Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

kwanini unampangia Mungu jinsi ya kumjua kwa njia zako za kipagani wewe ni nani kwake au unaweza mpa faida gani zaidi ya kumjazia tu dunia mpaka akushobokee ushaambiwa unataka kumuona utamuona kwa terms zake acha dhambi uzinzi na uasherati usengenyaji na matusi acha tamaa za mwili usiabudu miungu mingine waheshimu wazazi wako na umkubali kuwa yeye ni muumba wa mbingu na nchi ujinyenyekeze kwake then utamjua. Mungu hajidhihirishi kwa terms za wanadamu hata siku moja ni kwa anavoona yeye. Yani unataka Mungu akufuate bar nd uamini yupo sasa kungekuwa na maan gani ya watu kuacha dhambi ili wamuone Mungu.
Afu we sijui unaongea nini kwa hiyo dunia nzima isipokuwa pango la Muhammad ilikuwa bar au sio. Afu unakamia tamaa za kimwili..sio tamaa Ni natural mechanisms za evolution ambazo wanyama wote wanazo. Kwa Nini Ni kosa mi kutimiza haja zangu za kimwili. We ukiwa na njaa si unatamani kula. Mbona huachi kukidhi hio tamaa ya mwili.
 
Thibitisha kama dini ya kikristo imetetea utumwa kwa vifungu tuone hapa. Na wapi imeandikwa dunia ni flat. Wapi bible imesema tuibiane makanisani.
Dogo soma Biblia yako sawa. The four corners of the earth resting in pillars. Haya dunia ipo hivyo au. Mambo ya fungu la kumi si wizi huo. Slave obey ur masters as u obey Jesus Christ. Skia ingia Google tafuta verses condoning slavery utaziona zipo kote la kale na jipya sawa. Wakristo hamsomi Biblia yenu unaongea tu.
 
Moto wa milele usichanganye sio kuungua kila siku ila ni kifo cha milele maana mshahara wa dhambi ni mauti hivo utachomwa mpaka jivu la mwisho ndugu. Mungu atuokoe na adhabu hii.
Ni sawa na mi nakuambia nitakubaka usiponipa hela na we unatoa hela na unasema kakuokoa kutoka kwenye kibako. Siwezi weka maisha yangu kwenye control tactics za watu wa zamani wasioijua dunia.
 
Hapa kuna vitu viwili unachanganya kati ya view ya Mungu kwa wanadamu na view ya binadamu kwa Mungu. Kwa Mungu dini ni hukumu yako wewe yani ukiadhibiwa usije lalamika kuwa umeonewa(harsh but nd reality) ila kwa mwanadamu dini ni zawadi ya kuweza kumjua Mungu wa kweli na pia uwe na idea ya kitu gani utakutana nacho katika hukumu laki
Hahahahah! Kulingana na maneno yako unaonyesha dhahiri kuwa mungu kuna watu wake huwa anawachagua mapema tu ndio maana wengine anawapa neema then wengine anawazidisha maovu ili wapotee mazima ili baadae aje awaadhibu wakati uovu aliwawekea mwenyewe tena makusudi.

Halafu unavyoiona dini ni kitu kizuri yaani ni zawadi ya mungu kwa wanadamu kana kwamba tusiosali sio wa mungu na unasahau kuwa dini hizi zimefika africa karne ya 18. Je waliokuwepo hapo kabla wasiojua hizo dini mungu atawafanyaje??

Ila any way naamini mungu wa kwenye hivyo vitabu vya dini sio muumba wa ulimwengu.
 
