Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Mkuu kwanini unataka kumchunguza au kumjua Mungu kwa njia hiyo? Unauwezo mkubwa sana kiakili kwanini kwanini usiwekeze kwenye vitu vinavyo onekana? Kwanini unataka kuonyeshwa kwa vitendo mambo ambayo misingi yake ni imani.. kuhusu Mungu wewe amini tu .. maana hata ukichunguza kwa njia hiyo hakuna siku utajua kitu........ KAMA UNATAKA KUMJUA MCHUNGUZE kwanjia ya imani
 
Imani ni Nini?
 
Mi najiuliza maswali mengi. Mungu Ni Nini, anataka Nini na Yuko wapi.

Ukifuatilia historia ya binadamu tokea tukiwa wawindaji maporini miungu ilikuwepo. Wazee walikuwa wanaongoza vijana kwa kuwaambia kuwa Mungu anataka mfanye hivi, na hio miungu ilikuwepo pangoni ambapo wazee tu wanaingia, baadae vijana wakajitoa akili kwenda wakaona wazee ni waongo na hamna kitu mule. Wagiriki wakaja na miungu yao wakasema ipo ya milima ya Olympus.

Leo hii watu wamepanda milima yote ugiriki hawajaona miungu hio. Wakaja wayahudi, wakasema Mungu yupo mawinguni. Ukifuatilia hata Yesu alipaa mawinguni, Mungu alifungua madirisha ya mbinguni kuleta mafuriko, alichungulia kutoka mawinguni kwenye mnara wa babel, etc. Waislamu nao wakaja na mbingu Saba sijui. Anyways wazungu wametengeneza ndege na rocket zimeenda mawinguni, nje ya dunia, mpaka mwezini. Sasa hivi watu wa dini wanasema yupo nje ya ulimwengu.

So nikagundua trend, wanamficha, wanamweka mbali ili watu wasiweze kumfikia, why? Kwa sababu hayupo? Kwa sababu hajasema hizo sheria? Why wanamficha. Afu wanakuambia anataka uamini yupo ndo utapona usipoamini unaunguzwa. Ukiuliza nikimwona afu nikamwamini, anasema no, lazma usimwone ndo uamini. Na wanaweka kifo mwisho wa kumuani ili waweze kuendelea kutunga sheria kwa jina lake na kuweza kuendelea kutawala watu kwa sababu hamna mtu Ashawahi kurudi akasema baada ya kifo kipo hivi. Mwanasayansi mi nauliza Mbinguni Kuna Nini.

Hamna njaa hamna maumivu hamna ndoa hamna chochote zaidi ya kumuabudu Mungu. Watu kanisani na msikitini hawapendi kwenda unategemea watapenda milele ya Ibada. So wakaamua kuanzisha motoni kutishia watu kwamba wataunguzwa milele. Sasa, ukifa unaacha mwili wako hapa, wanasema una roho, roho ni Nini, hoo mawazo sijui pumzi, ukiuliza unajua kazi ya ubongo ni Nini mtu hajui, haya tufanye roho ni ka upepo kanaenda motoni ehe kanaunguaje, hakana nyama, hakana nervous system hakana ngozi, hakana pain receptors, hakana ubongo au spinal cord, maumivu unayasikiaje, na bado hatujauliza huu Moto upo wapi, walisemaga chini kisa mavolcano lakini now hawasemi Tena coz of elimu.

Tukienda kwenye sheria zenyewe sijui usivae nguo tofauti, usile shellfish, usichanganye mazao, usimwage nje, usiabudu sanamu lakini abudu kitu Cha kufikiriwa na myahudi, hivi kwa Nini mtu atengeneze nyota billion 60 na sayari trillion afu aje kujali binadamu wewe ambae ni Kama vumbi kwa huu ulimwengu unamwaga wapi. Na kwa Nini sheria hizi zinaonekana Kama sheria za kabila ya la zamani huko kwenye majangwa na haziendani na sheria za binadamu kuishi na watu vizuri. Na Wanavyosema tumuabudu siku ya Saba.

Siku zimekuja kutengenezewa baadae Sana na zimebadilika badilika Mara kwa Mara katika historia ya Mayans na Romans. Na wamechagua sun day coz ni siku ya pagans kuabudu jua. Ila yote haya tuyaache, why Mungu muweza yote anataka hela, mwisho wa siku wote mnabidi mgundue kuwa binadamu walitengeneza miungu ili kujibu maswali magumu yasiyojibika kipindi kile na kuwatawala watu kwa ujinga na hofu.
 
