Mbona matatizo madogo sasa hayo
Neno beberu mbona sio tusi, ubeberu ni ubepari uliokomaa
Sasa kwani hao mbuzi sio mabepari?
Hakuna haja ya urafiki kwa jina la diplomasia kama upande mmoja unanyonywa
Sisi kuna viterminologies tumekaririshwa na tunaona sifa kuviimba
Utasikia demokrasia, diplomasia, Haki za binadamu, utawala wa sheria nk vyote hivi ni mifumo ya kinyonyaji ambayo kwao hawaitekelezi kwa asilimia zote
Mzee analaumiwa kwa kuharibu demokrasia kwanza sio kweli pili kama hiyo diplomasia ni ya kinyonyaji acha aiharibu
Tunaambiwa ameharibu demokrasia, ingekuwa na maana au ni applicable Trump asingekuwa rais
Tunaambiwa utawala wa sheria, juzikati kuna maafisa walimtolea ushahidi Trump kuhusu uchaguzi akawatimua
Tunaimbishwa nyimbo ambazo kwao hawatekelezi na ambazo waliopuuza wametoboa
Tumeletewa mfumo wa elimu wa hovyo ambao mtu akishakaririshwa hizo terminologies hapo juu anaona fahari kuziimba hadharani na ati ndio usomi wenyewe
MUNGU BARIKI AFRIKA
Mzee Baba namkubali sana kwa work ethic yake, hands on n.k
Miaka miwili ya mwanzo kwa mimi alikuwa ni perfect, alianza kutatua matatizo(Uongozi) ambayo tulikuwa nayo kwa miaka 30. Uwajibikaji ulianza kuongezeka, ukusanyaji mapato ulipanda.
Kwa maoni yangu washauri (Mfumo) ndio umemwangusha kwa kumshauri vibaya. Kuanzia 2017 Mzee Baba aliachana na yale aliyokuwa ameanza nayo na ndio kipindi hicho mambo ya kuunga mkono juhudi yalianza, Neno Beberu lilianza wakati huo pia. Mabilioni ya pesa yakaanza kutumia kwenye kurudia uchaguzi n.k
Kwa mimi naona bado ana nafasi lakini arudi kwenye misingi ya mwanzo ya kutibu matatizo tuliyonayo ambayo ni "Uongozi"