Pre GE2025 Mzee Wasira: Wananchi wana njaa, hawawezi kula Katiba

Pre GE2025 Mzee Wasira: Wananchi wana njaa, hawawezi kula Katiba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ulimwengu waleo unaongelea barabara kwamba ndo maendelea miaka 60 ya uhuru!
Nenda Kongo uone kama Wana barabara nzuri kama za kwetu!
Waulize madereva wa malori yanayokwenda Kongo barabara za Kongo zina hali gani?!
Hapo Kenya tu barabara nzuri zipo Nairobi na kidogo Mombasa lakini ukienda mikoa mingine hali ya barabara zinatisha!
Moja ya mambo ya kumshukuru Mungu kwa TZ ni neema ya amani na utulivu tulionao!
Tungekuwa katika vita ya wenyewe hata haya maendeleo ambayo nyinyi mnayaona ni kiduchu yasingekuwepo!
Wengi wetu muda huu tungekuwa kwenye kambi za wakimbizi sijui za nchi gani tukiwategemea UNHCR watusaidie unga wa mahindi ya njano na maharage!
CCM imeisha fanya maendeleo makubwa na bado inaendelea kufanya mambo makubwa.
Leo Mh Rais Samia akiwa Kariakoo kaahidi ndani ya kipindi kifupi kijacho kujenga soko jingine kubwa kama la Kariakoo maeneo ya jangwani, hayo yote ni maendeleo yanayoletwa na CCM.
CCM HOYYEEE!
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesema kuwa serikali imetekeleza madai yote yaliyowasilishwa na vyama vya upinzani, ikiwemo maridhiano, kurejea kwa wanasiasa waliokimbilia uhamishoni, msamaha kwa waliokuwa gerezani, pamoja na kuruhusu maandamano na mikutano ya hadhara.

"Wapinzani wakiongozwa na CHADEMA walisema hali ni mbaya, wakataka maridhiano, wakataka waliokimbia warudi, wakarudi. Wakasema kuna watu 400 walioshtakiwa na kuhukumiwa mwaka 2020, utaratibu ukafuatwa wakaachiliwa kwa msamaha wa Rais kwa mujibu wa Katiba. Hilo nalo wakapata. Wakasema wanataka mikutano na maandamano, wakapewa, walikuja hata hapa Bunda na helikopta yao kwa sababu wanapenda sana show-off. Lakini nyinyi watu wa Bunda mkawasikiliza, hamna kitu!"

"Sasa kila mahali ni Katiba, Katiba, Katiba! Watu wana njaa, wanataka chakula, wanataka hospitali na elimu, wewe kila siku unasema Katiba! Watakula Katiba?" amehoji Wasira.
Njaa ambayo chama chake kimekuwa madarakani tangu uhuru hakijaweza kuifuta, njaa mbayo amekuwa serikalini kwa zaidi ya miaka 30 hajaweza kuitatua.
 
Hahaha unamfananisha Trump na huyo dingi??
Kabla ya nchi yako haijapata uhuru 1961 alkuwepo awamu ya kwnz mpaka leo hii kawa dingilii
Kuna kitu gani kipya atafanya?!

HAKUNA!
Kwani Trump kaenda ikulu kufanya nini ambacho hakukifanya awamu iliyopita ?!
Mzee Wasira umri wake sawa na umri wa Trump .
Kitu ambacho Wasira anacho na Trump hana ni UZOEFU!.
Mzee Wasira kakaa serikalini kipindi kirefu na kwenye chama pia ana muda mrefu kwahiyo mzee ana uzoefu wa muda mrefu kwenye siasa ambao Mbowe na Lisu hawana uzoefu kama wa Mzee Wasira na ndio maana mnamuandama kwa sababu mnajua kile ni chuma Cha nguvu kwa uzoefu alionao chadema hamtoboi kwa sababu Mzee Wasira mbinu zote za ushindi anazijua!
 
Tanzania hii ukiongelea kuhusu KATIBA MPYA,tena mbele ya CCM unaonekana mvuruga amani wa nchi
 
CCM ukitaka kuwavuruga we waambie mambo ya KATIBA
Mtajivuruga wenyewe! CCM wana ilani ya uchaguzi inayowaongoza.
Hawafanyi kazi kwa mihemko na kelele za wapinzani haziwazuwii kuwatumikia wananchi ambao wana kiu ya maendeleo.
Hakuna mwananchi mwenye shida na katiba mpya!.
Wananchi shida yao ni umeme, maji, shule, barabara,hospitali na madawa yake na VIFAA tiba! Mazingira rafiki ya kujiongezea kipato pamoja na usalama wao na mali zao!
Hayo ndiyo mahitaji ya wananchi, ama hiyo katiba mpya ni hitajio la Lisu na heche.
 
Akili ishaliwa na kutu, ubongo chakavu unabubujikwa machozi.
Luka mkalishe Babu yako umshauri atafia jukwaani.
 
Kwani Trump kaenda ikulu kufanya nini ambacho hakukifanya awamu iliyopita ?!
Mzee Wasira umri wake sawa na umri wa Trump .
Kitu ambacho Wasira anacho na Trump hana ni UZOEFU!.
Mzee Wasira kakaa serikalini kipindi kirefu na kwenye chama pia ana muda mrefu kwahiyo mzee ana uzoefu wa muda mrefu kwenye siasa ambao Mbowe na Lisu hawana uzoefu kama wa Mzee Wasira na ndio maana mnamuandama kwa sababu mnajua kile ni chuma Cha nguvu kwa uzoefu alionao chadema hamtoboi kwa sababu Mzee Wasira mbinu zote za ushindi anazijua!
Aisee wewe ni mzee Wasira!
 