Wewe dini hujasoma vizuri unanyapia nyapia tu navoona. Maandiko yameleta uhusiano wa kiroho kati ya mwanadamu na Mungu na pia uhusiano wa kiroho na mwili kati ya mwanadamu na mwanadamu mwenzie ila kwa akili yako unahisi basi watu walikuwa hawapigi hata story wala hawacheki wala hawachezi na ndo maan unaconclude science haikuepo. Maengineer wenu wanajisifu kwa skyscrapers wakati mnara wa babeli watu waliupandisha juu sana mpaka wakachanganya lugha sababu nia yao ilikuwa ovu. Watu walivuka kwenye maji sio kwa miujiza watu walichimba dhahabu watu watengeneza silaha watu walijenga mapyramid hayo watu walitengeneza mavazi na kila kitu ila wewe unahisi watu walikuwa wanasali tu tuu hakuna maendeleo. Kama hujui maendeleo mengi yametokana na hao waliopata siri za Mungu mwanzoni watu wamefundishwa technology mpaka na akina zeus ambao walikuw ma nephilists. Ila uko kulaumu muafrica dini nd imemfirisi wakati waarabu na hao wazungu sio maskini sababu mpaka wakaleta huku it means walijifunza kwanza wao kwann wasiwe masikini kwanza wao.
Wewe story ya Babel Ni ya uongo soma historia ya Babylon vizuri ndo utaelewa. Na kuchanganya lugha sio sababu kwa maana hata Burj khalifa imejengwa na watu tofauti wa nchi na lugha mbalimbali na Ni refu kuliko Hilo Babel na watu wametengeneza ndege, rockets zinaenda mpaka pluto. Haya Kama Mungu yupo mawinguni mbona hakuchanganya lugha za Hawa watu wa sayansi na ujenzi wa maghorofa marefu duniani.
 
Kwaiyo badala ya kutaka ilitakiwa asitake bali afanyeje kuonesha ukamiifu wake, eti naomba kuelimishwa kidogo kuhusu sifa ya mkamilifu inatakiwa afanyeje anapohitaji jambo fulani kukamimilika iwapo hatakiwi kutaka?

Tunajadili na kuelimishana and I stand to be corrected for what I believe on.​
 
S

Sasa hayo ya kutokuumba au kuumba hakushindwa ila ni mapenzi yake na sio yako na hakuna wa kumpangia kama ambavyo hukumpangia wewe uzaliwe au usizaliwe, uwe na jinsia me au ke hayo yote ni mapenzi yake ambayo yapo nje ya uwezo wako,

Ndio maana kakupa nawewe uhuru wa kufanya mapenzi yako hapa duniani but at your own cost, kwamba ukitenda mema utalipwa na ukitenda mabaya utalipwa.
Una uhakika na uthibitisho kwamba kilicho kufanya wewe uzaliwe ni Mungu?

Uta aminije uliumbwa na Mungu na si kitu kingine chochote kile..

Mungu ni nini?

Na muanzilishi wa hili jina Mungu ni nani?
 
Kwanza nikuweke sawa kuwa, mimi simfikirii Mungu kuwa sawa na binadamu.

Nimesema kuwa Mungu ana uwezo mwingi,akili nyingi,maarifa.mengi,ukamilifu mwingi ila kati vyote hivyo anavyo katika hali ya wingi na siyo katika hali ya ukamilifu wote (100%) ama ya kutokuwa na kikomo

Nasema hayo sija- Qoute kokote ila nimesema ni kutokana na jinsi anavyojipambanua yeye ndani ya vitabu vyake vitakatifu (rejea mifano miwili ya maswali niliyatolea mfano kwenye uzi).

Mungu angelikuwa na sifa zote hizo za ukamilifu basi hizo kasoro zilizojitokeza (zikapelekea dhambi) zingeweza kuepukika iwapo uumbaji huo angeufanya katika ukamilifu.

Zingatia kwamba, sijaribu kumkosoa/kumsahihisha Mungu katika uumbaji wake bali nataka tu kujua kwanini itokee hivo wakati yeye ana ukamilifu wote na uwezo wake hauna kikomo ?

Labda mnambie kama hizo kasoro aliziumba kwa maksudi kwa sababu anazozijua mwenyewe hapo nitawaelewa ila mkiendelea kunambia aliumba katika ukamilifu wote, hapo nitaendelea kuwauliza maswali yasiyoisha.

Mfano wako wa mpira kuwa na wachezaji 22 na kushindana kuingiza goli kwa miguuu.

Huu mfano kumbuka ni wa kanuni (sheria za kibinadamu ambazo tumeziweka wenyewe) na mara kwa mara hufanyiwa marekebisho kulingana za uhitaji.

Mfano sasahivi wanafikiria kupunguza dakika za kucheza ziwe 40 kwa kila kipindi badala ya 45.

