"Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji

"Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji

Halima Mdee amesema hadharani kuwa wamepata baraka za Chama chini ya uongozi wa Mbowe. Lakini, Mbowe hajatoka hadharani kukanusha hilo. Kwahiyo, simple logic ni kuwa Mbowe anaunga mkono wabunge hawa kuapishwa.

Mengine yanayoendelea ni kuwalaghai tu wanaharakati. Ni sawa na kumuahidi mtoto peremende ili aache kulia.
Kama kauli yake ni ya kweli mbona ametoroka kikao?

Inshort waje kwenye kikao ama wasije tunafukuza waje kuungana na mataga hapo Lumumba.
 
Naona umeamua kujivua akili kabisa, aliyekwambia wanaenda kufukuzwa ni nani? Wale waliitwa kuhojiwa sio kuvuliwa uanachama, pili kwanini huoji kupatikana kwao kama kulifuata taratibu zote za kichama ila unahoji wao kuitwa tu? Hivi ukiwa ccm lazima kutetea kitu hata kama sio cha haki? Unanajisi taasisi zile zote ulizopitia kielimu
Huyo siku hizi kapoteza uelekeo, nadhani yuko obsessed na kupata kauteuzi ka kuzeekea nako. Hatuko focused kama zamani.
 
Ila kwa Mdee kazi wanayo. Zitto aliwatikisa , Dr Slaa alijiondoa mwenyewe lakini kwa Mdee na kwa Chadema hii ilivyo disorganised watanyooshwa.

Uongozi ungekutana na hawa wanawake nje ya vikao rasmi ili kujadiliana bila kupasua chama. Bado wote wanahitajiana hakuna haja ya ubabe hasa nyakati hizi.
 
Halima Mdee amesema hadharani kuwa wamepata baraka za Chama chini ya uongozi wa Mbowe. Lakini, Mbowe hajatoka hadharani kukanusha hilo. Kwahiyo, simple logic ni kuwa Mbowe anaunga mkono wabunge hawa kuapishwa.

Mengine yanayoendelea ni kuwalaghai tu wanaharakati. Ni sawa na kumuahidi mtoto peremende ili aache kulia.
Mbowe anajua misimamo ya akina Lissu lakini pia bila ruzuku ataendesha vipi chama? Hao wapiga kelele wanachangia nguvu tu sio pesa! He is playing very smart.
 
Wewe Paskali nakuambiaga njaa na kujipendekeza ndio vinavyokusumbua. Huna moral authority ya kuzungumzia hili la kina Halima Mdee.

CHADEMA kama chama hakitambui uchaguzi na urudiwe, hivyo viti 19 vya kazi gani? Unata wakubaliane na huo ulaghai ili uchaguzi uhalalishwe? Ubongo wako umekwama sana.
 
Back
Top Bottom