Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Afu we sijui unaongea nini kwa hiyo dunia nzima isipokuwa pango la Muhammad ilikuwa bar au sio. Afu unakamia tamaa za kimwili..sio tamaa Ni natural mechanisms za evolution ambazo wanyama wote wanazo. Kwa Nini Ni kosa mi kutimiza haja zangu za kimwili. We ukiwa na njaa si unatamani kula. Mbona huachi kukidhi hio tamaa ya mwili.
 
Thibitisha kama dini ya kikristo imetetea utumwa kwa vifungu tuone hapa. Na wapi imeandikwa dunia ni flat. Wapi bible imesema tuibiane makanisani.
Dogo soma Biblia yako sawa. The four corners of the earth resting in pillars. Haya dunia ipo hivyo au. Mambo ya fungu la kumi si wizi huo. Slave obey ur masters as u obey Jesus Christ. Skia ingia Google tafuta verses condoning slavery utaziona zipo kote la kale na jipya sawa. Wakristo hamsomi Biblia yenu unaongea tu.
 
Moto wa milele usichanganye sio kuungua kila siku ila ni kifo cha milele maana mshahara wa dhambi ni mauti hivo utachomwa mpaka jivu la mwisho ndugu. Mungu atuokoe na adhabu hii.
Ni sawa na mi nakuambia nitakubaka usiponipa hela na we unatoa hela na unasema kakuokoa kutoka kwenye kibako. Siwezi weka maisha yangu kwenye control tactics za watu wa zamani wasioijua dunia.
 
Hahahahah! Kulingana na maneno yako unaonyesha dhahiri kuwa mungu kuna watu wake huwa anawachagua mapema tu ndio maana wengine anawapa neema then wengine anawazidisha maovu ili wapotee mazima ili baadae aje awaadhibu wakati uovu aliwawekea mwenyewe tena makusudi.

Halafu unavyoiona dini ni kitu kizuri yaani ni zawadi ya mungu kwa wanadamu kana kwamba tusiosali sio wa mungu na unasahau kuwa dini hizi zimefika africa karne ya 18. Je waliokuwepo hapo kabla wasiojua hizo dini mungu atawafanyaje??

Ila any way naamini mungu wa kwenye hivyo vitabu vya dini sio muumba wa ulimwengu.
 
Wewe story ya Babel Ni ya uongo soma historia ya Babylon vizuri ndo utaelewa. Na kuchanganya lugha sio sababu kwa maana hata Burj khalifa imejengwa na watu tofauti wa nchi na lugha mbalimbali na Ni refu kuliko Hilo Babel na watu wametengeneza ndege, rockets zinaenda mpaka pluto. Haya Kama Mungu yupo mawinguni mbona hakuchanganya lugha za Hawa watu wa sayansi na ujenzi wa maghorofa marefu duniani.
 
Kwaiyo badala ya kutaka ilitakiwa asitake bali afanyeje kuonesha ukamiifu wake, eti naomba kuelimishwa kidogo kuhusu sifa ya mkamilifu inatakiwa afanyeje anapohitaji jambo fulani kukamimilika iwapo hatakiwi kutaka?

Tunajadili na kuelimishana and I stand to be corrected for what I believe on.​
 
Una uhakika na uthibitisho kwamba kilicho kufanya wewe uzaliwe ni Mungu?

Uta aminije uliumbwa na Mungu na si kitu kingine chochote kile..

Mungu ni nini?

Na muanzilishi wa hili jina Mungu ni nani?
 
Ndugu inaonekana ulipendelea Mungu aumbe viumbe kama marobot, Kwamba vifanye kila kitu kutokana na matakwa yake bila kuwa na maamuzi binafsi
 
Waliabudu nature, Ukiabudu Milima, Mito mikubwa chochote ambacho unaamini kuna nguvu kubwa ambacho imefanya hiyo cha asili kuwepo umeabudu Mungu.....So naamini watu wa kale walimuabudu Mungu kwa njia hiyo
 
Waliabudu nature, Ukiabudu Milima, Mito mikubwa chochote ambacho unaamini kuna nguvu kubwa ambacho imefanya hiyo cha asili kuwepo umeabudu Mungu.....So naamini watu wa kale walimuabudu Mungu kwa njia hiyo
Aliye pachika jina hizo nguvu na kuzijumuisha zote kwa pamoja na kuziita "Mungu" ni nani???

Zamani babu zetu walitambikia mizimu na sala,maombi yao yaka jibiwa..

Hizo nguvu zinaweza itwa pia Mizimu.
 
