Naamini kwa dhati kabisa nguvu ya Makonda haitokani na kuwa kwake katibu mwenezi wa CCM, lazima kuna chanzo kingine kinampa kujiamini kiasi hiki

Sasa wewe unadhani yeye hajui.inachoongea? Hao wanaoutwa wateule hakuna Cha maana wanafanya kumsaidia Rais ndio maana kampa Rungu Makonda.

Tumuone Sasa wa kumbishia
 
Mchango wa Makonda katika watu kupotea na kutekwa na hata kuuwawa wakati wa Uraisi wa Magufuli unajulikana. Watu kama USA wana ushahidi wote ambao serikali iliambiwa kama wakibisha wako tayari kuuweka hadharani, wakaufyata mkia.

Ndio maana Samia alipokuwa raisi, pamoja na uhusiano wake wa karibu sana na Makonda, alimshauri Makonda asubiri kwanza hadi watu wasahau kidogo yaliyofanyika akiwa "Mkuu wa Mkoa" wa Dar es Salaam, japo Makonda alitaka apewe nafasi immediately.

Sasa kama kuna mwenda wazimu atafikiria Makonda anaweza kupewa nafasi ya uraisi, mtu ambaye ana tuhuma nzito za mauaji, basi siku hiyo ikitokea nitakuwa wa kwanza kushawishi watu kwamba demokrasia nchini haifanyi kazi tena na ni afadhali serikali itakayosimikwa kwa namna hiyo iondolewe madarakani hata kwa nguvu.

Hakuna sehemu popote kwenye vitabu vya uongozi panaposema kiongozi muuaji akichaguliwa kidemokrasia basi ni sawa tu aachwe asifanywe kitu. Hapana, dikteta yeyote, hata kama alichaguliwa kidemokrasia, anastahili kuondolewa kwa nguvu. Uchaguzi wa kidemokrasia ni wa siku moja, lakini uongozi wa kiongozi aliyechaguliwa ni wa miaka mitano. Huwezi kumvumilia kiongozi dikteta muuaji kwa miaka mitano eti kwa sababu alichaguliwa kidemokrasia. Alichaguliwa aue watu? Ondoa uchafu huo hata kwa mtutu wa bunduki.
 
Reincarnation… Hii nchi iko chini ya wa- TAIFA sio wa-SERIKALI tena
 

Makonda hata azunguke vipi, kuna siku wanaomlinda watakapoondoka, atasimama kizimbani kujibu mauaji yote ya raia wasio na hatia aliyoyaplan na kuyasimamia.
 
Pascal, nimekuelewa nadhani. Kwa tafsiri yangu nguvu ya YEYE inaweza kuwa ni abstract, kwa sababu binadamu tunaweza kuwa na nguvu na control juu ya mtu mwingine kutokana na nguvu ambazo ziko ndani yetu, ambazo sio lazima zianishwe kikatiba. Ni nguvu zinakuwa very powerful kiasi kama mtu anaweza kuwa hana kauli mbele ya influence ya hizo nguvu, kama vile kuwa chini ya hypnosis.

Pili, ni kweli kabisa CCM inapeta kwa sasa, na Makonda anachangia sana katika kupeta huko na hizo amsha amsha. Lakini pia tukumbuke amsha amsha inaweza ikawa amsha amsha inayoleta ngoma iliyovuma sana kupasuka. Mara nyingine watu wanasema usimwamshe mtu aliyelala, kwa sababu alipolala hakuwa conscious na lolote katika comfort zone ya usingizi wake, na akiamka anakuwa katika state ya kujiuliza na kufanya maamuzi

Mwalimu wangu wa physics, wakati tukisoma work done = force x distance, alisema ukijitwisha gunia la kilo 50 kichwani, ukatulia nalo sehemu moja hata kwa masaa kumi, hujafanya kazi. Baada ya Makonda kumaliza ziara zake za mikoa 20 (sidhani kama atathubutu kwenda Zanzibar), itakuwa kama gunia la kilo 20 alilojitwisha amelitua bila kuwa amelisogeza hata milimita moja. Gunia hilo ni matatizo ya watanzania yanayotokana na uongozi usiosimamia watendaji wa serikali ya CCM kuwajibika katika majukumu yao.

