Mzozo wa DRC: Waasi wa M23 watangaza Kusitisha Mapigano kwa 'Sababu za kibinadamu'

Mzozo wa DRC: Waasi wa M23 watangaza Kusitisha Mapigano kwa 'Sababu za kibinadamu'

M 23 wametangaza asubuhi hii kwamba watasitisha mapigano kwa muda ili watu walioathirika na vita waweze kupata msaada.
Kuanzia leo tarehe 4 watasitisha mapigano.
Hata hivyo, wanasema watakuwa macho ( alert) kuhakikisha jambo lolote baya halitokei.
Amani ya kweli itapatikana meza ya mazungumzo na siyo uwanja wa vita. Hongera kwa Dr. SAMIA na Dr. RUTO kwa kuandaa mkutano wa kuwapatanisha Tshisekedi na Kagame siku ya Jumamosi hapa Dar
 
Naona Rwanda kanusa kuvamiwa na wanajeshi wa jwtz anajitoa haraka ili tukiingia tuonekane wakorofi!!

Wanajeshi wetu wawili Kagame atalipa gharama kubwa Sana
Hahaha! Watanzania kwa kulitukuza jeshi letu hatujambo. Kama kuna taasisi serikali inapaswa kuitunza kwa wivu na ujivuni basi ni JWTZ sababu ni very professional na inapendwa na kuaminiwa mno na raia.
 
Waburundi wamewamaliza. Wamewaua kama nzige jamaa yangu kaniambia.
Ilikuwa waungane na waasi wa Burundi ambao mlima wao upo karibu na Bukavu.
Sasa inasemekana huku ni kwa Wabongo waliosaini SGR ya Uvinza na waburundi na wachina..
Hiyo nimepewa na mtu wa ndani Burundi
Kuna jamaa nilimueleza juzi kuhusu jeshi la Urundi akanibishia mbaya kigezo chake Burundi hawawezi ni masikini sanaa, nikaamua nikae kimnyaaa na burundi yenyewe si unajua ni mtoto wetu pendwa?

Kilochotokea ni kwamba Bongo haina bifu la moja kwa moja na Mrefu ila mrefu ndio ana choko choko kwahiyo Bongo iliamua kumlisha Mrundi data zote,

Basi last born wetu Urundi akakiwasha na akapita na biti mule mule🤣🤣
 
Kagame anaposema hajui kama wanajeshi wake wapo congo anazuga au vipi, inakuaje amiri jeshi mkuu asijue wanajeshi wake walipo? Halafu hao waasi wa congo kusitisha mapigano baada ya kuteka maendo ni kwamba wasifurushwe au wanazuga ili wajipange vema kuteka maeneo mengine zaidi? Hii ni zuga tu
 
Kuna jamaa nilimueleza juzi kuhusu jeshi la Urundi akanibishia mbaya kigezo chake Burundi hawawezi ni masikini sanaa, nikaamua nikae kimnyaaa na burundi yenyewe si unajua ni mtoto wetu pendwa?

Kilochotokea ni kwamba Bongo haina bifu la moja kwa moja na Mrefu ila mrefu ndio ana choko choko kwahiyo Bongo iliamua kumlisha Mrundi data zote,

Basi last born wetu Urundi akakiwasha na akapita na biti mule mule🤣🤣
Mkuuu nataman kuelewa vizuri ila sijui niko nyuma ya saa....kunani? Nieleze kidogo
 
Muungano wa makundi ya waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametangaza usitishaji mapigano wa kibinadamu kuanzia Jumanne.

Katika taarifa, kundi hilo - linalojumuisha waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda - lilitaja "sababu za kibinadamu" za kusitisha mapigano, baada ya kuteka maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo.


Umoja wa Mataifa umesema takriban watu 900 wameuawa na wengine 2,880 kujeruhiwa katika mapigano ya hivi majuzi katika na karibu na Goma, mji mkubwa wa mashariki mwa DRC, baada ya kutekwa na waasi.

Mataifa ya G7 na EU yamelaani mashambulio hayo kama ukiukaji wa wazi wa uhuru wa DR Congo.

Muungano wa makundi ya waasi - unaojulikana kama Muungano wa Mto Congo - umeshutumu jeshi la Kongo (Congo River Alliance) - kwa kuua watu wakitumia ndege kupiga mabomu maeneo wanayoshikilia.

Pia soma: Rais Samia kuwa mwenyeji wa mkutano wa marais wa nchi za SADC na EAC kujadili Mgogoro wa DR Congo

Iliongeza kuwa haina nia ya kunyakua eneo lolote zaidi, licha ya kusema vinginevyo wiki iliyopita, na itashikilia misimamo yake.

Katika taarifa, muungano huo ulisema: "Tunasisitiza dhamira yetu ya kulinda na kutetea raia na nafasi zetu."

Mapigano ya kikanda yameshuhudia mamia ya maelfu ya watu wakihama makazi yao katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Tangu kuanza kwa 2025, zaidi ya watu 400,000 wamelazimika kutoka kwa makazi yao, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi.

Rais wa Rwanda Paul Kagame - ambaye pia ni kamanda mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda - alisema hajui kama wanajeshi wa nchi yake walikuwa nchini DRC

"Kuna mambo mengi sijui. Lakini ukitaka kuniuliza, kuna tatizo nchini Congo linaloihusu Rwanda? Na kwamba Rwanda ingefanya lolote kujilinda? Ningesema 100%," aliiambia CNN siku ya Jumatatu.
Kagame kaogopa vikwazo
 
Habari wakuu

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wanaingia Congo wanateka miji na maeneo yenye utajiri wa dhahabu.

Congo ni kubwa mara 50 ya Rwanda

Je ni kitu gani kinaikwamisha Congo kuivamia Rwanda ili isiendelee kuvuruga amani nchini humo yaani kukabia mbele

Naomba kujuzwa
 
"BREAKING: Kagame withdraws troops after SA Allegedly Threatens to Use Long Range Ballistic Missiles, Deploy Navy Seals and Commando Units
President General Kagame has issued an executive order directing all Ruwandan military forces to withdraw from all DRC border towns and regroup in the capital Kigali with immediate effect"
The conflict should not be frozen but it should be resolved categorically ! Freezing of conflict is the wastage of resources. All involved parties should resolve this conflict by any means possible although negotiation is preferred. Anyone pretending is not involved in the conflict should be dealt with as he or she is trying to freeze the conflict. Niongeze nini sasa nieleweke!!!.
 
Back
Top Bottom