Naacha Pombe kuanzia leo

Hii kauli hakuna mnywaji ambae hajawahi kuitoa akiwa na mning'inio. Huwa ni kauli ya asubuhi pale unapoona maisha magumu hayana maana ila subiri hangover itoke mchana au jioni kama mwenyewe hujasema ngoja nipate kamoja aisee
 
Nimekuwa mnywaji nisiye na kiasi, hivyo naona pombe siyo salama tena kwangu, hivyo kuanzia leo Jumatano tarehe 25 August 21 nimeamua kuacha pombe bye bye Safari lager
Toa mathara nasisi tukufuate mkuu😅
 
Kuacha pombe ni kazi ngumu sana. Siku nyingine uamke huna hamu ya kula kichwa kinazunguka tuuuu unajiapiza sinywi teenaaa mwili ukikaa sawa tu unarudi kulekule kwa kina viti virefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…