Hakuna lolote ninalotaka mimi zaidi ya kuhoji na kuthibitisha tu, kuangalia logical consistency katika dhana ya kuwepo Mungu.Inaonekana dhana ina contradictions ambazo hazijatatuliwa.
Ninaelezea "logical consistency" tu. Kwa mujibu wa maelezo ya dhana ya kuwepo Mungu, haya si maneno yangu, si ninachotaka mimi, ni wanaosema Mungu yupo wanavyosema.
Haya si mambo ninayotaka mimi, ni maelezo kuhusu uwepo wa Mungu yanavyosema.
Tunaambiwa:-
1. Mungu ni muweza yote.
2.Mungu ni mjuzi wa yote
3. Mungu ni mwenye upendo wote.
Mpaka hapo hakuna ninachotaka mimi, hizo ni sifa za Mungu kwa mujibu wa wanaoamini Mungu yupo.
Halafu, tunaona kwamba kuna ulimwengu ambao una mabaya, unaruhusu mabaya kutokea.
Hili si jambo ninalotaka mimi, ndivyo ulimwengu ulivyo.
Mpaka hapo hakuna ninachotaka mimi, nimeeleza sifa za Mungu kwa mujibu wa waamini, na ulimwengu ulivyo kama tunavyouona.
Sasa nauliza swali tu, hapa sisemi kwamba nataka ulimwengu uwe hivi au vile, nauliza swali kutafuta logical consistency, kuhakiki na kuelewa tu.
Kama Mungu ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, imekuwaje kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Hujajibu swali hili, unaniambia nisimpangie Mungu kuumba ulimwengu ninavyotaka mimi, sijampangia, nauliza kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana, na hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Hujajibu swali hili.
View attachment 2610255