Mzee Yusuph: Maisha yangu yamekuwa magumu baada ya kuacha muziki

Ni bahati mbaya kwamba wengine tunadandia Maandiko Matakatifu kwa mbele.Mungu anaposema hayo juu ya kujikana hamaanishi kuacha kujishughulisha kwa ajili ya mahitaji ya uzima Wa kimwili.Uzima Wa kimwili na kiroho ni vitu vinahitajiana.Na mwishoni mwa nyakati miili ya wote waliokwisha kulala mauti itafufuliwa ili iungane na Roho ama iwe kufaidi uzima au Moto Wa Milele.Kwa hiyo kujipatia ridhiki kwa njia halali sio dhambi na wala huo sio msalaba.

Mzee Yusufu mimi sielewi kwa nini aliacha mziki.Mziki sio dhambi.Mziki ni kistarehesho cha akili.Akili ndio Engine ya mwili na nafsi.Ikiwa Yusufu aliacha mziki kwa sababu za kiafya au kustaafu tu au sababu nyingineyo nje ya kuona kwamba alikuwa anafanya kazi ya "kikafiri" sioni issue katika suala lake.Ila kama alishauriwa kuwa kazi aliyokuwa anaifanya ingempeleka jehanamu basi alikuwa ameingizwa mkenge.Dhambi huja tu pale mhusika anapotumia kazi hiyo kuwaletea watu wengine ama yeye mwenyewe madhara kwa makusudi.Kwa mfano Yusufu katika kupiga Taarabu angekuwa anawauza watazamaji kwa ngono hiyo ingemsabibishia Yusufu dhambi.Ni Yusufu pekee anakuwa na dhambi tu na wala sio Taarabu yenyewe(fani),vyombo vya mziki anavyotumia na/au ukumbi wenyewe Wa mziki.Kwa Wakiristo wataelewa hili suala vizuri.Yesu alipowachapa wale Wayahudi waliokuwa wanafanya biashara ya kuuza njiwa Kanisani aliwachapa wauzaji tu na wala hakukataza watu wasiendelee kuuza njiwa na/au hakubomoa hekalu ambamo biashara ile ilikuwa inafanyika.Vitu hawezi kutenda dhambi na haviwezi kuwa na dhambi baada ya mtumiaji kuvitumia kutekeleza dhambi husika.

Na hata kama Yusufu alikuwa nyimbo za maudhui mabaya dhambi inakuwa kwake lakini wimbo au madhui yenyewe haviwezi kuadhibiwa.

Kwa hiyo Yusufu iwapo anaona mambo "yanabana" kivile arudi tu apige kazi.Kwa mziki wake watu wengine walikuwa wanapoteza stress.Wengine walikuwa wanapata uhai mpya Wa kiakili na kimwili na hivi kufanya kazi kwa nguvu tena baada ya uchovu.Kwa mziki wake alikuwa anawasaidia wenye ndoa kuburudika na hivi ku-extend lifespan ya ndoa zao.Kwa mziki wake nchi ilipata kodi.Kwa kodi wagonjwa walipata dawa hospitalini.Watu walilipwa mishahara kwa mziki.Wanafunzi walisoma kwa mziki wake na msururu kibao Wa manufaa.

Kwa hiyo ikiwa watu walikuja "kumtongoza" kuwa angeenda mtoni kwa mziki wake basi huyo aliingizwa chaka.Ataenda Motoni kwa matendo yatokanayo na fani husika ikiwa hakutumia akili kuchenjua mabaya na mema.
na kama aliroga na kuwafanya watu misukule hapo asitubu?
 
Kila atakaekunifuata, ajikane mwenyewe, aubebe msalaba wake anifuate..

Itamfaidia nini mtu akiupata ulimwengu wote akaukosa uzima wa milele na nafsi yake kupotea?

Hayo ni maneno ya kwenye Biblia

Hayo maneno alisema allah? allah ni Mungu? Wapi alaah alisema hivyo?
 