Workdone ya Makonda = Force x distance = 0,

japo force itakayokuwa imetumika ni kubwa sana. Sijaona namna yeyote tunayoweza kusema Makonda ametatua matatizo ya wananchi. Ukienda Shinyanga alikopita tayari, je hawana matatizo tena yanayotokana na uongozi wa mkoa usiowajibika? Labda tum-assess katika kuonyesha kwamba serikali iko mbali na wananchi katika kutatua matatizo yao, kitu ambacho Fereshi, in a very pathetic and mediocre way, amaejaribu kuki address.
 
Bashite kwa ubora wake. Baba kamrithisha mwanae toka kuzimu.
 
Naona unazinguka Sana : Makonda ni Mtoto wa Familia za Kawaida Kabisa za Kitanzania na anajua uchungu wa kuumizwa na Mafisadi papa na anajua wako wanaoendelea kuumia zaidi na zaidi kwasababu ya kupumbazwa na Taarifa za Fedha wakati Mwananchi wa Kawaida anachotaka kukiona ni Mazingira rafiki ya yeye kuishi. Na Ukiona Makonda una nongwa kwa Makonda jua ni sehemu ya kundi linalosababishia Wengine umasikini.
NB: Makonda anatakiwa kutiwa Moyo kwa Mambo makubwa anayoyafanya ya kuwakumbusha Watendaji mbalimbali wa Serikali (Wauza Duka) maana yeye ni sehemu ya Wenye Duka (CCM).
Na Kwa Mwendo wa Makonda naona Picha ya JPM na ndoto zake kwenda kutimia awamu hii ya 6. Samia hoyeeeee, Tanzania Hoyeeeee, Mkonda hoyeeeeee. Nisema tu Piga kazi Mpaka wakasirike
 
Sasa wewe unadhani yeye hajui.inachoongea? Hao wanaoutwa wateule hakuna Cha maana wanafanya kumsaidia Rais ndio maana kampa Rungu Makonda.

Tumuone Sasa wa kumbishia
Sijui kama unaelewa unachosema hapa? Jaribu kuweka mantiki katika hoja unayotoa. Not this.

Una maana Rais anateua mamia ya watu kufuja mabilioni ya serikali bila kufanya kazi ya maana hadi Makonda ategemewe kutenda hiyo β€œmiujiza” yake kwa gharama kubwa zaidi?

Tunatangaziwa mara kwa mara Rais akiteua na kutengua. All in vain?

Anyway kwa vile Watanzania wameamua kutulia katika ujinga, acha CCM iendelee kuwacheza shere hadi kiama.
 
Kwa hiyo baada ya ziara ya Makonda Mbeya, mwezi ujao nikitembelea Mbeya nitakuta wananchi wa Mbeya hawana matatizo, kwa sababu Makonda alipita?

Unajua kuna watu hamna kabisa uwezo wa kutafakari, mnaona vitu kwa ukaribu sana? Wazungu wanasema "you don't see further than the end of your nose"
 
Sasa ulitaka makonda aje nyumbani kwako?au ni chuki na wivu umekujaa

Tarizo hamkutegemea makonda atapewa tena cheo ,Mlikuwa mnatembea na hukumu zenu mfukoni
Jambo moja ninakuunga mkono 100% ni kwamba hatukutegemea Makonda atapewa tena cheo, kama ilivyokuwa kwa wengi tu ndani ya CCM na ndio maana Samia alipata wakati mgumu kidogo kulazimisha Makonda ateuliwe. Watu wenye busara walimshauri lakini alikataa, na labda kwa sababu ya influence ya Makonda juu ya Samia pia. Hatujui kwa nini Samia aling'ang'ania sana lazima Makonda arudi.

