Mzizi wa fitna: Pacome vs Chama, nani zaidi?

Dong Jin

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2018
Posts
968
Reaction score
2,034
... 🔖 𝙉𝘼𝙉𝙄 𝙕𝘼𝙄𝘿𝙄 ?

Baada ya ushindi wa Simba (6-0) dhidi ya Jwaneng nimeona mijadala mitandaoni watu wakibishana nani zaidi kati ya Chama na Pacome ?! Nami nimeona nisipitwe na mjadala huu. Kama kawaida yangu huwa naongea na takwimu kisha nawaachia mchambue wenyewe kama hivi ;

𝘾𝙃𝘼𝙈𝘼 𝙋𝘼𝘾𝙊𝙈𝙀
_________________________________________
15 ......... Michezo ligi kuu ........... 15
6 .... Michezo group stage CAF-CL ..... 6
4 ............ Magoli ligi kuu .............. 6
3 ........... Assists ligi kuu .................... 3
1 ............ Magoli CAFL-CL ............ 3
1 ............ Assists CAF-CL ................... 2
5 ......... Magoli yote ya msimu ..... 9
4 ......... Assists zote za msimu ......... 5

CAF champins league group stage !

𝙋𝙖𝙘𝙤𝙢𝙚 𝙕𝙤𝙪𝙯𝙤𝙪𝙖 ;

1 ◎ ⚠️ vs CR Belouizdad 🇩🇿
2 ◉ ⚽ vs Medeama 🇬🇭
3 ◉ ⚽ vs Al-Ahly 🇪🇬
4 ◉ ⚽ + 🎯 vs Medeama 🇬🇭
5 ◉ 🎯 vs CR Belouizdad 🇩🇿
6 ◎ ⚠️ vs Al-Ahly 🇪🇬

𝘾𝙡𝙖𝙩𝙤𝙪𝙨 𝘾𝙝𝙖𝙢𝙖 ;

1 ◎ ⚠️ vs ASEC Mimosas 🇨🇮
2 ◎ ⚠️ vs Jwaneng 🇧🇼
3 ◎ ⚠️ vs Wydad Athletic 🇲🇦
4 ◎ ⚠️ vs Wydad Athletic 🇲🇦
5 ◎ ⚠️ vs ASEC Mimosas 🇨🇮
6 ◉ ⚽ + 🎯 vs Jwaneng 🇧🇼

Key 🔑
__________
🎯 — Assists
⚠️ — Hakuna goli wala Assist

C&P
 
Mtamlinganisha Chama na kila mtu, ila Chama atabaki kuwa Chama..

He has been consistent for more than five years. Leta orodha ya wafungaji wa muda wote wa CAFCL. Utamuona wa saba pale juu.

Pacome yu wapi? Leta takwimu za miaka yote na siyo za mwaka huu pekee, utajinyea ukiziangalia.
 

Kwanini tulete takwimu ya miaka ya nyuma wakati kwasasa wote wanakipiga kwa pamoja? NBC wote wapo na champions league wote wapo. Tunalinganisha kwasasa sio yaliyopita
 
Kwanini tulete takwimu ya miaka ya nyuma wakati kwasasa wote wanakipiga kwa pamoja? NBC wote wapo na champions league wote wapo. Tunalunganisha kwasasa sio yaliyopita
Kuna tofauti ya form na class, Ili pakome awe class ya Chama anatakiwa kuyafanya haya Kwa miaka mingi Kama mitano. Binafsi Kwa form ya pakome ya Sasa anamzidi Chama ila still hapaswi kufananishwa na Chama angalau ayafanya haya Kwa miaka kadhaa. Form is temporary na class ni permanent
 
Chama kaanza vitu vyake enzi zile za Nkana pale kwa Mkapa, akatoka pale akaenda kwa As Vita, wakati huo vyura mnaogelea tu kwenye tope hata CAF CL hamuijui ina rangi gani..

Huyo Pacome wenu wakati huo alikuwa anakunywa uji wa mama yake kwao Ivory Coast.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
✅✅✅
 
Kama Chama ana class kwanini hakuna timu yeyote ile inayomuhitaji? Katoka Berkane karudi Simba na hapandi daraja ya kutakiwa na timu nyingine za daraja la juu?

Kwasasa kila mwana Yanga anaingia mashaka, huenda Pacome akakosekana msimu ujao. Na hili nakuhakikishia Pacome akiendelea na performance yake hiyo hiyo hatobakia Yanga msimu ujao ila Chama utasikia tetesi zake za kutakiwa na Yanga pekee basi.
 
Kama Chama ana class kwanini hakuna timu yeyote ile inayomuhitaji? Katoka Berkane karudi Simba na hapandi daraja ya kutakiwa na timu nyingine za daraja la juu?...
Ukweli mchungu
 
Ni mjinga tu ndo anayeweza kumfananisha Pacome na Chama.

Hata mashabiki wenyewe wa simba ukiwaekea kati ya Pacome na Chama wachague mmoja ki uhalisia hawawezi kumchagua Chama.

Pacome kila mechi anapafomu yupo katika kiwango bora kabisa.

Chama baada ya mechi ya jana ndo wanaanza kumfananisha na Pacome, kwanini isiwe mechi za nyuma?

Kwasasa huwezi kumfaninisha Chama na Pacome.

Ni kumuonea tu Chama.

Mengine yatabaki kuwa ushabiki.
 
Kama Chama ana class kwanini hakuna timu yeyote ile inayomuhitaji? Katoka Berkane karudi Simba na hapandi daraja ya kutakiwa na timu nyingine za daraja la juu...
Nyie utopenga kila msimu mnamtolea macho[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Chama ana faa kwa aina ya soka letu la taratibu na madoido ndani yake, Pacome anacheza soka la kisasa lenye mahitaji ya ufundi, nguvu na Kasi.

Hii inapelekea Chama kushindwa kuendana na soka la Kasi kule kaskazini ila akija uku kwetu ni mfalme.
Pacome ni Ngumu msimu ujao kuendelea kucheza kwetu kwakua ufundi,nguvu na Kasi vinamfanya achukuliwe na klabu kubwa za kaskazini au kwingineko.
 
Kwakuwa mpira unachezwa hadharani, currently PACOME kulinganishwa na Chama ni kutokujua sayansi ya mpira na ni kumkosea heshima PACOME

Chama anaibuka mechi moja tu tena ya vibonde alafu mnaleta kelele nyingi.
 
Chama fundi wa mpira.. Ubora wake unadhihirika misimu kadhaa sasa, Pacome ni mchezaji mzuri pia tumpe muda tuone ubora wake ukizingatia ndio msimu wake wa kwanza pale Yanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…