Hatushirikiani chochote na makafiri katika mambo ya Ibada. CHOCHOTE KILE. Kuwapongeza makafiri katika sikukuu zao za kishirikina ni kuwapongeza na kuwaunga mkono katika ukafiri na ushirikina wao na ni katika kushirikiana nao katika dhambi na uadui.
1. Kuamini kuwa Yesu Mwana wa Maryam (Amani iwe juu yake na Mama yake) ni Mungu ni ukafiri. Ametakasika Allah kutokana na wanayomshirikisha nayo.
2. Kuamini kuwa Allah amejifanyia mtoto ni ukafiri. Allah Ametakasika kutokana na kuwa na mshirika na Ametakasika kutokana na kuwa na mwana. Hana mwana wala mke.
3. Yesu (Amani iwe juu yake) ni Mtume wa Allah, sio mwanae Allah, sio Mungu wala sio katika nafsi tatu za Allah. Ametakasika Allah kutokana na kuwa mtoto na wala Mola wetu hana nafsi 3 na Allah Ametakasika kutokana na kuwa na mshirika yoyote yule. Yesu (Amani iwe juu yake) ni Mtume wake na ni Mtumwa wake.
4. Wakristo wanasheherekea krismasi wakiamini ni siku aliyozaliwa wanayemuabudu kinyume na Allah ambaye wanadai ni mtoto wake, bali wanadai kuwa ndie Mungu mwenyewe. Haya ni matusi makubwa kwa Allah. AMETAKASIKA MOLA WETU KUTOKANA NA YALE WANAYOMSHIRIKISHA NAYO. Hivyo hatushirikiani nao katika huu ushirikina na matusi makubwa wanayomtukana Allah Aliyetukuka. Na wala hatuwapi pongezi katika hili.
5. Sikukuu ya krismasi ni sikukuu ambayo asili yake ni ya kipagani, ina asili ya upagani wa kale huko. Hili wasomi wa kikristo wenyewe wanalijua. Na ina mchanganyiko wa upagani mwingi na mambo yasiyohusiana kabisa na Nabii Yesu
(Amani iwe juu yake) kama mti wa krismasi au "santa claus" uhusika uliojaa uongo na kuwadanganya watoto na stori za uongo za kishirikina.
6. Nabii Yesu (Amani iwe juu yake) hakuzaliwa katika siku hii. Wakristo wenyewe (wasomi) wanalijua hili.
7. Hata kama ingekuwa kweli Nabii Yesu inajulikana siku aliyozaliwa, basi tusingeisheherekea siku hiyo kwa sababu yeye mwenyewe hakusheherekea siku yake ya kuzaliwa, wala Mtume Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake) ambaye ni Mtume wa mwisho aliyekuja na Shari'ah ya mwisho ambayo inapaswa kufuatwa na watu wote mpaka Qiyama hakuisheherekea.
Kama ingepaswa kusheherekea siku ya kuzaliwa kwa Nabii Yesu (Amani iwe juu yake) basi Allah Angemfunulia hili Nabii Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake) na angeisheherekea siku ya kuzaliwa Ndugu yake wa karibu sana na Waislam wangekuwa na haki zaidi ya kusheherekea siku ya kuzaliwa Mtume Yesu (Amani iwe juu yake). Lakini haijaja katika Shari'ah ya Kiislam kuwa tusheherekee siku ya kuzaliwa Nabii Yesu (Amani iwe juu yake) wala ya mwengine yoyote yule.
Hivyo hata kama ingejulikana siku ya kuzaliwa Nabii Yesu (Amani iwe juu yake) ni lini basi kuisheherekea ingekuwa ni uzushi katika Dini kama vile ilivyo uzushi katika Dini kusheherekea siku inayodaiwa alizaliwa Nabii Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake) yaani Mfungo Sita tarehe 12. Bali ni uzushi katika Dini kusheherekea Mawlid kabisa.
Yesu (Amani iwe juu yake) hakuwafundisha wafuasi wake kusheherekea siku yake ya kuzaliwa ambayo haijulikani ilikuwa ni lini na Allah hajatujulisha kuwa ilikuwa ni lini, wala Mtume Muhammad ( Swala na Salamu ziwe juu yake) hajatusomesha kusheherekea siku ya kuzaliwa kwa Ndugu yake Yesu (Amani iwe juu yake) wala yeye mwenyewe hakuisheherekea wala Maswahaba zake (Radhi ziwe juu yao wote) hawakuisheherekea.
8. Waislam tumekatazwa kushirikiana na washirikina katika sikukuu zao. Sikukuu za washirikina ni Ibada kwao.
9. Tunaruhusiwa kutumia ugunduzi wa kiteknolojia wenye manufaa kwetu katika Dunia yetu hata kama umegunduliwa na kafiri.
10. Actually ugunduzi wa mambo ya kisayansi na teknolojia ni mchakato ambao Allah Amewawezesha watu wa Dini tofauti tofauti na mila tofauti tofauti na rangi tofauti tofauti kuugundua. Waislam pia wana mchango katika maendeleo ya sayansi na teknolojia zamani na sasa. Hivyo hii IPhone sio kwamba imeibuliwa tu, bali ukichimba utaona kuna mchakato wa fikra, majaribio na misingi iliyowekwa zamani na watu ikiwemo Waislam ambayo imekuwa ni misingi ya gunduzi zote za sasa. Kuna mikono ya watu wengi ikiwemo Waislam katika maendeleo ya Sayansi na Teknolojia zamani na sasa.