For your information, hata watu kama ubalozi wa USA walishangaa sana. Si unakumbuka, walisema Makonda enzi za Magufuli alikuwa akiwanyima watu haki yao ya kuishi, na walikuwa na ushahidi. Unajua nikikunyima haki yako ya kuishi maana yake nitakufanya nini?
 
Anyway sina jibu lakini Makonda angalau anaonyesha njia kwamba kuinyoosha hii nchi inawezekana. Imagine tuna raisi, Makamu wa rais, Waziri mkuu, spika wa bunge na mawaziri na makatibu wakuu pamoja na wakuu wa mikoa na wenyeviti wa chama wenye ujasiri kama wa Makonda hii nchi ingenyooka tu. Tuendelee kumwombea Makonda na si kumponda.
 
Mimi binafsi yangu nitakua wa mwisho kuamini kile anachofanya mwenye cheo cha ukatibu mwenezi hadi pale zile kero zinazosemekana kwamba anaziskiliza kutoka kwa wananchi na kwamba anazichukulia hatua.
Ni muendelezo wa kile kinachoaminika kwamba sisi watanzania ni rahisi sana kusahau unapewa kofia ya "wananchi" halafu unapigia kura chama tawala
Yaani tumeshasahau swala la bandari, katiba, sasa tuko na makonda aaaaagh!!!!!
 
Kwa maelezo yako ni wazi kwamba Makonda ana baraka zote za Rais. Rais baada ya kuona hana ubavu wa kuwakoromea watendaji aliamua kumtafuta mtu wa kaliba ya Magufuli ila ambaye anammudu pia. Rais hakuwa ana uwezo wa kummudu Magufuli, ila anammudu vizuri Makonda. Kwa njia hii, Rais anafurahia tu kazi yake na milakati yake
 
Makonda ana kitu cha tofauti ndani yake, wakati ambapo watu wengi tulitarajia kwamba amepotea kwenye siasa, kaibuka na ndio gumzo sasa.

Kila nafasi atayopata hata ikiwa udiwani atang'aa sio kwasababu anafanya jambo la kipekee kuliko wengine, ila ana neema au charisma inayofanya awake.

Chadema wana vijana wengi makini kuliko Makonda, lakini wamelala, nakumbuka harakati za Marehemu kamanda Mawazo hakukaa kinyonge, he was vocal and bold, hata ukisikiliza hotuba zake utaona hilo.
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘βœ…βœ…βœ…βœ…
 
Makonda ananguvu zaidi ya Mama Abdul kwasasa.Ndio anakwenda hivyo,
Nihivi!!Makonda hafai hata kidogo lakini kwasasa nibora Makonda mara 100 kuliko Ccm yoote na baraza zima la Mawaziri.Sisemi Bunge mana bado ndani ya Bunge wapo wabunge wachache wenye nafuu zaidi ya Makonda.

Sent from my SM-A107M using JamiiForums mobile app
 
Deep state wamemweka hapo kuvunja nguvu ya Msoga at al.
Mkuu ulichoandika ndiyo ukweli wenyewe. Hata mimi simkubali Makonda kabisa na nina threads zangu nyingi humu.

Ila nilichokiona ni kwamba awali Mama alichukua watu wote alioelekezwa na Mstaafu wa Msoga na akawapa kazi kama akina Januari, Mchechu, Maharage, Nape, nk

Lakini watu hawa hawajamsaidia Rais Samia katika kufanya kazi, mfano Δ₯ali ya TANESCO na giza tulilonalo.

Worse enough akaonekana Katibu Mkuu wa zamani Chongolo akiwa ana conspire na Team Msoga kutaka waweke mgombea mwingine mwaka 2025.

Kwa Tanzania ya sasa hatukubali tena Mstaafu wa Msoga ashiriki kutuonyesha nani anafaa kuwa Rais kwa kuwa hana uwezo na Samia kishajua hiyo conspiracy.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…