"Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji

Paskal mayala kaenda kwa mdee kuchukua pesa eti aje kuwatetea mitandaoni njaa mbaya sana
 
Waliosema samaki hukunjwa angali m'bichi hawakukurupuka wajomba..

Haya sasa lisamaki limeshakauka hilo hapo mkunje kama anakunjika tena.. Too late.
 
Hawatakiwi kwenda kwa sababu hawatatendewa haki. Tayari ishara za kutokutenda haki zinaonekana.
Wao wasiwe watabiri huko Bungeni mbona hawakutabiriwa walikwenda kama wachawi , nasikia juzi makada wa CCM walijilia mmoja wamepata wachumba wapya ccm hata Paskal mayala kalala kwa mdee ndiyo maana kaamua kuja na uzushi wake uliojaa mifano ya kipumbavu mitupu
 
Mbowe siyo CHADEMA
 
Chadema wakubali yaishe. Walishiriki uchaguzi ili wapate kura .Wamepata wabunge 20.Si haba wawape ushirikiano wawashe moto bungeni. Waendelee kujenga chama. Na waongee hoja bungeni. Maana huku nje wakiongea wanaitwa wachochezi.

Umenena logic sana mdogo wangu!
Wenyehekima watayaishi maono yako!
Hao watu ni wazuri kufikisha hoja za wananchi na kujadili mstakabali wa Taifa.

Sisi kama wanachama hatuo sababu ya kuendeleza malumbano yasiyo na tija.
Siasa ni ujira na wao washaula. Tuache roho za korosho
 
Roho za korosho wanazo akina Mdee waliopora ubunge kwa njia za kihuni na kuwaacha list husika iliyokuwa imepitishwa na kamati kuu
 
Kuna kitu kinaitwa pyrrhic victory.

Tuseme wakashinda yote hayo unayosema na wakabaki kuwa wabunge kwa juhudi za makada wa CCM na viongozi wa serikali watakuwa kweli na legitimacy ya kujiita wapinzani mbele ya kadamnasi? Baada ya miaka mitano kumalizika watarudi tena kuomba uteuzi wa chama chao walichokipigania kwa damu na machozi ili wapewe dola na kama itashindikana waweze kuisimamia serikali?

Mtu shupavu na mwenye mapenzi na chama chake angeendelea kupigania msimamo wao ndani ya chama chao. Hizo nafasi zingebaki wazi maana Spika na NEC hawana mamlaka ya kuteua watu kutoka kwenye vyama vingine. Kwa kufanya walivyofanya wameonyesha umma kuwa wao wanajiona wako juu ya chama chao kwa kuamini kuwa hamna ambacho wanaweza kufanywa. Aidha, wamewapora wanachama wenzao wa kike ambao walipigania nafasi hizo na walishinda na hivyo walistahili uteuzi kuliko baadhi ya hili genge.

Kwa kusema ukweli wameonyesha umimi uliopitiliza na wakae wakijua kuwa wale wanaowakumbatia wakati huu watawatema pale watakapoacha kuwahitaji. Na itakapotokea hivyo, hamna ambae alikuwa pamoja nao kwa hali na mali wakati wakipambana kutetea maslahi ya wananchi atakaewaonea huruma. Miaka mitano sio mirefu sana.

Amandla...
 
Chadema wakubali yaishe. Walishiriki uchaguzi ili wapate kura .Wamepata wabunge 20.Si haba wawape ushirikiano wawashe moto bungeni. Waendelee kujenga chama. Na waongee hoja bungeni. Maana huku nje wakiongea wanaitwa wachochezi.
CHADEMA wao wanajiona ndio machampioni wa haki za wanawake mpaka katika ilani waliwawekea kipengele cha kuwafunga jela waume halali wa ndoa kwa hoja kuwa wanabaka wake zao. Wawaache wakapiganie hizo haki za wanawake bungeni
 
Huu ni uchochezi kusema kweli. Hivi kwa nini watu hipenda nyumba ya jirani isiwe na amani au isiendelee?
Kama utaratibu umekiukwa na katibu mkuu kasimamia hii hoja ya ukiukwaji huo si ingekuwa jambo jema kujenga hoja kuwa utaratibu haukukiukwa kwa vigezo halali?
 
CHADEMA wao wanajiona ndio machampioni wa haki za wanawake mpaka katika ilani waliwawekea kipengele cha kuwafunga jela waume halali wa ndoa kwa hoja kuwa wanabaka wake zao. Wawaache wakapiganie hizo haki za wanawake bungeni
Haki za wanawake zipiganiwe na list ya wanawake waliokuwa wamepitishwa na kamati kuu siyo hiyo list ya kugushi iliyotengenezwa na mdee kihuni
 
CCM inafagilia ukiukaji wa taratibu huko chadema ili kesho waje kusema chadema inaendeshwa kihuni katibu mkuu hana nguvu yupo chini ya Bawacha, kutetea uvunjifu wa Kanuni ni upumbavu ulioje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…