Ndugu inaonekana ulipendelea Mungu aumbe viumbe kama marobot, Kwamba vifanye kila kitu kutokana na matakwa yake bila kuwa na maamuzi binafsi
Huwezi kuumba viumbe usitake wawe robots but wasipokuwa robots unakasirika. Huu Ni ukichaa. Ukimpa mtu maamuzi mpe, na mbona nchi zilizoendelea ambazo hazishikilii dini Zina amani kuliko nchi za dini. Ina maanisha hauhitaji kitabu kikuambie usiuwe, we mwenyewe unaakili ya kujua kwamba kumtoa maisha mwenzako Ni kosa. Lakini akili hio hio kwa sababu ya dini ndo inafanya mtu kujilipua na kuuwa watu, kupiga watu mawe na kuangusha watu magorofani. Sasa kosa Ni Nini hapa dini au akili ya binadamu.
 
Waliabudu nature, Ukiabudu Milima, Mito mikubwa chochote ambacho unaamini kuna nguvu kubwa ambacho imefanya hiyo cha asili kuwepo umeabudu Mungu.....So naamini watu wa kale walimuabudu Mungu kwa njia hiyo
Lakini saa hivi hauabudu milima na mito kwa sababu unaelimu ya juu vinavyofunction. Elimu na internet ndo inafanya dini ionekane haina maana kwa sababu majibu ya watu wa kale sio ya sahihi na wanasayansi wamegundua vitu vingi kwa sababu wameamua kuutafuta ukweli na sio kuogopa zawadi na adhabu za kufikirika.
 
Una uhakika na uthibitisho kwamba kilicho kufanya wewe uzaliwe ni Mungu?

Uta aminije uliumbwa na Mungu na si kitu kingine chochote kile..

Mungu ni nini?

Na muanzilishi wa hili jina Mungu ni nani?
Nakujibu lakini naomba pia unijibu maswali yangu niiliyokuuliza kwenye last quote sababu huu ni mjadala wa kuelimishana na wala si kushindana so mimi pia napenda kujifunza kutoka kwako huenda nikapata kitu kipya na nikabadili mtazamo wangu.

Kwangu maandiko yanathibitisha kuwa kilichofanya mimi nizaliwe ni Mungu. Sijui wewe unaamini ni nini kilichofanya uzaliwe, unaweza nishirikisha na kunishawishi pia huenda nikaamini tofauti kama utakuja na strong points am not rigid and I stand to be corrected. Usinikatalie nachoamini bila kuniaminisha unachoamini na kunipa sababu za msingi zitakazoniaminisha. Nafikiri hapo nimekujibu swali la kwanza na pili.

Kwa uelewa wangu Mungu ni nguvu ya uumbaji na uendeshaji wa mifumo iliyopo na kila kilichopo ulimwenguni tunachokiona na tusichokiona tunachokijua na tusichokijua, beyond our knowledge and abilities, nafikiri unajua tofauti ya ulimwengu na dunia.​

Lakini according to bible Mungu ni neno. Unaweza kusoma kitabu cha mwanzo for more explanations.

Mungu ana majina Mengi ila kwa Kiswahili ndio hilo, lengo la jina la Mungu ni kumpa ukuu na kumtofautisha na vitu vingine. Ila kwa mtazamo wangu unaweza mchagulia jina lingine ambalo litawakilisha huo ukuu na haitabadilisha chochote. Nafikiri pia nimemaliza kujibu maswali yako yote​
 
'Ni tusitumie jina la mungu kuhalalisha ujinga wetu
 
Imani ndo huanza.
Kwani Abrahamu alikuwa na dini?
Alikuwa na Imani Wala sio dini, mara ngapi Abraham aliwadanganya Abimeleki na Farao kuwa Sara ni dada yake Ili asiuwawe?
MBONA alimuingilia Hagai bila ya kumuoa?
Wewe unaamini abrahamu alikuepo???????Mbona hautoi mifano ya wabantu??????Unatoa mifano ya watu wa jamii tofauti na yako???
 
Maoni yako wewe yakoje?


Kuna mambo bado huyaelewi.

Imani haitegemei dini. Dini ni mifumo tu iliyoanzishwa wala haina uhusiano wa moja kwa moja na imani. Kuna watu wapo kwenye dini moja lakini imani zao zimeegemea sehemu nyingine.
Ebu fafanua mkuu
 
Aliye pachika jina hizo nguvu na kuzijumuisha zote kwa pamoja na kuziita "Mungu" ni nani???

Zamani babu zetu walitambikia mizimu na sala,maombi yao yaka jibiwa..

Hizo nguvu zinaweza itwa pia Mizimu.
Mizimu ni neno la kisasa tu mkuu, kwa ukanda wa Africa mashariki kabla ya ujio wa waarabu kiswahili hakikuwepo
 
Sio kweli mkuu kwa wahindi ng'ombe wanaamini ni mizimu ya ndugu zao waliotangulia fuatilia vizuri hapo unacompare vitu tofauti.
Ebu fafanua mkuu?????? Au tumtafute muhindi atusaidie hapa???????Kwao wahindu ngombe ni mtume wa mungu
 
Mkuu ukrsto wa kikatoliki na kiothordox na kicoptic mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…