Mzungu huyu atakuwa ameamua tuachane au yuko busy?

Mzungu huyu atakuwa ameamua tuachane au yuko busy?

Penz la mwanzo Lina kimuhemuhe chake

Anyway angekuwa mswahili mwenzako hata usingekuja huku kuuliza

Ngoja akutumie nauli uende ujikute kwenye usambazaj wa sembe au madanguro

Sikutishi ila muda mwalimu mzuri sana

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app

Usipende ku assume vitu usivyo na uhakika, ht angekua ni mtz km ningempenda na yuko mbali na mm sina access nyngn ya kumfikia ningekua worried vilevile...after all yy ndio alikua anampango wa kuja sio mm niende na ikifikia muda labda anismbie niende sitaenda kichwakichwa sina ulimbukeni unaonifikiria...assnte kwa ushauri though.
 
Niliona video chat, aim ya swali langu ilikuwa ni hizi normal phone calls...like if you know his mobile digits, umejaribu kupiga uone kama itakupeleka kwa voicemail au atapokea mtu hivi?

And how long have you known each other, kama ukicount since day one hadi hapo mbuzi alipokata kamba?

No kupiga kawaida sijawahi sababu niikua natumia whatsapp lbd nifikirie hvy baadae nikiona kimya.
 
Hii jua wachana nayo mse[emoji28] ukikamata mgodi lazma ukae kijanja usije ukapoteza line ya fuba![emoji28]
Fikiria unachomwa na jua hadi unasikia harufu ya nyama choma, halafu unaona watu wana drive tu ndinga kali kali barabarani halafu watoto wadogo. Hadi unajiuliza kama binadamu wote ni sawa[emoji23][emoji23].
Fursa ikitokea ni kuchangamkia tu, kisa cha kuzeeka mapema ni nini? Yaani binti wa miaka 25 anakuwa kama mama wa miaka 40 na wakati ana namna ya kurahisisha maisha[emoji23]
 
Sista Njoo taratibu hata sms hajafungua unaanza kutoa vilio . Jee akizifungua na hasijibu sii utakufa kabisa.

Mimi silii sababu namuhitaji saana ni kitendo cha muda tu naweza kupata mwngn tokana na mazingira yangu ya kazi na dating sites km hizo.. hofu yangu ni niendelee kumuhesabia au niendelee na mambo yangu tu!?
 
Atakutafuta leo. Si unaona ilikuwa ni weekend? Mpenzi wako alienda kwa mpenzi wake na simu anayotumia kuchat na wewe aliiacha nyumbani kwake akaondoka na nyingine ambayo sasa wewe hauna.
Usijali atarudi leo, muendelee mlipoishia.
Mpenzi wako ameenda kwa mpenzi wake kwahio ni maswala tu ya kuvumiliana kila mtu ana wakati wake! 😅😅😅 Eh bana this is sick!!!
 
Habari za leo wanajamvi!

Nimeona nilete hili jambo kwenu labda nitapata msaada wa mawazo na ushauri wenu ili nielewenini nifanye.

Mimi ni binti wa mid 20's km unavyojua kila mtu hua na malengo yake katika maisha basi na ana machaguo yake katika maisha km ambavyo mtu anapendelea mwanamke mwenye shape nzuri, au macho mazuri au sura nzuri, vivyo hivyo baadhi ya mabinti hupenda wanaume warefu mara wenye hela basi mimi ni binti nnaependa kudate na ngozi nyeupe (wazungu) ila si vile vibabu vya kizungu[emoji23].

