Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Nimekuuliza kuhusu story ya Adam na Eve vs evolution. Me naweza amini the universe was created by a creator na bado nikaamini kwenye evolution na nisijicontradict. Wewe unaamini story ya Adam and eve 6000 years ago in a garden with a talking snake au huamini.
 
Na huyo highest creator katengenezwa na nani
 
Unachotaka wewe nikwamba Mungu afanye kile wewe unaona nisahihi, suala la Mungu kufanya hichi ili iwe hivi ni juu yake kwasababu yeye ndo muamuzi wa kila jambo, yani hapa Mimi nawewe tunajadili ndiyo isiyo na mwanzo na mwisho isiyo na mwisho, kwamfano Leo tungejadili kuhusu uwepo wa Mungu ...tungejadili mwanzo usiokuwa na mwisho mana tunge ulizana Mungu katokana na nini, na kilichomfanya Mungu kuepo kimesababishwa na nini? Kwa maana hii tungerudi mwisho usiokuwa na mwanzo, itoshe kusema kuwa kazi ya Mungu haina makosa, ameamua ndio iwe ndio na sio iwe sio, upingamizi wetu haubatilishi uwezo wake kamwe.
 
Hakuna lolote ninalotaka mimi zaidi ya kuhoji na kuthibitisha tu, kuangalia logical consistency katika dhana ya kuwepo Mungu.Inaonekana dhana ina contradictions ambazo hazijatatuliwa.

Ninaelezea "logical consistency" tu. Kwa mujibu wa maelezo ya dhana ya kuwepo Mungu, haya si maneno yangu, si ninachotaka mimi, ni wanaosema Mungu yupo wanavyosema.

Haya si mambo ninayotaka mimi, ni maelezo kuhusu uwepo wa Mungu yanavyosema.

Tunaambiwa:-

1. Mungu ni muweza yote.
2.Mungu ni mjuzi wa yote
3. Mungu ni mwenye upendo wote.

Mpaka hapo hakuna ninachotaka mimi, hizo ni sifa za Mungu kwa mujibu wa wanaoamini Mungu yupo.

Halafu, tunaona kwamba kuna ulimwengu ambao una mabaya, unaruhusu mabaya kutokea.

Hili si jambo ninalotaka mimi, ndivyo ulimwengu ulivyo.

Mpaka hapo hakuna ninachotaka mimi, nimeeleza sifa za Mungu kwa mujibu wa waamini, na ulimwengu ulivyo kama tunavyouona.

Sasa nauliza swali tu, hapa sisemi kwamba nataka ulimwengu uwe hivi au vile, nauliza swali kutafuta logical consistency, kuhakiki na kuelewa tu.

Kama Mungu ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, imekuwaje kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Hujajibu swali hili, unaniambia nisimpangie Mungu kuumba ulimwengu ninavyotaka mimi, sijampangia, nauliza kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana, na hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Hujajibu swali hili.

 
Hapana mkuu bado unang'ang'ania kwamba Mungu angeumba ulimwengu ambao mabaya yasingewezekana, na wakati yeye ameumba ulimwengu ambao mabaya na mazuri ni chaguo la waishio ndani ya ulimwengu, mbona wewe unatakq angeumba ,unavyotaka wewe ili kukuridhisha wewe? ,,,,,,na imagine hapa kama Mungu angekupa choices kwamb nikuumbe vipi Kiranga bila shaka ungechangua kuwa more than God, kwasababu wewe unaonekana ni mbishi na hautaki kabisa kuelewa kabisa kuhusu Mungu,na hii inasababishwa na sababu zako binafsi ambazo hata haziwez kuathiri au kugairisha kaz zake
 
Mimi binafsi naamini Mungu katika kristo, kna mambo ya ki-Mungu ambayo nimekosa majibu yake hadi Leo ila bado naendelea kumwamini hivyo hvyo ,Moja ya mambo hayo ni kama vile
1.Nimefundisha kuwa Mungu anajua mambo yote yajayo, hvyo naamini kuwa wakati anawaumba malaika alipaswa kutambua kuwa kna malaika angekuja kumsaliti ili azuie hilo lakini hakuzuia, alipaswa kutambua kuwa akimuumba Eva atakuja kuharibu ili azuie ila hakuzuia.
2.Mungu anajua hatima ya Kila mmoja wetu, Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa kna mmoja atamsaliti na petro aliambiwa atamkaja Yesu na kweli ikatokea,means isingetokea Yesu angeonekana Muongo na reputation yake ingepotea, kwaiyo Kuna vitu tushapangiwa kuvifanya hata tukwepe vipi Sasa kosa letu liko wapi jaman,nishapangiwa kuwa ntakuja kuwa mzinzi ,kosa langu liko wapi kuwa natenda dhambi wakati ndo nishapangiwa hvyo?
 
