Na wao hulipwa posho za per diem?

 
Kwa hiyo kwa akili yako hiyo hela hawatorudi nayo kuja kuhonga malaya wa bongo?
Hawatotumia kulewa kwenye baa zetu?
Hawatosaidia kulipa ada za ndugu zao?
Hawatotoa msaada kwa ndugu zao?
We huna akili, hujui ht nn multiplier effect ya watakacholipwa.
Unapenda siku zote kusikia pesa hizo wanalipwa viongozi wa serikali tu!
 
Aiseee ona huyu anazungumzia nini!
Kwa akili zako hayo matumizi uliyoyaainisha ni mnufaiko mkubwa ama mnufaiko mdogo wa jamii!?
Kwani mie nilisema pesa walipwe viongozi wa serikali!?
Kwa bajeti ya kusafiri na hao wasanii jumlisha gharama ya vyakula na malazi jumlisha na posho kama watapewa,unajua hizo pesa zingesaidia wapi kwa kiasi kikubwa kwa raia!?
Tanzania bado kuna vijiji kibao maji shida,kuchimba kisima kirefu plus mtambo wa kusafisha maji ni milioni 47-50.
Je unajua kwa hizo pesa visima vingapi vingechimbwa!?
Jinga kabisa.
 
Kuna watu baada ya kutoka hiyo safari ukiwauliza nini kilijadiliwa hawataweza kukuambia chochote cha maana.
Hilo ni moja!

La pili, waambie waandike muhtasari wa aya moja tu kuhusu hiyo safari, watakayoyaandika unaweza kudhani yameandikwa na bata.

Uandishi mbovu. Hakuna nukta, koma, herufi kubwa mahala stahilifu, makosa lukuki ya kitahajia, n.k.

Bure kabisa.
 
🤣🤣

Pia nimejiuliza hili swali: watu serious Kama Julius Nyerere na Benjamin Mkapa kweli wangeweza kuambatana na rundo la waigizaji namna hiyo na kushiriki mjadala wa mambo ya uigizaji?
Nilishawaambia hii nchi kwa sasa inaongozwa na under age..tiss imejaza under age watupu, under age kwa maana umri wao na majukumu ya kazi wanazofanya havilingani, sawa ana elimu lakin umri kulingana na majukumu mtu anapaswa kuyafanya ni muhimu sana, kasoro hii ilianza awamu ya 4..ndio maana mambo ya kitoto ni mengi sana ndani ya serikali..jaribu kufikiri, watu wazima na akili zao wanaweza kuwaza kuweka mabango ya kiongozi nchi nzima kana kwamba anaowaongoza hawajui mazuri anayofanya? Hizi ni akili za kitoto, ni kama ikulu tumeachia watoto na wanachaguana wao kwa wao..Biteko, bashungwa, mchengerwa, katambi, mavunde nk..mtu mzima hawezi kuruhusu msafara wa aina hii pamoja na Rais wa nchi..wametweza sana nafasi za uongozi kuanzia ma DC, DAS, hata Wakuu wa mikoa..ujinga ujinga mwingi sana tofauti na awamu ya 3 kurudi nyuma..kwa sasa DC kuzaa nje ya ndoa ni kitu cha kawaida kabisa.
 
Kila mwaka report ya CAG inasema shirika letu la ndege linapata hasara za mabilioni ya dollar/shillingi. Sababu ni ndio hizi, wanatumia ATCL kubebana na hawalipi nauli kwasababu ni ziara zao.

Kama mkopo waliisha kubali kutupatia wangeenda wahusika kusign hakukua na haja ya kubeba team nzima ya watawala na washangiliaji.

Na hawa hulipwa, huu ni mwaka wa uchaguzi wasipolipwa hawata mshangilia mgombea wao.

Rais Magufuli alikataa kuishi angani kila siku safari, na wakianza safari ya kurudi wanaanza wako kwenye simu kutafuta safari, wakikosa hata Burundi wanaenda ilimradi tu asikae nchini.
 
Kama serikali ndo inagharamia gharama za hao wasanii kwenye hiyo safari, hayo ni matumizi mabaya sana ya kodi za wananchi.
 
Kama serikali ndo inagharamia gharama za hao wasanii kwenye hiyo safari, hayo ni matumizi mabaya sana ya kodi za wananchi.
Serikali inagharimia safari, kula, kulala, na shopingi, na posho ya kujikimu. Budget ya ikulu haikaguliwi na CAG, tena safari na mapocho pocho ndio kabisaa, wanatumia bila ukomo na hatutajua ni kiasi gani kimetumika.
 
nimejaribu kumzingatia huyo bonge naamini haelewi kinachoendelea anaangalia kucha zake........ nadhani yeye ndiye mtu pekee mwenye simu meza nzima.....

bado tunaona wanavyopwaya ila tutawarudisha pale pale bila kujali
 

Attachments

  • IMG_20240605_011048.jpg
    185.8 KB · Views: 1
Nchi inajengwa na Watu wenye moyo na huliwa na Watu wenye meno
 
nimejaribu kumzingatia huyo bonge naamini haelewi kinachoendelea anaangalia kucha zake........ nadhani yeye ndiye mtu pekee mwenye simu meza nzima.....

bado tunaona wanavyopwaya ila tutawarudisha pale pale bila kujali
Usi myanyapae kwa sababu ya unene wake, meza nzima ni wageni waalikwa hata hawajui wanafanya nini, wanasubiria muda wa kula na kwenda kutembea madukani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…