Tetesi: Mzungu/Muitaliano wa January Makamba kuongea na waandishi wa Habari kesho Saa Nane, Hyatt Hotel

Status
Not open for further replies.
Ingekuwa ngozi nyeusi hapo kungefanyika namna lakini NYEUPE kutoka yuropu,sidhani kama inaweza fanyika lolote iwapo hii taarifa ni ya kweli zaidi labda ni kumfukuza nchini
Ni kweli ngozi nyeupe hata ikiwa jangili ikitunguliwa inageuzwa kesi kuwa alikua kwenye doria.
 
Ombi kwa watakao hudhuria:
1. Muulizeni nia yake ya kutafuta influence toka serikalini kwa kutumia rushwa
2. Muulizeni immigration status yake hapa Tanzania tangu kuja kwake
3. Kama ni investor atwambie miradi yake aliyo wekeza Tzn na kodi aliyo kwisha lipa
4. Muulizeni kama ana RB ya police kuhusu malalamiko yake.
5. Swali la jumla: Ni halali kumrecord mtu katika mazungumzo bila yeye kujua na bila ridhaa yake?
Kwa January Makamba: Uwe tayari kujiuzuru kupisha uchunguzi kama utakuwa indicted.
 
Naona boss wako kashokwa pabaya ,,kipindi cha kampeni si ndo alikuwa anagawa hela,,,
 
Magu akimkingia kifua huyu bwana nitamshangaa sana na kuamini hili jina walilompachika mtaani kwetu la bwana JANGALA ni kweli linamfaa,kwani akiona nyomi hupagawa na kuanza kuropoka mambo ambayo mengine hayawezi.

Viongozi wengi wa kiafrika wanaojipendekeza sana katika uongozi wa juu utumiwa na wafanyabiashara wakubwa wa kimataifa kama chambo ya kurahisisha Uwekezaji wao.Watatafuta mzawa ambaye anaushawishi fulani katika serikali na kumtumia hili kutimiza azma zao.

Kwa kuwa Magu alishatahadharisha michezo hii tangu awali kwa kiongozi yeyote aliyemteua,basi January akaona kuendelea na huyu bwana kutampeleka segerea.Anambwaga huku yeye na dadake wameshamramba mabilioni ya pesa.Muitaliano naye anamwaga mboga baada ya Makamba's kumwaga ugali.

Mikataba mibovu migodini na ubinafsishaji usio na tija kwa taifa vilitokea kwa sababu za tabia kama hizi za kidalali ambazo January anazifanya.Tuepushie mbali,kama huyu january angekuwa rais nani anajua clauses zingezokuwepo katika mkataba wa ujenzi wa hiyo bandari,si yangekuwa yale yale yaliyotufikisha hapa.

Uzuri na mfuatilia dada yake kwenye mtandao wa instagram.Yeye kila siku ni kuruka viwanja na mabilionea across the continent.Na hii ni sababu moja wapo inayoniaminisha kuwa this might very well be an ugly truth that hiki kitu ni ukweli mtupu.

Kama Magu ana nia thabiti ya kuirudisha hii nchi katika mstari.Basi wenye mindset kama January ni kuwaogopa kama ukoma.Kama anatimua wengine kwa tuhuma basi naye huyu asimchekee.Unless awe na double standards.
 
Tunajua January ana jeshi kubwa kwenye mitandao. Ila poleni sana.... Kesho hamtaamini macho yenu
 
UVCCM wenyewe saizi washamegeka. Wanatoa tamko, then watakanusha.... Wamejaa unafiki, njaa, utapeli, na kujipendekeza
Mipasuko inaeleweka lakini lazima kila upande utoe taarifa rasmi ...jana kanusho lilikuwa rasmi while taarifa yako haikuwa rasmi ....weka wazi ili uaminike zaidi ...
 
Cha Ajabu Mods wapo na Wanaliacha jukwaa likizidi kushushwa hadhi kwa andishi la Huyu jamaa... Andishi ambalo ukilisoma kwa Makini unajua kabisa ni Upuuzi...
 
huu ni utani kabisa 'watu wazima naona tunachezewa picha sasa' am sure kesho hicho kitu hakipo na huyo mtu hayupo

wajua kutoa rushwa ni kosa,kumshawishi mtu apokee mlungula ni kosa pia?
 
Mkuu si utulie mpaka hiyo kesho ili ukosoe vizuri akili za hao unaowaita wapumbavu.. Kama una hakika sana kwamba haiwezi tokea subiri hiyo saa 8 basi
 
wizara aliyotoka enzi za jk? Iweje babake azungumzie ranchi na mashamba kama ndio ufisadi?hana mashamba ,mifugo na babake achunguzwe
 
Mzungu anadai katapeliwa 1m dollars aliyotoa ili apewe tender ya kujenga Bagamoyo port, wakati hivi ss kazuiliwa na hotel ya Hyatt asitoke mpaka alipe deni la hotel, haiingi akilini..
 
Naona boss wako kashokwa pabaya ,,kipindi cha kampeni si ndo alikuwa anagawa hela,,,
Hao vijana wa UVCCM walizoea kupewa vilaki moja moja na January saizi naona wanahaha kweli kweli.... Hawataki kutafuta kazi halali, wanabaki kujipendekeza tu...

Juzi kwenye msiba wa Kaka yake Jakaya, yaani niliwaona vijana hawa wa UVCCM wanahaha kumsalimia kila mtu, wanaomba ela mpaka msibani na kutafuta UDC..... Kazi yangu ni kuwapaka watafute ajira xa kudumu
 
Wanataka kumhujuma Makamba tu, Makamba Magufuli akikufukuza jitokeze hadharani kuhusu Ushindi wa Magufuli, usikae kimya watakuita fisadi maisha yako yote. Ni vizuri kuvumiliana wakati huu mgumu kwako
Hivi mlivyokiwa mnamuita lowassa fisadi bila hata chembe ya ushahidi mlikua hamjui hili?njia ya mwongo, mwizi na mnafiki ni fupi sana, let us wait and see, it is going to be a tough week for January Makamba and family
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…