[emoji1][emoji1]
 
Story ya Adam na Eve ndiyo Creation theory,.. ambayo Mimi nimesema naamini hiyo story kuliko Evolution Theory.
 
Na huyo highest creator katengenezwa na nani
Ukisoma Sifa za Highest Creator Utagundua kwamba Swali lako Linakufa automatically kabisa, KWASABABU YEYE NDIYO CREATOR/DESIGNER WHO BROUGHT ALL THINGS INTO EXISTENCE,.. HE IS THE CREATOR OF ALL ENGINEERS.

Hivyo basi, Creator of Everything.... Ili awe Creator of Everything hawezi kutengenezwa na kitu Kingine.
 
True Kila nikiimagine hayo maswali napoteza focus kabisa na nakuwa kama sioni maana yoyote ya kuishi
 
Mkuu,

Ngoja nikupe mfano rahisi sana labda utanielewa vizuri.

Wewe, kwa hiyari yako mwenyewe, ukisema huwezi kukosa penati kwenye mpira, halafu tukaona unacheza mpira ukakosa penati, tukikuuliza kwa nini umekosa penati wakati wewe mwenyewe umesema hukosi kufunga penati, tutakuwa tunang'ang'ania kuwa ungefunga penati kwa matakwa yetu au tunakuhoji kwa nini umekosa penati wakati wewe mwenyewe ulisema hukosi penati?

Nikikuhoji kwa nini hujafunga goli la penati, wakati ulisema huwezi kukosa kufunga goli la penati, hapo utasema mimi nalazimisha ninavyotaka mimi ufunge penati, wakati wewe mwenyewe ndiye uliyeanza kusema kwamba huwezi kukosa kufunga penati?

Mtu anayehoji kwa kutafuta logical consistency utasemaje analazimisha anavyotaka yeye?
 
Ila we huoni ukisema hivi ni kisingizio Cha kila kitu. Niambie tofauti ya dunia yenye Mungu na isiyo na Mungu. Kama vitu vizuri vipo na vitu vibaya vipo.
 
Asante.
 
True Kila nikiimagine hayo maswali napoteza focus kabisa na nakuwa kama sioni maana yoyote ya kuishi
Jamani kwani maana ya kuishi ni kwenda mbinguni mbona dini Zina waharibu hivyo. Life is short n finite ishini maisha yenu vizuri, hii ndo maana ya kuishi.
 
Kwa Nini asitengenezwe katokea wapi? Hii Ni imagination tu kwa sababu tumeshindwa kufikiria so tunapambikiza creator. Huyo creator alikuwa wapi wakati anatengeneza, why lazma awe being. Most importantly why lazma aabudiwe na awe na heaven na hell kutishia watu. Na Kama yupo ulimwenguni yupo wapi na Kama yupo nje ya ulimwenguni bac hayupo
 
Story ya Adam na Eve ndiyo Creation theory,.. ambayo Mimi nimesema naamini hiyo story kuliko Evolution Theory.
Creation myths zipo nyingi duniani za tamaduni mbalimbali wagreek wanayo ya Pandora, kina Vikings wanazo, kina mesapotemia wanayo ya epic of Gilgamesh ambao wayahudi wameedit kuwa Adam n Eve. Sasa why unaamini creation myth moja Kati ya zote duniani, una hakika gani ilikuwa Adam na Eve kwa udongo na mbavu na ibilisi ndani ya bustani yenye miti ya maajabu, una ushahidi gani juu ya hii story kuizidi zingine nyingi za uumbaji. Sababu yako ni moja tu dini yako bac, lakini ukimfuata muhindu atakupa story nyingine ya uumbaji, kwa Nini usiamini hiyo. Uzuri Sayansi haijipingi, haichagui sehemu Wala tamaduni, ndo maana nasema Bora nikubali kitu chenye evidence na worldwide acceptance kuliko kitu chenye myths.
 