Mwongo mkubwa anazurura huku mikoani akitoa mihadhara ndani ya Benz kali anakula dhakat ya waarabu waliomsimamisha kuimba
 
HIVI MZEE WW NI WA KULALAMIKA? MTU SHOW MOJA ULIKUWA UNAPIGA MAMILIONI? GARI KALI ULIZOKUA NAZO VEPE
Majumba ya kifahari, mtu ulikua unaenda USA, UK na DUBAI every time
Hadi watu wakaanza kukilinganisha na kina kiba na mondi kwa pesa
Leo ndo imekua hivyo daaaah
Hakuna wasanii walikua wanalipwa vizuri kama wa bendi yake alikua anawalipa vizuri ile mbaya wengi wamejenga kupitia bend yako.pesa ilikua ndefuuu mpk mwez wa ramadhan wasanii wanapewa fungu la ukweli leo ndo mzee yusuf unalia so sad!
 
Mzee alikua na hela mkwanja mrefuu kinoma asikwambie mtu
Hivi wasanii huwa hawaweki akiba?alikua milionea
 
Ni bahati mbaya kwamba wengine tunadandia Maandiko Matakatifu kwa mbele.Mungu anaposema hayo juu ya kujikana hamaanishi kuacha kujishughulisha kwa ajili ya mahitaji ya uzima Wa kimwili.Uzima Wa kimwili na kiroho ni vitu vinahitajiana.Na mwishoni mwa nyakati miili ya wote waliokwisha kulala mauti itafufuliwa ili iungane na Roho ama iwe kufaidi uzima au Moto Wa Milele.Kwa hiyo kujipatia ridhiki kwa njia halali sio dhambi na wala huo sio msalaba.

Mzee Yusufu mimi sielewi kwa nini aliacha mziki.Mziki sio dhambi.Mziki ni kistarehesho cha akili.Akili ndio Engine ya mwili na nafsi.Ikiwa Yusufu aliacha mziki kwa sababu za kiafya au kustaafu tu au sababu nyingineyo nje ya kuona kwamba alikuwa anafanya kazi ya "kikafiri" sioni issue katika suala lake.Ila kama alishauriwa kuwa kazi aliyokuwa anaifanya ingempeleka jehanamu basi alikuwa ameingizwa mkenge.Dhambi huja tu pale mhusika anapotumia kazi hiyo kuwaletea watu wengine ama yeye mwenyewe madhara kwa makusudi.Kwa mfano Yusufu katika kupiga Taarabu angekuwa anawauza watazamaji kwa ngono hiyo ingemsabibishia Yusufu dhambi.Ni Yusufu pekee anakuwa na dhambi tu na wala sio Taarabu yenyewe(fani),vyombo vya mziki anavyotumia na/au ukumbi wenyewe Wa mziki.Kwa Wakiristo wataelewa hili suala vizuri.Yesu alipowachapa wale Wayahudi waliokuwa wanafanya biashara ya kuuza njiwa Kanisani aliwachapa wauzaji tu na wala hakukataza watu wasiendelee kuuza njiwa na/au hakubomoa hekalu ambamo biashara ile ilikuwa inafanyika.Vitu hawezi kutenda dhambi na haviwezi kuwa na dhambi baada ya mtumiaji kuvitumia kutekeleza dhambi husika.

Na hata kama Yusufu alikuwa nyimbo za maudhui mabaya dhambi inakuwa kwake lakini wimbo au madhui yenyewe haviwezi kuadhibiwa.

Kwa hiyo Yusufu iwapo anaona mambo "yanabana" kivile arudi tu apige kazi.Kwa mziki wake watu wengine walikuwa wanapoteza stress.Wengine walikuwa wanapata uhai mpya Wa kiakili na kimwili na hivi kufanya kazi kwa nguvu tena baada ya uchovu.Kwa mziki wake alikuwa anawasaidia wenye ndoa kuburudika na hivi ku-extend lifespan ya ndoa zao.Kwa mziki wake nchi ilipata kodi.Kwa kodi wagonjwa walipata dawa hospitalini.Watu walilipwa mishahara kwa mziki.Wanafunzi walisoma kwa mziki wake na msururu kibao Wa manufaa.

Kwa hiyo ikiwa watu walikuja "kumtongoza" kuwa angeenda mtoni kwa mziki wake basi huyo aliingizwa chaka.Ataenda Motoni kwa matendo yatokanayo na fani husika ikiwa hakutumia akili kuchenjua mabaya na mema.
Muziki si dhambi kwa imani unayoiamini wewe au imani anayoaminj mzee yussuf?
 
Arudishe milion 25 za watu,aache kumsingizia Allah.
 
Aweke namba yake ya Tigo Pesa tumchangie Maalim wetu.
 
Back
Top Bottom