hahaaa, mimi sikusoma mzumbe secondary, ila nimesoma Mzumbe chuo, sekondari nimesoma ilboru form 1 hadi 6, nimevutiwa na hii thread kwa kuwa kipindi kile mzumbe na ilboru tulikua wapinzani wa jadi, enzi shule za vipaji zikiwa ndio vinara kwenye matokeo ya form 4 na 6 kabla private hawaja take over,
ile obsession na rivalry kati ya school hizi nimeimiss kweli, kibaha nao walikuwepo.
ila naona kama serikali imeshindwa kuzi update ili kuendana na ukisasa wa shule za sasa hivi zinazofanya vizuri,
maabara za kizamani na majengo yamechakaa, miundombinu za maji pia ni shida
mara ya mwisho kwenda ilboru naona wamejitahidi kwenye majengo kukarabati ila mzumbe bado,
sasa hivi ni kama watoto wa masikini ndio wanaosoma pale sababu ya mazingira mabovu, hakuna ile pride ya zamani tena.. inasikitisha