Safi sana ndg! Kwa namna ambavyo umeleta hoja za kumfanya mtu kufikiri na kutaka kujua zaidi kuhusu nguvu ya asili hisiyo ya kawaida yaani (Mungu) na kwa nn kumekuwepo na mapungufu pia katika Malaika na Ubinadamu kulingana na Biblia. Mimi nafikir Wahubiri wengi wangekuwa wanajiuliza vzr kuhusu haya maswali yako na kuyaleta vzr mbele za watu ingekuwa rahisi sana watu kumuamini Mungu kwa uhakika na wala wasingewadanganya watu na kuchukua pesa zao wakilinganisha pesa bila kutenganisha Uungu au maisha ya mbinguni. Sasa basi ukitaka kujua kuwa Mungu ni mkamilifu na hana mapungufu ya kufikirika inafaa kwanza tumuamini kuwa yupo Imani ni hisi ya sita katika zile tano ambazo tumekuwa tukizitumia katika maisha haya ya kawaida hapa dunia na hii inamuhusu Mungu pekee.
Kiimani - 1. Mungu alikuwa na sifa za zote kabisa ikiwepo kuwa Mungu Mkuu mwenye mamlaka, Mkombozi, mponyani, mwenyehaki, Mwenye Upendo Mwenye Amani na vitu vingine vikamilifu vyote tunavyovijua. Sasa basi hisingewezekana kuvidhihirisha vitu vyote hvyo wakati kila kitu nikikamilifu Mbinguni na duniani yaani Malaika wote wawe wakamilifu wenye nguvu kamilifu bila mapungufu na tujue Malaika ni viumbe katika kiwango flan kisicho cha kibinadamu hivyo ili Mungu aweze kuonyesasha sifa yake ya Ukuu na Nguvu ilibidi uhasi uwepo ili yeye awe upande wa ukombozi na Nguvu namna ile ile alivyotenganisha Maji ya Bahari na nchi kavu.
2. Mwanamke(Hawa) kuwa mdhahifu ni ili tu kuruhusu kosi lifanyike ili jamii ya mwanadamu kuingia dhambini alafu yeye Mungu mkamilifu mwenye sifa ya ukombozi kudhihirisha sifa yake iyo. Alafu kitu ambacho sayansi si muda mrefu imedhibitisha ni iki hapa.. Walikuwa wanasema kiumbe chenye ukaribu sana na mwanadamu ni Sokwe mtu lakini hakuna uwezekano wa Sokwe kumuongezea damu mwanadamu kuonyesha kwamba hakuna ukaribu wa hvyo. Lakin inaonekana kuna gape katiya Sokwe na Mwanadamu kwamba hapa katika kuna kiumbe kingine ndio biblia inatupa jibu kuwa kabla ya Mungu kumlaani nyoka alikuwa na ukaribu sana na mwanadamu na ndie aliyeweza kumdanganya Hawa na kuweza kuchanganya damu na kupata uzao.. Baada ya Hawa kukutana na Nyoka na baadae Adamu kulitokea uzao watoto wawili walizaliwa Kaini na Abil ikiwa Kuwa Abili alikuwa mtoto wa Adamu na Kaini mtoto wa Nyoka hii inadhibitika zaidi katika maisha yao. Kumbe kunawezekano wa mama kubeba mimba ya wababa wawili tofauti kwa wakati mmoja na watoto wakazaliwa kila mmoja na baba yake imetokea Uganda na sehemu zingine.. Hvyo kwa maelezo hayo tunaweza kuona Mungu ni mkalimifu mwenye sifa zote zikiwepo hizo zinazoonekana ni udhahifu ili baada ya maisha haya aturudishe kwenye maisha yasikuwa na mapungufu..Asante
 
Hapa mtu huwezi chomoka...jamaa kabana kote kdk
 
Hataki Mungu wenu wa kutunga na mwenye sheria according to tamaduni mbalimbali miaka ya kale
 
We nakuachia kiranga akukoshe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…