Naachana na harakati za kisiasa Tanzania, hazina faida yoyote

Harakati za kisiasa maana yake ni nn?
Uzalendo wako ni zaidi ya uanasiasa acha uanasiasa jitahidi kuwa mzalendo
 
Mkuu sio Tanzania tu duniani kote tumekuwa Infiltrated na Illuminati. They are the one concerned with all this, people are slept (Trance) hawajui cha kufanya. Watu wameshikilia misimamo yao ya dini wakiamini Mungu yupo wa kuwasaidia, hakuna..wengi wanaamini Yesu au Mohamed anarudi kumbe dini hizo zinawaharibu pasipo kujua kuwa tumenyemelewa na Illuminati wanataka kuchukua dunia yote.
Wake up people.
 
Karibu sana Burundi mkuu!! Mimi nipo huku kwa wiki ya pili sasa!! Hali ya hewa ni nzuri sana kwa kilimo na pia kwa makazi!!

Wenyeji wamenibatiza jina wananiita Tate Mkuu lunziza!! Yaani nimesahau kabisa kuhusu Tanzania na TOZO zake!
 
Mkuu technically umechukuwa uwamzi sahihi kabisa!

Binafsi sijawai kufangamana na siasa za Tanzania kwa namna yoyote ile!


Kufungamana na siasa za Tanzania ni kujitafutia msongo wa mawazo unaoweza kuepukika.

Ni mtu mpumbavu pekee anaetumia nguvu kubwa kueneza chuki, kejeri na dharau dhidi ya wanasiasa ikiwa hafaidiki kwa namna yoyote ile kimasilahi na siasa za Tanzania.
 
Kiufupi nimeachana na siasa, nimeachana na Tanzania nimekata tamaa, nimepoteza uzalendo nitaondoka Tanzania na kwenda kuishi na familia yangu kwenye nchi nyingine inayofuata misigi ya Sheria, Haki na Uwajibikaji wa viongozi.
Kila laheri ndugu.
 

Nyerere aliiacha Tanzania yenye wafu wanaotembea so usijisumbue na ninamshangaa sana Mbowe sijui anamtesekea nani…. Bora awe mtukanaji wa mitandaoni Kama sisi tu.
 

Wanachofanya ccm wanategemea watu wote watakata tamaa kama ww, hapo walipo ccm wameshakata pumzi baada ya kupoteza ushawishi kwa umma, hivyo wanategemea nguvu ya dola tu. Tunakutakia mapumziko mema kama kweli umefikia muda wa kustaafu, tuache vijana tuendelee hata kama hatutafanikiwa leo, basi muda sio mrefu lazima tufanikiwe kwa faida ya kizazi chetu.
 
Pole mkuu. Mpiganaji hakati tamaa. Kukata tamaa ni kusaliti mapambano. Na mapambano kwa mazingira ya TZ siyo lelemama.
 

tushakutana sehem kwenye comment nkakwambia uachane na kelele kwenye ajira za watu, hatimae umeniskia! na bado kuna wengine wamebaki wanatetea kitu wasichokijua! hio miaka saba ungetumia kwenye familia yako tu
 
Usiondoke wala kuacha siasa kwani saa ya ukombozi ipo karibu zaidi ya unavyofikiria!
 
Niliwahi kufanya hili lakini kila nikisoma habari za nyumbani, moyo husononeka!
Kiufupi nimeachana na siasa, nimeachana na Tanzania nimekata tamaa, nimepoteza uzalendo nitaondoka Tanzania na kwenda kuishi na familia yangu kwenye nchi nyingine inayofuata misigi ya Sheria, Haki na Uwajibikaji wa viongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…