Well, km ijulikanavyo huwez kupata kitu km hukifanyii efforts so nilikiunga na dating sites kadhaa katika one of the dating site nikakutana na kijana mmoja wa umri wa miaka 31 kutoka nchini Norway, huyu hakua kijana pekee niliewah kukutana nae ila wengi hawakuonyesha userious so na mm sikutaka kuwa entertain till nilivyoanza kuchat na kijana huyu, mwanzo alionyesha ukawaida km wengine so ckumtilia maanani sana ila ndani ya muda mfupi tu wa kuchat km week1 alionyesha km ana ka userious flan km kujibu txt ontime, kutoomba nudes (picha za utupu), kutaka kunijua kiundani na kufikia maamuzi ya kuomba if I can be his girlfriend of which I accepeted..alipanga aje nchini mwishon wa mwez huu na alishakata flight ya tarehe hizo za mwishon na hii ni only after 2 weeks of knowing each other, well niliona km things are going too fast ila sikuichukulia in negative way sababu mapenzi hayanaga formula.

Week 2 baada ya kua tunachat nae every day nilipata minor accident iliyonipelekea kuvunjika vidole vyangu vitatu vya mguu nikafungwa P.O.P (hogo) nikamtaarifu kua nimeumia na kumtumia picha swali la kwanza ni aliniuliza "Do you have western union?" Nikamjibu sina akaniuliza unaweza kutumia njia gani kupokea heka kutoka abroad nikamwambia ngoja niulize maana kiukweli nilikua sijui ndio one of my friend akaniambia nitumie "Worldremit" baada ya kumtumia hiyo app alishangaa maana hakuwahi kuitumia before ila aliidownload na akawa ananitumia screenshot kila hatua ili aweze kufill details zangu...baada ya dakika km mbili simu yangu ilisoma nimepokea laki7 za kitanzania kutoka kwake nilimshukuru kwa kweli ukizingatia sikumuomba ile hela na wala sikua na wazo hilo..aliniambia zitanisaidia kwa transport fees baada ya kujua sina personal car.

Tukawa tunaendelea kuchat by the time alikua na likizo za sikukuu za Christmas and new year so muda mwingi alikua online, he seems like he is an introvert masna kwenye video call hua ni km aina ya mtu anaeishiwa maongez though ni mchatiji mzuri, aliniuliza nacope vp hali ya kuwa nyumban mda wote wakat niko na ile P.O.P nikamjib kawaida tu sina jinsi inabid nitulie akaniuliza km nchini kwetu tuna Netflix nikamjibu ndio ila sikua na account akanitumia details za his personal account means user name yake na password yake na na akaniambia " do not freak out there is another girl using my account but thats my sister" so tulikua tunatumia hiyo accout mimi, yeye na huyo user mwingine ambae sikufatilia sana kumjua as long as alishaniambia ni dada yake..akanitumia kias kingine nijiunge na unlimited internet ili nisiwe bored.

Tuliendelea kuchat mpk alipomaliza likizo ya kaz na alivyoanza kazi, well mawasiliano yalipungua sio chatting za muda wote ila nilielewa sababu ya ubusy, ila lazima atatuma txt mara tu baada ya kutoka kazini mtachat au kuongea kidogo ndio atalala.

Juzi ndio ulikua mwisho wa mimi kuchati nae na our last conversation..aliniambia anatoka mara moja kutembea sababu amekaa ndan muda mrefu and he asked me how was my leg? Nilimjibu ila text ile haijafunguliwa mpk leo

Txt inadelever ila in grey tick which means haijafunguliwa, his last seen inaonyesha muda ule ule ambao tulichat mara ya mwisho so ni km hajaingia online tena, ila txt zinafika hofu yangu ni kua ya Mungu ni mengi amepata tatizo labda au? Maana siwez kujump kwenye bad conlclusion maybe amepata tatizo ila txt zinadeliver sena hazijafunguliwa tu na hajaingia online...ameamua kuquit mahusiano au? But hatujapishana kwa lolote au ni mimk ndie nina overthink?

His netflix account still works to me here, sijatuma txt nyingi sababu sion point ya kutuma txt wakati za mwanzo hazijajibiwa na hayuko online...je kwa wengine ishawahi watokea kitu km hii? Ina uwezekano akawa yuko busy sana? Isije nikasubiri meli wakati niko airport..Ndio masna nikaja hapa sababu ya ushauri wenu na mitazsmo yenu inaweza nisaidia.

