Huu ni msemo wa Kiswahili kuwa Mzoea Vya Kunyonga, vya kuchinja haviwezi! Chadema ilizoea kuwanyonga wanachama wake kwa kuwafukuza kienyeji enyeji na kujinga jinga, nimeisoma taarifa hii kwa faraja.
Halima Mdee ni mwanamke shujaa, msomi na mwanasheria, anaijua katiba ya Chadema, na vikao vya mamlaka ya nidhamu ni kama ifuatavyo.
- Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, ili kumvua mtu uanachama kuna mlolongo wa kanuni na taratibu za kufuatwa na miongoni mwake ni hizi nitakazo ziorodhesha hapa chini, jee zilifuatwa?
- Kuandaa Hati ya Mashtaka kwa maandishi yenye tuhuma zote ambazo mtuhumiwa anakabiliwa nazo. Jee hati hizi za mashitaka kimaandishi ziliandaliwa?
- Hati hiyo ya mashitaki kimaandishi inatakiwa ikabidhiwa kwa mtuhumiwa kwa "despatch" ili kuthibitisha imemfikia. Je, hili lilifanyika? Nimesikia kuna watu waliitwa kwa simu, je huu ndio utaratibu kwa jambo zito kama hili?
- Mtuhumiwa atatakiwa kuzijibu tuhuma za mashitaka hayo ndani ya kipindi cha siku 14 tangu tarehe aliyopokea barua ile ili apate muda wa kutosha kutafakari, je hili litafanyika?
- Baada ya majibu ya hati ile ya mashitaka kurejeshwa, ndipo mamlaka ya nidhamu ingepaswa kuitisha kikao rasmi kwa mujibu wa katiba na kumwalika mtuhumiwa kwa barua ili kuwapa nafasi ya kujieleza na kumsikiliza kabla ya kufikia maamuzi!. Jee this time Chadema itafuata taratibu?
Halima na genge lake they are very right, Chadema ilizoea kufanya mambo kienyeji, leo imekutana na kisiki cha mpingo!
Chadema sasa lazima ijifunze kufanya mambo kwa kufuata katiba yake, sheria, taratibu na kanuni!, kufanya mambo kwa kienyeji enyeji kwa mtindo wa zimamoto, sasa basi!
Hongera sana Kamanda Mhe. Halima Mdee na makamanda makomandoo wa kike kwa kuifunza nidhamu chama chenu cha Chadema.
Paskali