Kwa hiyo hizi ni kanuni ambazo tumweziweka na tunazibadilisha muda wowote tutakaotaka
Ndugu inaonekana ulipendelea Mungu aumbe viumbe kama marobot, Kwamba vifanye kila kitu kutokana na matakwa yake bila kuwa na maamuzi binafsi
 
Mkuu

Ni KWELI super natural power AMBAYO waliamua kuiita Mungu IPO/yupo!


Kinachsikitisha ni kwamba:-


Africa maarifa kumhusu yaliletwa karne ya 18,ina maana waafrica waliishi miaka 1800 bila kujua Mungu wala Dini hizi za ukristo na uislam na SASA tuna miaka 223 TANGU tumfaham MUNGU wa kigeni tuliyeletewa maarifa yake!!!
NB
2023-1800=223 miaka ya maarifa ya Mungu mpya!!


Ni HIVYO tu mkuu anzia hapo kutafakari kwamba maisha ya baby zetu yalikuaje kuanzia mwaka 0 HADI 1800!!?

Tafakari!
Waliabudu nature, Ukiabudu Milima, Mito mikubwa chochote ambacho unaamini kuna nguvu kubwa ambacho imefanya hiyo cha asili kuwepo umeabudu Mungu.....So naamini watu wa kale walimuabudu Mungu kwa njia hiyo
 
Waliabudu nature, Ukiabudu Milima, Mito mikubwa chochote ambacho unaamini kuna nguvu kubwa ambacho imefanya hiyo cha asili kuwepo umeabudu Mungu.....So naamini watu wa kale walimuabudu Mungu kwa njia hiyo
Aliye pachika jina hizo nguvu na kuzijumuisha zote kwa pamoja na kuziita "Mungu" ni nani???

Zamani babu zetu walitambikia mizimu na sala,maombi yao yaka jibiwa..

Hizo nguvu zinaweza itwa pia Mizimu.
 
Ndugu inaonekana ulipendelea Mungu aumbe viumbe kama marobot, Kwamba vifanye kila kitu kutokana na matakwa yake bila kuwa na maamuzi binafsi
Huwezi kuumba viumbe usitake wawe robots but wasipokuwa robots unakasirika. Huu Ni ukichaa. Ukimpa mtu maamuzi mpe, na mbona nchi zilizoendelea ambazo hazishikilii dini Zina amani kuliko nchi za dini. Ina maanisha hauhitaji kitabu kikuambie usiuwe, we mwenyewe unaakili ya kujua kwamba kumtoa maisha mwenzako Ni kosa. Lakini akili hio hio kwa sababu ya dini ndo inafanya mtu kujilipua na kuuwa watu, kupiga watu mawe na kuangusha watu magorofani. Sasa kosa Ni Nini hapa dini au akili ya binadamu.
 
Waliabudu nature, Ukiabudu Milima, Mito mikubwa chochote ambacho unaamini kuna nguvu kubwa ambacho imefanya hiyo cha asili kuwepo umeabudu Mungu.....So naamini watu wa kale walimuabudu Mungu kwa njia hiyo
Lakini saa hivi hauabudu milima na mito kwa sababu unaelimu ya juu vinavyofunction. Elimu na internet ndo inafanya dini ionekane haina maana kwa sababu majibu ya watu wa kale sio ya sahihi na wanasayansi wamegundua vitu vingi kwa sababu wameamua kuutafuta ukweli na sio kuogopa zawadi na adhabu za kufikirika.
 
Una uhakika na uthibitisho kwamba kilicho kufanya wewe uzaliwe ni Mungu?

Uta aminije uliumbwa na Mungu na si kitu kingine chochote kile..

Mungu ni nini?

Na muanzilishi wa hili jina Mungu ni nani?
Nakujibu lakini naomba pia unijibu maswali yangu niiliyokuuliza kwenye last quote sababu huu ni mjadala wa kuelimishana na wala si kushindana so mimi pia napenda kujifunza kutoka kwako huenda nikapata kitu kipya na nikabadili mtazamo wangu.

