi kula Katiba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesema kuwa serikali imetekeleza madai yote yaliyowasilishwa na vyama vya upinzani, ikiwemo maridhiano, kurejea kwa wanasiasa waliokimbilia uhamishoni, msamaha kwa waliokuwa gerezani, pamoja na kuruhusu maandamano na mikutano ya hadhara.

"Wapinzani wakiongozwa na CHADEMA walisema hali ni mbaya, wakataka maridhiano, wakataka waliokimbia warudi, wakarudi. Wakasema kuna watu 400 walioshtakiwa na kuhukumiwa mwaka 2020, utaratibu ukafuatwa wakaachiliwa kwa msamaha wa Rais kwa mujibu wa Katiba. Hilo nalo wakapata. Wakasema wanataka mikutano na maandamano, wakapewa, walikuja hata hapa Bunda na helikopta yao kwa sababu wanapenda sana show-off. Lakini nyinyi watu wa Bunda mkawasikiliza, hamna kitu!"

"Sasa kila mahali ni Katiba, Katiba, Katiba! Watu wana njaa, wanataka chakula, wanataka hospitali na elimu, wewe kila siku unasema Katiba! Watakula Katiba?" amehoji Wasira.
Huyu mpumbavu Hana akli
 
..kwa kweli Mzee Wassira amefifia kifikra.

..kama Katiba ni kitu kisichokuwa na maana kwa jamii kwanini Ccm iliandika Katiba mwaka 1977?
 
Eleza katiba tuliyonayo sasa ina tatizo gani?! na ni faida gani wewe utaipata tukiwa na katiba mpya ambayo umeishupalia.!
Mapungufu ni mengi sana, mfano Madaraka makubwa ya Rais: Katiba ya sasa inampa Rais madaraka makubwa, ikiwa ni pamoja na kuteua viongozi wakuu wa mihimili mingine ya serikali, kama vile Jaji Mkuu na viongozi wa vyombo vya usalama. Hii inachangia kudhoofisha uhuru wa mihimili ya dola, hususan Bunge na Mahakama. Alafu huoni kwa stail hii ya uwongozi circle ya watu watakaokuwa wanapata hizo kazi za juu watakuwa hao hao, na familia zao na mifano halisi ipo mkuu, baba alikuwa raisi na mtoto anakuwa raisi, baba alikuwa raisi mama anateuliwa kuwa mbunge keki ya taifa inaliwa na watu wachache na ina loop mule mule. Kwa stail hii hatuwez kupata mtu compitent sababu tutakaokuwa tunawaweka ni wale tunawajua na tutawaweka kwa kujuana na sio kwasababu wana capabilities za kuleta kinachotakiwa...KASOME KATIBA UTAELEWA, JENGA UTAMADUNI WA KUSOMA VITABU, ACHA KUNYWA VISUNGURA NA K VANT ZILE KUBWA HAZINA FAIDA YEYOTE...READING IS FUNDAMENTAL "READING IS FUN TO MENTAL"...
 
Sasa ndio anajenfa kaburi la chama chake miaka 60 mmeshindwa kuzuia nhaa sembuse sasa ? Hizo propaganda za kizanani sana sio sasa zee zima hovyo........
 
..kwa kweli Mzee Wassira amefifia kifikra.

..kama Katiba ni kitu kisichokuwa na maana kwa jamii kwanini Ccm iliandika Katiba mwaka 1977?
Huy Mzee nikimsikiliza nasikitika sana. Mzee Wassira anasema Katiba ya Nchi haina maana, yeye kateuliwa makamu kwa gharama sana ya Katiba ya Chama! Kwanini hakuliona hilo

Wassira kafanya kazi na Viongozi wote wa Nchi hii, Nyerere hadi Samia. Kawa Mkuu wa Mkoa , naibu Waziri na kisha Waziri. Katika utumishi wa miaka 60 hajaweza kuwaeleza Wananchi kwanini ni masikini !

