Mzee Yusuph aamua kuachana na muziki na kumrudia Mungu wake

adden

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
7,033
Reaction score
15,638
Habari za jioni wanajamvi.

Taarifa nilizozipata punde zinasema mfalme huyo wa taarabu anaacha rasmi mziki huo na kumrudia mungu.
Mungu amjaalie wepesi afanikiwe katika dhamira yake

UPDATES;

Mzee Yusuph ameamua kuachana ma Muziki na kumrudia Mungu wake na amewataka watu wote wamsamehe ili apate msamaha kwa Mola wake.

Mzee Yusuph Ameapa kuto kujihusisha na Muziki na kutaka Nyimbo zake zisipigwe tena kwenye Media zote. Mzee Yusuph alionekana analia kwa uchungu katika msikiti wa Bongoni Ilala na kujutia yale aliyokuwa akiyafanya enzi za Ujahili wake.

Assalaamu alaykum warahmatullahi wabarakaatuh

BREAKING NEWS

Aliyekuwa Mfalme na gwiji wa muziki wa taarabu Afrika mashariki MZEE YUSUF ameamua kuachana na mziki na kumrudia Allah.

Mzee Yusuf ametangaza Nia yake hiyo leo ijumaa tarehe 12-08-2016 Muda mfupi baada ya kumaliza kuswali swala ya ijumaa ktk msikiti wa ilala bungoni (Masjid Taqwa)

Alizungumza huku akibubujikwa na machozi mengi Mzee Yusuf amemuomba Allah amsamehe madhambi yake yote pamoja na kuwaomba waumini wote wamuombee msamaha kwa Allah. Kadhalika amewaomba wanamuziki wengine ambao ni waislamu kuachana na muziki na kuzitumia fani zao walizonazo ktk kutangaza na kusifia Shamaail za bwana mtume muhammad (s.a.w).

Gwiji huyo wa zamani wa taarabu amewaomba watu wote waliokuwa na Cd zake majumbani mwao kuacha kupiga nyimbo zake na wakikaidi wafahamu madhambi yote yatakuwa juu yao kwani yeye hivi sasa anafanya toba kwa Allah.

Pia amevitaka vituo vyote vya televisheni na redio kuacha kupiga nyimbo zake kwani yeye Hana dhimma hiyo Tena. Ikumbukwe hali kama hii ilishawahi kutokea kwa aliyekuwa msanii wa bongo fleva SUMA LEE kuamua kuachana na mziki na sasa ni mpenzi mkubwa wa mtume muhammad (s.a.w)

Yaa rabbi awape tawfiiq wanamuziki wote wa kiislamu waachane na muziki pamoja kutupa mwisho mwema wao pamoja nasi in shaa Allah.

Hakuweza kuendelea kuongea zaidi ya maneno hayo na kuangua kilio kilichomsababishia maneno kutoweza kutoka mdomoni mwake.
 
Kha ametajirika anaona taarabu haina deal, akifilisika asirudi tena kwenye gemu, tatizo ili nyimbo zao ziheat wanashinda kwanza kwa waganga, ndo maana analia, I thank God huwa sisikilizi ma nyimbo yao ambayo mpaka wakazindikwe kwanza ndo watoe.
 
Aiseeee, basi poa kama ni kweli.
IMG_0115.JPG
 
Back
Top Bottom