Kwanza nikuweke sawa kuwa, mimi simfikirii Mungu kuwa sawa na binadamu.
Nimesema kuwa Mungu ana uwezo mwingi,akili nyingi,maarifa.mengi,ukamilifu mwingi ila kati vyote hivyo anavyo katika hali ya wingi na siyo katika hali ya ukamilifu wote (100%) ama ya kutokuwa na kikomo
Nasema hayo sija- Qoute kokote ila nimesema ni kutokana na jinsi anavyojipambanua yeye ndani ya vitabu vyake vitakatifu (rejea mifano miwili ya maswali niliyatolea mfano kwenye uzi).
Mungu angelikuwa na sifa zote hizo za ukamilifu basi hizo kasoro zilizojitokeza (zikapelekea dhambi) zingeweza kuepukika iwapo uumbaji huo angeufanya katika ukamilifu.
Zingatia kwamba, sijaribu kumkosoa/kumsahihisha Mungu katika uumbaji wake bali nataka tu kujua kwanini itokee hivo wakati yeye ana ukamilifu wote na uwezo wake hauna kikomo ?
Labda mnambie kama hizo kasoro aliziumba kwa maksudi kwa sababu anazozijua mwenyewe hapo nitawaelewa ila mkiendelea kunambia aliumba katika ukamilifu wote, hapo nitaendelea kuwauliza maswali yasiyoisha.
Mfano wako wa mpira kuwa na wachezaji 22 na kushindana kuingiza goli kwa miguuu.
Huu mfano kumbuka ni wa kanuni (sheria za kibinadamu ambazo tumeziweka wenyewe) na mara kwa mara hufanyiwa marekebisho kulingana za uhitaji.
Mfano sasahivi wanafikiria kupunguza dakika za kucheza ziwe 40 kwa kila kipindi badala ya 45.
Kwa hiyo hizi ni kanuni ambazo tumweziweka na tunazibadilisha muda wowote tutakaotaka