Mzee Wassira kabla hujafungua kinywa, una siri kubwa unayopaswa kueleza Umma.
Kwa miaka zaidi ya 60 ya Uhuru na Utumishi wako kwanini Tanzania ni moja ya Nchi masikini duniani.
 
Inachekesha CCM kusema wananchi tunanjaa. Ni kweli sasa twanatutoaje hapa, au ndio tunasubiri rushwa za October 2025?
 
Ila katiba ndio inayowawezesha kupata chakula na kushiba. Tunachotaka katiba ibadilishwe kudhibiti watawala wanaokimilikisha nchi na kujishibisha wao na familia zao,huku wenye nchi wakitaabika kwa mlo mmoja kwa siku na wengine wakishindia uji.
Wonders shall never end! Huyu Mheshimiwa aliwahi kumchapa mtu makonde kwa sababu alimuita Swahiba. Mahakamani akajitetea kwamba alipatwa na hasira kwani alifikiri neno Swahiba ni tusi yaani ni sawasawa na shoga. Na kisa hicho kilitokea takriban miongo mitatu iliyopita akiwa kijana!
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesema kuwa serikali imetekeleza madai yote yaliyowasilishwa na vyama vya upinzani, ikiwemo maridhiano, kurejea kwa wanasiasa waliokimbilia uhamishoni, msamaha kwa waliokuwa gerezani, pamoja na kuruhusu maandamano na mikutano ya hadhara.

"Wapinzani wakiongozwa na CHADEMA walisema hali ni mbaya, wakataka maridhiano, wakataka waliokimbia warudi, wakarudi. Wakasema kuna watu 400 walioshtakiwa na kuhukumiwa mwaka 2020, utaratibu ukafuatwa wakaachiliwa kwa msamaha wa Rais kwa mujibu wa Katiba. Hilo nalo wakapata. Wakasema wanataka mikutano na maandamano, wakapewa, walikuja hata hapa Bunda na helikopta yao kwa sababu wanapenda sana show-off. Lakini nyinyi watu wa Bunda mkawasikiliza, hamna kitu!"

"Sasa kila mahali ni Katiba, Katiba, Katiba! Watu wana njaa, wanataka chakula, wanataka hospitali na elimu, wewe kila siku unasema Katiba! Watakula Katiba?" amehoji Wasira.
CCM wangempa hata Luhaga Mpina umakamu mwenyekiti ingefaa zaidi maana ana mawazo ya kisasa zaidi. Lakini huyu Mzee aliyejikatia tamaa ya maisha wametukosea Sana wananchi na yeye anazidi kutukosea. Yaani Tatizo uliloleta wewe unajisifia kuwa upo kwenye michakato ya kulitatua.
 
Hiyo yote ni dharau ya mtanifanya nini, viongozi wote kuanzia serikali za mitaa ninao wahitaji nawapata kwa gharama ya dola sasa nyie wananchi mlie tu.
 
Africa haina shida ya katiba bora Wala tume bora ya uchaguzi bali inahitaji mifumo ya kubadili fikra za watu ili wawe na akili ya kuziona fursa tele zinazowazunguka.
Ghana, Malawi, Zambia, Kenya anaeshinda ndie anayepewa still maisha ni afadhali ya Tanzania.
Chaguzi za Africa ni mbinu za kuiba pesa za wananchi.
Africa inahitaji mfumo mpya wa kubadili fikra za watu
 
Yeye yupo toka enzi za mwalimu, walishindwa nini kuwapa wananchi chakula?

Ila veggies mnaboa sana mnataka tumtukane babu tuonekane hatuna adabu..!! Mxieeeeww
Kijani utawaweza basi
 
Africa haina shida ya katiba bora Wala tume bora ya uchaguzi bali inahitaji mifumo ya kubadili fikra za watu ili wawe na akili ya kuziona fursa tele zinazowazunguka.
Ghana, Malawi, Zambia, Kenya anaeshinda ndie anayepewa still maisha ni afadhali ya Tanzania.
Chaguzi za Africa ni mbinu za kuiba pesa za wananchi.
Africa inahitaji mfumo mpya wa kubadili fikra za watu
Ni nfumo gani huo ambao hauhitaji katiba, sheria na kanuni.
 
