N haramu kumtakia heri ya xmas ndugu yako mkristo ila si haramu tumia iphone CEO Gay

Hizo ni propaganda za Waislam wachache wenye chuki.

Quran 5 :5
"Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha walio pewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao".

Karibun Christmas ndugu zangu Waislam. Tule tunywe na tufurah kwa pamoja
 
Ebu jaribu kunielezea ili nielewe.
Sababu Christmas ni ibada yaani sikuu yeyote ya kidini ni ibada na inataratibu ndio maana watu wanaenda kanisani siku hiyo hata Idi ya Kiislamu Kuna swala ya Idi.

Kwa hiyo kushiriki katika kitendo chochote kinachohusiana na ibada ya dini nyingine ni kusapoti hilo tendo unakuwa unajiingiza kwenye kukufuru.

Kingine Kumbuka Christmas inasherekea kuzaliwa kwa Yesu ambaye kwa mujibu wa Imani ya Kikiristo ni Mungu yaani ni sawa na kusherekea happy birthday ya Mungu ambapo Kiislamu kusema Yesu ni Mungu ni kufuru kubwa . Sasa iweje ukatae kuwa ni Mungu halafu usherekee na kutoa salamu Sherehe za kuzaliwa kwake utakuwa upo sawa ?

Ni sawa Mimi nimumtukane mama yako halafu au nimuue halafu niandae Sherehe ya kuadhimisha tukio hilo wewe mtoto utatoa salamu ya hizo Sherehe na kupokea chakula Cha Sherehe hiyo ? Kumsema Mungu ana mtoto au kumpa kiumbe cheo Cha Uungu ni kufuru na matusi makubwa kutokana na Imani ya Kiislamu sasa Muislamu kufurahia na kushiriki kwa namna yeyote si sawa na kutukana Imani yake ?
 
Kuhusu simu , simu haihusiani na ibada na hazitengenezwi kwa ajili ya ibada hapo hakuna uharamu hata atengeneze Myahudi sababu haihusiani na dini .

Ndio chakula cha mkiristo siku za kawaida naweza kula ila sio cha Christmas sababu kimefungamanishwa na tukio la kiiibada upo ?
 
Iphone na dini ya ukristo vinahuusiano gani?

Kwani Papa ndo alkua injinia?

Kuna mada zingine unajiuliza huyu mleta mada anakichwa au boga

Muelewe kwa namna hii.
Kwanza Zingatia neno Haram.

Kumtumia heri ya Christmas mkristo ni Haram kwa baadh ya waIslam.
Ushoga ni haram.
CEO wa Iphone ni shoga.
Bas wenye kuona haram kumtuma heri ya Xmas bas wasitumie na iphone. Kwasababu zote ni Haram.
 
Tunafuata Maandiko mzee vitabu havidanganyi katika Surat Al-Khafirun Mwenyezi Mungu kupitia Malaika Gibril alimwambia Mtume Mhamad kuwa Quran 109-1-6

1. Sema: Enyi makafiri!
2. Siabudu mnacho kiabudu;
3. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
4. Wala sitaabudu mnacho abudu.
5. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
6. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.

Kuhusu iPhone sina pingamizi ni simu nzuri
 
Kuhusu simu , simu haihusiani na ibada na hazitengenezwi kwa ajili ya ibada hapo hakuna uharamu hata atengeneze Myahudi sababu haihusiani na dini .

Ndio chakula cha mkiristo siku za kawaida naweza kula ila sio cha Christmas sababu kimefungamanishwa na tukio la kiiibada upo ?
Point hujaelewa badl
 
Sababu Christmas ni ibada yaani sikuu yeyote ya kidini ni ibada na inataratibu ndio maana watu wanaenda kanisani siku hiyo hata Idi ya Kiislamu Kuna swala ya Idi.

Kwa hiyo kushiriki katika kitendo chochote kinachohusiana na ibada ya dini nyingine ni kusapoti hilo tendo unakuwa unajiingiza kwenye kukufuru.

Kingine Kumbuka Christmas inasherekea kuzaliwa kwa Yesu ambaye kwa mujibu wa Imani ya Kikiristo ni Mungu yaani ni sawa na kusherekea happy birthday ya Mungu ambapo Kiislamu kusema Yesu ni Mungu ni kufuru kubwa . Sasa iweje ukatae kuwa ni Mungu halafu usherekee na kutoa salamu Sherehe za kuzaliwa kwake utakuwa upo sawa ?

Ni sawa Mimi nimumtukane mama yako halafu au nimuue halafu niandae Sherehe ya kuadhimisha tukio hilo wewe mtoto utatoa salamu ya hizo Sherehe na kupokea chakula Cha Sherehe hiyo ? Kumsema Mungu ana mtoto au kumpa kiumbe cheo Cha Uungu ni kufuru na matusi makubwa kutokana na Imani ya Kiislamu sasa Muislamu kufurahia na kushiriki kwa namna yeyote si sawa na kutukana Imani yake ?

Vipi kuhusu mwaka mpya..
Huwa hamuwaambii watu heri ya mwaka mpya?.

Maana ni mwaka mpya ulioanzishwa na Warumi wakristo.
(Roma na papa Gregory).
 
Ebu jaribu kunielezea ili nielewe.
😂😂😂😂😂😂
1766622981193.jpg
 
Back
Top Bottom