I have developed some feelings for him honest speaking ila ni vyema nikajua niko position gani kwa sasa ili nisipoteze muda na hisia kwa mtu ambae labda si km nimfikiriavyo au nijaribu kumpigia kwa simu ya kawaida?

What do u think I should do guys? Au nisubiri tu nione itakuaje?
Hebu na mimi nitumie hizo details za Netflix nikiwa natafakari ni kipi kimemsibu shemeji yetu mtarajiwa
 
Fikiria unachomwa na jua hadi unasikia harufu ya nyama choma, halafu unaona watu wana drive tu ndinga kali kali barabarani halafu watoto wadogo. Hadi unajiuliza kama binadamu wote ni sawa[emoji23][emoji23].
Fursa ikitokea ni kuchangamkia tu, kisa cha kuzeeka mapema ni nini? Yaani binti wa miaka 25 anakuwa kama mama wa miaka 40 na wakati ana namna ya kurahisisha maisha[emoji23]
Hahahahahaha unatambaa na chaki tu😅 sini life tu 😅
 
Atakutafuta leo. Si unaona ilikuwa ni weekend? Mpenzi wako alienda kwa mpenzi wake na simu anayotumia kuchat na wewe aliiacha nyumbani kwake akaondoka na nyingine ambayo sasa wewe hauna.
Usijali atarudi leo, muendelee mlipoishia.

Ah basi km ni hivyo afanye haraka arudi kwa mpenz wake mie kikubwa cha peke yetu kaburi, nimekua na hofu sababu siku niliyopata ajali nikavunjika nilitoka kuchat nae km lisaa tu nikapata ajali mbaya sana ya bajaj ila nashukuru Mungu nilivunjika vidole vya mguu tu katika kujaribu kujinasua, so ingekua vibaya zaidi ningeweza hata kupoteza maisha so my point ni kua chochote kinaweza kutokea ndani ya muda mfupi.
 
No kupiga kawaida sijawahi sababu niikua natumia whatsapp lbd nifikirie hvy baadae nikiona kimya.

You have to try...

Unajua kumtumia tu mtu text inakuwa haina ushahidi kama kaona au kasoma au hajasoma...

Ukipiga simu utakuwa na uhakika kama imepokelewa au lah, na hata ikienda kwa voicemail utajua na utaacha ujumbe...
 
Halafu uache kutumia account ya watu ya netflix, sio uendelee kujimwaga huko bila aibu
 
World remmit, sendwave zote huwa napokelea pesa[emoji28] toka unyamwezini kwa voda yangu! Hapo hujadanganya kabisa.

Kutuma kwenda nje ndio huenda haifai

Watanzania wenzangu tushazoea kudanganyana na vichai vya hapa na pale so sijashangaa sana[emoji28]
 
Kama ulizidisha shida na vizinga ndio ushaachwa hivo

Sikuwahi kumuomba hela wala kumtangazia shida yoyote hata hiyo hela aliyonitumia sikumuomba pia na sikuweka mazingirs ya kumuomba hela...na sikua hata na wazo hilo actually.
 
Mimi silii sababu namuhitaji saana ni kitendo cha muda tu naweza kupata mwngn tokana na mazingira yangu ya kazi na dating sites km hizo.. hofu yangu ni niendelee kumuhesabia au niendelee na mambo yangu tu!?
Unamuhitaji huyo jamaa zaidi ya sana. Siku tatu tu umekuwa na hofu kiasi hicho. Bora hata ingekuwa mwezi,.kweli mapenzi upofu.
 
Cha kwanza nilichokiona tu kwako una tatizo la njaa kwenye mahusiano sio rahisi kwa mtu wa kawaida kukwambia hilo ila most girls wanaowinda wazungu huwa ni sababu ya njaa tu na si kingine. Cha pili tuliza mshono.

Huyo jamaa atakutafuta tu usioneshe kuwa demanding sana huwa mambo yanaendaga smooth tu!
Hahahaha mzee naona umemchana Live
 
Back
Top Bottom