Hiyo yote ni dharau ya mtanifanya nini, viongozi wote kuanzia serikali za mitaa ninao wahitaji nawapata kwa gharama ya dola sasa nyie wananchi mlie tu.
Nawaza tunatokaje hapa?? 60+ miaka baada ya uhuru tunaishi Kwa kubahatisha kama ndege porini. Waliotufikisha huko hawana habari kabisa tofauti na kujisifia Kwa kutuharibia mfumo wa maisha yetu. Ukiangalia ajira hamna, huduma mbovu za afya, miundo mbinu mibovu halafu aliyetufikisha hapo anajimwambafi anapiga kazi.
 
Miaka 60 iliyopita Tanzania ilikuwa na idadi ya watu wa ngapi na hivi leo tuko wangapi ?!
Miaka 60 iliyopita kwenye mkoa wako barabara za lami zilikiwa kilometa ngapi na leo zipo kilometa ngapi?!
Miaka 60 iliyopita kwenye wilaya yako palikuwa na shule za sekondari ngapi na leo zipo sekondari ngapi?!
Miaka 60 iliyopita Tanzania nzima ilikuwa na vyuo vikuu vingapi na Leo hii vipo vingapi?!
Miaka 60 iliyopita nchi nzima tulikuwa na vituo vya radio vingapi na leo hii vipo vingapi?
Miaka 60 iliyopita nchi nzima tulikuwa na vituo vya television vingapi na Leo hii vipo vingapi?!
Miaka 60 iliyopita nchi nzima kulikuwa na hospitali za rufaa ngapi na Leo hii tunazo ngapi?!
Miaka 60 iliyopita palikuwa na vyama vya upinzani vingapi na leo vyama viko vingapi?!
CCM IMELETA MAENDELEO MAKUBWA SANA!
CCM HOYYEEEEEE!!
Naona CHAWA Tlaatlaah umeamua kuja kivingine na I'd mpya !!!
 
..kwa kweli Mzee Wassira amefifia kifikra.

..kama Katiba ni kitu kisichokuwa na maana kwa jamii kwanini Ccm iliandika Katiba mwaka 1977?
CCM Wanajua fika katiba ya wananchi itawaondoa madarakani ni swala la muda tu, jamii mafuvu yakirudishiwa akili katiba itapatikana tu

Huwezi kuwapumbaza watu muda wote, tena kwa kizazi hiki cha kidigitali ambacho kinaweza kutafuta taarifa sahihi na kuzitafakari Kwa kina
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesema kuwa serikali imetekeleza madai yote yaliyowasilishwa na vyama vya upinzani, ikiwemo maridhiano, kurejea kwa wanasiasa waliokimbilia uhamishoni, msamaha kwa waliokuwa gerezani, pamoja na kuruhusu maandamano na mikutano ya hadhara.

"Wapinzani wakiongozwa na CHADEMA walisema hali ni mbaya, wakataka maridhiano, wakataka waliokimbia warudi, wakarudi. Wakasema kuna watu 400 walioshtakiwa na kuhukumiwa mwaka 2020, utaratibu ukafuatwa wakaachiliwa kwa msamaha wa Rais kwa mujibu wa Katiba. Hilo nalo wakapata. Wakasema wanataka mikutano na maandamano, wakapewa, walikuja hata hapa Bunda na helikopta yao kwa sababu wanapenda sana show-off. Lakini nyinyi watu wa Bunda mkawasikiliza, hamna kitu!"

"Sasa kila mahali ni Katiba, Katiba, Katiba! Watu wana njaa, wanataka chakula, wanataka hospitali na elimu, wewe kila siku unasema Katiba! Watakula Katiba?" amehoji Wasira.
Kwa umri huo miaka 80 kukubali kuteuliwa na kutumwatumwa ni lazima uwe na njaa.
Aache watu wàpiganie haki zao siyo kuwanyima haki kisa wana njaa.
 
Back
Top Bottom