Naachana na harakati za kisiasa Tanzania, hazina faida yoyote

Kiufupi nimeachana na siasa, nimeachana na Tanzania nimekata tamaa, nimepoteza uzalendo nitaondoka Tanzania na kwenda kuishi na familia yangu kwenye nchi nyingine inayofuata misigi ya Sheria, Haki na Uwajibikaji wa viongozi.
Ukiipata hiyo nchi uni'tag', nijiridhishe kama kweli upo salama huko.
 
Achana na siasa, mabomu hua yanalipukaga ynyewe bila hata influence ya wanasiasa ,tena la kwanza litalipuka soon na linaitwa 'vijana waliokosa ajira'
hii itakuwa nchi gani mkuu. Kama watu walinyimwa ajira miaka 4 na hajafanya kitu,kama watoa ajira sekta binafsi ilivurugwa miaka 5 hakuna aliyefanya kitu.

Suala la tozo za kijinga mimi kwangu ndio uthibitisho wa mwisho kwamba hatuna wananchi bali ni makondoo tu yakuswaga kokote
 
Hata wewe u ayeandika hukuweza KUANDAMANA kilele zako ziko kwenye keyboard tu . Ungejitokeza na bango huenda tungekuunga mkono hukutoka.
Labda utakuwa bundle linakata tu au unabadili ID
 
Nimekuelewa vizuri Sana mkuu, sisi wananchi ndiyo tatizo. Tukibadilika sisi basi system itabadilika Mara moja, maana hata hao viongozi ni zao la sisi wenyewe wananchi
 
Be patient mkuu,ili nakuhakikishia
 
Pole, kama uliitiliia maanani siasa za nchi hii, na Jua umeumia sana. Usije shangaa hata ulio wapigania Chadema kumbe wapo CCM.
 
Mkuu unaandamana wapi wakati watawala wakontayari kuua kwa ajaili ya maslahi madogo tu. Yaani kichaa anakukimbiza na Panga unasimama?
 
Duh, na wataacha wengi siasa mwaka huu kuaga kutakuwa kwingi kwelikweli...
 
Congrats ingawa imekuchukua muda kuufikia ukweli.

Kilichokutokea ni kwamba mahasimu wako (CCM) wamekushinda kimkakati. Mfumo mzima wa CCM umesukwa kuhujumu na kufisidi nchi kupitia dola. Mkakati wao mkuu ni GHILBA kwa wananchi kupitia mtandao mzito wa propaganda.

Kwa wale wagumu kughilibika, propaganda zimelenga kuwakatisha tamaa kwamba demokrasia, haki na utawala bora HAVIWEZEKANI Tanzania. Ni mambo/utamaduni wa mabeberu! Watanzania hawataki hivyo; wanataka maendeleo tu. Halafu wanasiasa wote hawaaminiki; wako Sawa. Aidha, hakuna chama kingine kitakachokuja kuongoza Tanzania zaidi ya CCM.

Kwa wale wagumu zaidi ni kufilisiwa, kesi, jela, vipigo na shaba zisizozidi 3 (kwa viwango vyao rasmi).

Ulipofikia ni kwamba WAMEKUKATISHA TAMAA (frustrate); WAMEKUCHOSHA (exhausted); WAMEKUPOTEZEA MWELEKEO (disoriented) na hivyo WAMEKUSHINDA kama tu walivyowamaliza Watanzania.

Hiyo ndiyo CCM na watenda kazi wake. Wengi walioshindwa kupambana nao hatimaye wamejiunga nao na kuendeleza propaganda za ghilba kwa nguvu zaidi! Wamekuwa co-opted. CCM ni zaidi ya chama!
 
Nashukuru Sana MUNGU nimeachana na siasa tokea June mwaka huu Kwa sasa Nina Amani ya moyo sanaaa......
Kitu ambacho nashukuru moyo wangu nikiachana na kitu kinachosumbua moyo naachana nacho milele
 
Ukitaka kufurahia siasa za TZ uwe CCM. Yaani ni mtelezo tu.
Sawa kabisa. Ni bata tu almuradi dhamira yako haikusumbui.

Kuwa memba wa chama tawala kwenye nchi zetu hizi ndio ufunguo wa maisha kwa wanaosaka mtelezo.

Hata enzi za NAZI Germany, wengi walijiunga na chama cha NAZI ili kupata mtelezo au “raha” ya kuwa pamoja na watawala na kusulubu wapinzani: The lightness/ease of being a NAZI!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…