Naachana na harakati za kisiasa Tanzania, hazina faida yoyote

Mbona kwenye mitandao tunasoma kuwa watu wapo tayari kuingia barabarani hata Mbowe alisema ataitisha maandamo nchi nzima ya bila kikomo.
 
Maisha ya hapa Duniani ni mafupi sana walikuwepo wakina Kambona,Mapalala,Mtikila nk.
Umefanya jambo jema ingawa wazo la kuhamia nchi isiyokuwa na mizengwe ungelipitia upya maana walioongoza kuipigania Demokrasia ndiyo wanaoongoza kuivunja.
 
We ndio unajua Leo mkuu ?

Watanzania ni creatures ya ajabu tangu kuumbwa na kwa dunia, tafuta pesa kula na familia yako achana na watanzania.
 
Mkuu umechelewa sana. Mimi toka Lowassa ashindwe wananchi wakawa tayari kwa lolote lakini hakuna kilichotokea mimi ikawa ndio basi tena mpaka leo
 
Mtoa mada umeongea ukweli mtupu.

Kuna mambo mengi ya uonevu yanafanyika lakini tunakosa umoja wa kupigania haki.

Hii nchi tumegawanyika sana, Wapo wachache wanaokemea tu bila utekelezaji, wapo wanaojionea kawaida tu maana hayajawakuta wao, pia wapo wanaofurahia.
 
Kweli tupu.

Tatizo la Tanzania ni uoga wa wananchi wake.

Watanzania sisi ni watu wa ajabu sana uoga unafki uongouongo ndo vitu tunavyoweza.

Na usijiroge ukajifanya unataka kuwapigania yakikukuta wao ndo wa kwanza kukusema pembeni.
Hapo kwenye unafiki ungebold kabisa
 
Jitahidi uachane na roho yako pia ili upumzishe mwili kwa amani😁😁😁😁
 
Kamanda elekea Burundi hapo ni karibu unaweza rudi fasta wakati wowote ukitaka kuja kusalimia nyanya yako baba yako na mama yako
 
Hongera kwa kutambua kuwa CCM sio tatizo, sasa nakukaribisha rasmi kwenye chama chetu wanamapinduzi, huku hakuna stress ni furaha mwanzo mwisho🤣
Your browser is not able to display this video.
 
Tatizo kuu la msingi nchini hujalisherehesha. Laana ya watanzania ni kada ya watumishi. Polisi, mahakama, mahospitali, watu wa maji, umeme, mainjinia, tra, hazina, wizara, idara, mashirika na makampun ya umma hayana tija, kuna uzembe, wizi, ubadhirifu rushwa, ufisadi na upendeleo. Hawa ndio wanaotengeneza na kuendesha MFUMO, kielelezo cha jamii yetu jinsi isivowajibika
 
Nayaheshimu maamuzi yako ya kioga, askari hatakiwi kukimbia uwanja wa vita, anachotakiwa ni kutafuta njia mpya za kukabiliana na adui.
Njia aliyoitafuta kwa zaidi ya miaka 7 bila kuiona?
 
Watanzania sio binadamu halisi bali ni misukule ama kwa jina lingine ni ndondocha...
Sasa vipi tenaaa[emoji852][emoji852]? Magufuli wetu mliye mchukia si kawapisha njia na mlishangilia kabisa kufa kwake ,sasa mbona mnaendelea kututukana wakati huu ndiyo wakati wenu wa kula bata
 
Tulishasema:

• Wapinzani wakweli Tanzania walikuwa

  • Oscar Kambona
  • Mch. Mtikila
  • Maalimu Seif
  • F.Mbowe (ambaye naye anakosa support ya Wananchi kama wenzie waliomtangulia)

Hawa kina Lipumba, Mrema, Lowassa, Sumaye na kina Zitto hamna kituuuu
 
Magufuli alikuja -akawa anakusanya ghalani kwa nguvu mkamwita dictator
Samia amekuja - anatapanya kwa nguvu ,sasa mnaanza kulia tena ,
Sasa hapo ndiyo mtajua mtapanyaji au mkusanyaji yupi kiongozi bora
Magu tunakukumbuka hadi chagadema wameanza kukata tamaa na nchi
 
Sasa vipi tenaaa[emoji852][emoji852]? Magufuli wetu mliye mchukia si kawapisha njia na mlishangilia kabisa kufa kwake ,sasa mbona mnaendelea kututukana wakati huu ndiyo wakati wenu wa kula bata
Umemuelewa mleta hoja hata kidogo ?!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…