Kwangu maandiko yanathibitisha kuwa kilichofanya mimi nizaliwe ni Mungu. Sijui wewe unaamini ni nini kilichofanya uzaliwe, unaweza nishirikisha na kunishawishi pia huenda nikaamini tofauti kama utakuja na strong points am not rigid and I stand to be corrected. Usinikatalie nachoamini bila kuniaminisha unachoamini na kunipa sababu za msingi zitakazoniaminisha. Nafikiri hapo nimekujibu swali la kwanza na pili.

Kwa uelewa wangu Mungu ni nguvu ya uumbaji na uendeshaji wa mifumo iliyopo na kila kilichopo ulimwenguni tunachokiona na tusichokiona tunachokijua na tusichokijua, beyond our knowledge and abilities, nafikiri unajua tofauti ya ulimwengu na dunia.​

Lakini according to bible Mungu ni neno. Unaweza kusoma kitabu cha mwanzo for more explanations.

Mungu ana majina Mengi ila kwa Kiswahili ndio hilo, lengo la jina la Mungu ni kumpa ukuu na kumtofautisha na vitu vingine. Ila kwa mtazamo wangu unaweza mchagulia jina lingine ambalo litawakilisha huo ukuu na haitabadilisha chochote. Nafikiri pia nimemaliza kujibu maswali yako yote​
 
Msingi wa ukristo ni matendo mema kumuelekea Mungu muumba mbingu na nchi hivo na sio kujua kama mti uliota upande wa kulia wa mto au upande wa kushoto. Inatakiwa uje hapa usema hii bible imesema kuzini ni dhambi ila hii imesema kuzini ni sawa. Halafu huo mfano uliotoa una tafsiri yake hasa kwenye kuapa pale nd moja ya mifano kutaja jina la Mungu bure kama ni ndiyo semeni ndiyo kama ni hapana semeni hapana dhamira yenu nd iwe mwanga. Na hii imeepusha wale wa kutumia haki ya Mungu na kumbe ni waongo halafu wanawaamisha wenzao vitu vya uongo.
'Ni tusitumie jina la mungu kuhalalisha ujinga wetu
 
Imani ndo huanza.
Kwani Abrahamu alikuwa na dini?
Alikuwa na Imani Wala sio dini, mara ngapi Abraham aliwadanganya Abimeleki na Farao kuwa Sara ni dada yake Ili asiuwawe?
MBONA alimuingilia Hagai bila ya kumuoa?
Wewe unaamini abrahamu alikuepo???????Mbona hautoi mifano ya wabantu??????Unatoa mifano ya watu wa jamii tofauti na yako???
 
Maoni yako wewe yakoje?


Kuna mambo bado huyaelewi.

Imani haitegemei dini. Dini ni mifumo tu iliyoanzishwa wala haina uhusiano wa moja kwa moja na imani. Kuna watu wapo kwenye dini moja lakini imani zao zimeegemea sehemu nyingine.
Ebu fafanua mkuu
 
Aliye pachika jina hizo nguvu na kuzijumuisha zote kwa pamoja na kuziita "Mungu" ni nani???

Zamani babu zetu walitambikia mizimu na sala,maombi yao yaka jibiwa..

Hizo nguvu zinaweza itwa pia Mizimu.
Mizimu ni neno la kisasa tu mkuu, kwa ukanda wa Africa mashariki kabla ya ujio wa waarabu kiswahili hakikuwepo
 
Sio kweli mkuu kwa wahindi ng'ombe wanaamini ni mizimu ya ndugu zao waliotangulia fuatilia vizuri hapo unacompare vitu tofauti.
Ebu fafanua mkuu?????? Au tumtafute muhindi atusaidie hapa???????Kwao wahindu ngombe ni mtume wa mungu
 
Ukristo gani una sanamu za kuchonga wakati biblia imekataza. Zungumzia system ya ukristo na njia zake usizungumzie eti kwa sababu katiba inasema kiongozi achaguliwe na wananchi halafu akatokea kiongozi akapindisha katiba kwa kulazimisha aongoze wananchi wewe uanze kusema katiba hii ni mbovu mbona fulani kafany hivi.
Mkuu ukrsto wa kikatoliki na kiothordox na kicoptic mkuu
 
Back
Top Bottom