Mzungu akisaidiwa, humtaja aliyemsaidia na kumshukuru hadharani. Mswahili huishia kusema Mungu umenisaidia

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Najiuliza hivi kwanini mtu akiwa shidani, wa ngozi nyeupe, ukimkwamua shidani mwake, atakushukuru sana na hatoona aibu kusema hadharani, fulani kanisaidia.

Lakini sasa sisi kina Mtokambali, ukisaidia na fulani, humtaji, hata ukiulizwa ile shida yako umeitatuaje? Unaishia kusema ni Mungu amenisaidia.

Hivi Waswahili, kwanini tuko hivi? Je, hii ndio roho yenyewe ya uchawi ya kutaka wengine wenye shida kama yako waendelee kutabika bila msaada? Au sisi ndio tuko karibu sana na Mungu kuliko wazungu?
 
Mkuu ww km unauwezo wakusaidiaa ww saidiaa tu .MUNGU atakulipiaaa
 
Sifa na utukufu vyote apewe Mungu. Sasa chawa wanataka sifa na utukufu apewe Samia
 
Najiuliza hivi kwanini mtu akiwa shidani, wa ngozi nyeupe, ukimkwamua shidani mwake, atakushukuru sana na hatoona aibu kusema hadharani, fulani kanisaidia.

Lakini sasa sisi kina Mtokambali, ukisaidia na fulani, humtaji, hata ukiulizwa ile shida yako umeitatuaje? Unaishia kusema ni Mungu amenisaidia.

Hivi Waswahili, kwanini tuko hivi? Je, hii ndio roho yenyewe ya uchawi ya kutaka wengine wenye shida kama yako waendelee kutabika bila msaada? Au sisi ndio tuko karibu sana na Mungu kuliko wazungu?
God is like malware for the human brain 🧠
 
Lakin hata kwa anaesaidia pia wapo ambao hupita kutangaza bila mimi yule isingekua hivi.....hiyo unaionaje?
 
Back
Top Bottom