Wala sio lazima aseme kwamba alitoa rushwa, anaweza kusema kwamba alitoa $1M kwa Makamba kama malipo ya udalali wa kupigania tenda. In this case mzungu hajatoa rushwa na Makamba atakuwa matatizoni kwa kuwa dalali wa tenda ambayo mzungu analalamika kutopata.
Ila tu niseme kwamba sio kweli kwamba mtoa rushwa na mpokeaji wote wana makosa. Mtoa rushwa anapotoa rushwa na kusema tunamwadhibu kwa kosa gani? Rushwa ni bei ya haki inayotozwa na mtu mwenye mamlaka au dhamana. Kwa maana hiyo kuna mnunuzi na muuzaji. Mnunuzi ananunua kwasababu anahitaji haki ambayo anashindwa kuipata katika muda na njia husika kwasababu muuzaji amefanya muda na njia husika kutopitika na mnunuzi. Hivyo basi kumwadhibu mtoaji rushwa sio sahihi na kufanya hivyo kunaendeleza rushwa! Nikitoa rushwa kumbe sitakiwi kusema maana nikisema kumbe sina utofauti na yule aliyepokea: if that is the case nitatoa na kutunza siri. Lazima tubadiri hii sheria au desturi inayosema kutoa rushwa ni kosa na badala yake tuseme mtoa rushwa ambaye atagundulika alitoa bila kutoa taarifa ataadhibiwa. Hii itamfanya mpokeaji kukataa maana hana uhakika kama mtoaji atakaa kimya!