Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Baraka zako hazina uhusiano wowote na michango unayotoa. Mmezidi kuwafanya wenzenu mazezeta.Kutoa ni moyo wala si malalamiko we ukiona kutoa huwezi na hutaki unapiga kimyaaa unaacha watowaji watoe na wabarikiwe.
Mnatumia matatizo ya watu(umasikini, magonjwa n.k) kujipatia pesa...hiyo sio sawa.Kutoa ni moyo wala si malalamiko we ukiona kutoa huwezi na hutaki unapiga kimyaaa unaacha watowaji watoe na wabarikiwe.
Mbinguni ndio hapo kwa Wachungaji?SADAKA unamtolea Mungu sio mwanadamu....ukienda kwa "angle" hiyo ya Imani basi hutapata kigugumizi cha kutoa sadaka hata kama mchungaji wako akitaja aina kumi za sadaka.
Mbona kwenye harusi unachangia tu kiulaini ila huku kwenye "harusi" ya Yesu unaleta kinyongo😀😀.
MATHAYO 6:20-21Jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba. Maana pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako.
٠.9oINTRODUCTION:
Ndugu moderators naomba uzi huu usipelekwe kwenye Forum ya Dini.
Natumaini nimeeleweka.
SCENARIO:
Mistari ya Machungaji/Padre kwenye ibada/misa moja ...
1. Tutaanza na sadaka ya ujenzi wa kanisa .....
2. Jamani kanisa linampango wa kutembelea wajane na mayatima, tafadhali tutoa chochote kwa ajli ya hilo.
Kwani sadaka ya Dikonia si ipo?
3. Na huu ndio muda wa kutoa Fungu la kumi
4. Sadaka ya ahadi na jengo kwenye bahasha tafadhali.
5. Hiki ni kipindi cha katikati ya mwaka, malimbuko ni muhimu.
6. Sadaka ya mchungaji kwa ajili ya wageni kutoka nje.
7. Na sasa ni muda wa sadaka ya Shukrani ya pekee
8. Sadaka ya mavuno tafadhali
9. Mchungaji anahitaji kununua gari, tumchangie tafadhali
10 ..... Utaendelea mwenyewe mwana JF.
CONCLUSION.
Wakati huo nakua 1994 na kuendelea nikiwa katika usharika wangu mkubwa kabisa pale Dar, tulikuwa tunatoa sadaka 3 kwa kunyanyuka mara mbili.
1. Sadaka ya kupeleka mkononi, hii inategemea na siku
2. Sadaka ya ahadi na jengo, hizi huwekwa kwenye bahasha.
*Sadaka ya ahadi = Mwanzo wa mwaka msharika ana muahidi Mungu atamtolea kiasi fulani mwaka mzima.
*Sadaka ya jengo = kwa ajili ya ujenzi wa kanisa.
Ila sasa hivi mweeeh..!!!
Anyway, kama ishu ni pesa mchungaji na wewe si ufanye kazi.
Yaani, tafuta ajira fanya, au lima kama sisi..!!!!
Anyway mimi ni Mlutheri niliye batizwa, Kipaimara na kupata mafundisho kamili ya Sunday school kutoka Kwenye Usharika wangu ndani ya DMP.
#YNWA
#YANGA_BINGWA