Aisee wewe ni mzee Wasira
😂😂😂😂😂😂😂
Yamekuwa hayo tena?!
Mimi hata kadi ya CCM sina wala siitaki kama ambavyo sihitaji kadi ya chama chochote!
Mimi nimeona chadema mnamuogopa sana mzee Wasira ndio maana mnamshambulia sana kama wahenga walivyosema kwamba
MTI WENYE MATUMDA..............................................!
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesema kuwa serikali imetekeleza madai yote yaliyowasilishwa na vyama vya upinzani, ikiwemo maridhiano, kurejea kwa wanasiasa waliokimbilia uhamishoni, msamaha kwa waliokuwa gerezani, pamoja na kuruhusu maandamano na mikutano ya hadhara.

"Wapinzani wakiongozwa na CHADEMA walisema hali ni mbaya, wakataka maridhiano, wakataka waliokimbia warudi, wakarudi. Wakasema kuna watu 400 walioshtakiwa na kuhukumiwa mwaka 2020, utaratibu ukafuatwa wakaachiliwa kwa msamaha wa Rais kwa mujibu wa Katiba. Hilo nalo wakapata. Wakasema wanataka mikutano na maandamano, wakapewa, walikuja hata hapa Bunda na helikopta yao kwa sababu wanapenda sana show-off. Lakini nyinyi watu wa Bunda mkawasikiliza, hamna kitu!"

"Sasa kila mahali ni Katiba, Katiba, Katiba! Watu wana njaa, wanataka chakula, wanataka hospitali na elimu, wewe kila siku unasema Katiba! Watakula Katiba?" amehoji Wasira.
Hahaha obsessed na chakula tu kwa anafikri kila mtu anafikiria tumbo tu na kande
 
Birthday ya Wasira makamu mwenyekiti wa CCM ni
1 July 1945,
Birthday ya Trump rais wa USA ni
14 June 1946.
Tafauti ya umri wa Trump na umri wa Wasira ni mwaka mmoja tu kwahiyo Donard Trump rais wa USA mwaka kesho atakuwa na miaka 80 sawa na mzee Wasira na Bado Trump ataendelea kuwa rais hadi 2029.
Nakusudia kusema kwamba :
IKIWA WASIRA HAFAI KUWA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM na TRUMP HAFAI KUWA RAIS WA USA.

Msikilize kwanza Makongoro Nyerere akikuoa historia ya Wassira kabla ya vita vya Kagera yupo, Mkapa anaingia madarakani yupo. Kikwete yupo, Magufuli yupo na sasa Samia yupo.

Trump alikuepo 2017 na amekuja baada ya miaka yake minne anaondoka. Msamiati wa kung'atuka ulikuwepo toka enzi za Nyerere Wassira hana. Wassira kukaa kwenye uongozi ndio mpango pekee uliokuwepo kichwani kwake.

Hawezi kuonyesha mapungufu ya serikali ys CCM kama mzee mwenye hekima jaji Warioba alivyosema kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa 2024. Wassira ni kusifia tu ili apate uhakika wa tumbo lake na uzao wake, nilifikiri anaweza muiga Warioba kutoka kwao Musoma kumbe hili zee la hovyo kuwahi kutokea CCM.

Nilichogundua huyu mzee ni zaidi ya chawa, huyu ni KUPE. Hatoki na haachii labda apigwe fumigation tena dawa kali, ningependekeza mheshimiwa Heche hebu mfanyie fumigation huyu mzee anawadhalilisha watu wa Musoma
 
CCM wanaiogopa KATIBA MPYA,maana wanajua ikibadilika na wao watakuwa WAPINZANI
Na chadema wanamuogopa mzee Wasira kwasababu kwa uzoefu alionao wa kukaa serikalini na kwenye chama muda mrefu , mbinu za ushindi zote anazijua kwahiyo imewauma sana kuona mzee kapewa nafasi muhimu kwenye chama kwahiyo chadema mnaweweseka kwa hofu ya kuogopa kishindo cha Mzee Wasira. Naamini mnajua kwanini rais Kikwete alimpa Mzee Wasira jina la TYSON!
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesema kuwa serikali imetekeleza madai yote yaliyowasilishwa na vyama vya upinzani, ikiwemo maridhiano, kurejea kwa wanasiasa waliokimbilia uhamishoni, msamaha kwa waliokuwa gerezani, pamoja na kuruhusu maandamano na mikutano ya hadhara.

"Wapinzani wakiongozwa na CHADEMA walisema hali ni mbaya, wakataka maridhiano, wakataka waliokimbia warudi, wakarudi. Wakasema kuna watu 400 walioshtakiwa na kuhukumiwa mwaka 2020, utaratibu ukafuatwa wakaachiliwa kwa msamaha wa Rais kwa mujibu wa Katiba. Hilo nalo wakapata. Wakasema wanataka mikutano na maandamano, wakapewa, walikuja hata hapa Bunda na helikopta yao kwa sababu wanapenda sana show-off. Lakini nyinyi watu wa Bunda mkawasikiliza, hamna kitu!"

"Sasa kila mahali ni Katiba, Katiba, Katiba! Watu wana njaa, wanataka chakula, wanataka hospitali na elimu, wewe kila siku unasema Katiba! Watakula Katiba?" amehoji Wasira.
Hili lizee ni gari bovu.
 
Back
Top Bottom