Na hali hii ya mvua DSM: Kama upo ndani ya mnyama Toyota Kluger punga mkono tusalimiane !

Dah! Jf tunadharauliana kishenzi. Pitisha gari lako jangwani na mimi nipitishe usafiri wangu sijui ni nani atakaezama kwenye maji.
Kausafiri kangu hapa hapo
 
 
Watu mnadharau sana, ngoja nipaki kwanza Mercedes GLE 63 amg Coupe yangu kwanza ndo tuongee vizuri, maana nyie wenye magari mnayonunua Kwa kuigana kama sare za kitchen party mnaongea sana na Vitoy vyenu vya chenji za nyanya.
 

Nami nimeshangaa jinsi Toyota Kluger inavyokata maji katika madimbwi na mifereji ya barabara za Dar. Hilo gari nimelikubali. Hasa baada ya kumsikia mtu mmoja akiita Prado "Lori", pale BF gerezani.
 
Kumbe na rangi inasaidia usipate taabu na mvua mkuu
 


Mi Vitz yangu poa kabisa na ninavuka Jangwani kama mchezo maana kwa sasa naitumia as a boat na ninavusha watu, kwa siku sikosi milioni 3.
 
Mnaoponda kluger, msitukosee heshima huo mtambo ni technology ya juu sana
 
Haya Haya...msiempenda KAJA. Mvua hizooooo, Crown, Verosa, Alteza, MarkX, na taka ngumu nyingine za aina hiyo ziachwe nyumbani. Mnavyozimika zimika barabarani mnatuletea msongamano sisi wenye vyombo vya all weather.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…