Sasa kwenye hiohio kesi, huyo mtu alielawiti ni shoga (gay rapist).
Kwa wanyama wao hawana idea ya 'mapenzi' wao ni kufanta tendo tu basi..
 
Umepuliza alafu ukang'ata. Akaufanya moyo wa falao kuwa mgumu, akamwadhibu falao na Misri yote.
 
Unaweza kusema una nguvu lakini hayupo unaeshindana nae ?
 
Kuwepo kwa vitu ulimwenguni sio uthibitisho wa kuwepo kwa Mungu, if that's the case maana yake na yeye pia ana creator kwa sababu unaamini ili kitu kiwepo lazima kiwe na creator, so kama ana hiyo equation ya creator itaendelea to infinity.

Yawezekana kweli kuna creator wa vitu na science (hata dini majibu ni mepesi mno) haina majibu ya moja kwa moja, lakini kumbuka hiyo ni science ya leo, hatujui knowledge ya miaka 1000 ijayo yawekana tukawa na jibu

Ywezekana kukawa na creator or creators etc hakuna mwenye jibu la moja kwa moja si dini wala science, so kuamini uwepo wa Mungu kisa umeona vitu ni mere belief tu.
 
Uko sahihi kuwaza hivi, ila trust me shida imeanzia kwenye hii equation.

Our knowldge is still limited, ndio maana tunawaza hivi.
 
Mungu wa kwenye vitabu vya dini ni Mungu aliyetengenezwa na binadamu, yuko tofauti na Mungu alieumba dunia na vitu vyake
 
Wewe unamfahamu Yeye ashindaye? Unamfahamu mtumwa muaminifu?
 


Mimi naomba uifanyie summary hii mada (weka maswali yako yanayokusumbua) kisha uniruhusu kukujibu kwa mujibu wa Dini ya Kiisilamu.

Maana yangu ni hii; You need to try in Islamic perspective.
 
Wakuu poleni kwa upambanaji.

Binafsi mimi kuna mda huwa nikitulizaga kichwa changu huwa naanza kujiuliza maswali mengi sana kuhusu mimi (binadamu) na ulimwengu kiujumla (Universe)...
Nimesoma mitazamo ya watu kibao kwenye huu uzi hadi sasa sijapa jibu kwa maana najiuliza maswali kama yako


Sitaki kuamini sayari zote gaĺaxy zote universe nzima ni binadamu pekee ndio tunachomwa

Halafu walioandika bible waliiandika kipindi hakuna elimu yoyote ndio maana wamesema mungu kaumba dunia jua na mwezi hawazungumzii sayari nyingine zozote

Nafikiria pia kuhusu mambo ya dunia inakuaje na ying na yang kwanini kila kitu kisiwe sawa? Kwanini kuna watu wanatesekana na wengine wanainjoy?? Ni kweli ukimsujudia shetani utapata mali na pesa kama wanavyosema freemason?? Kwa maana hata biblia inasema yesu alijaribiwa na mali

Pia kwanini mungu aumbe binadamu kwa dhumuni la kuwachoma? Si anaijua kesho maanayake anajua anachokifanya

Ninahisi kuwa hakuna anayecontrol kitu chochote kinachoendelea ulimwenguni yote yanaoendelea ni matokeo ya vitu vinavyotokea ulimwenguni na kwa sababu kila kitu ni energy including human na energy haijawai kutengenezwa wala kufa ni inabadilika tuu means kwamba hata sisi hatuna mwanzo wala mwisho ni tutabadilika tuu kwenda kwenye form nyingine (labda ndio spiritualy iguess)

Ni mtazamo wangu tuu hata mimi pia nahitaji maelekezo kwa wajuzi wa haya mambo
 
Finishing nzuri naomba huu Uzi ufungwe maana umemaliza Kila kitu mkuu.
 
Hicho kinachofanya ushindwe kuelewa ukamilifu ndo ukamilifu wake sababu wewe na yeye level tofauti kabisa .
 
Hata hivyo alivyoumba sio kwa ukamilifu, na kwa wengine" kwanini wengine wawe wakamilifu, na wengine wasiwe na ukamilifu, hawa watakua kundi, gani??
 
Tuseme yupo ila ana mapungufu yake. Angekuwa na uwezo angemuua shetani ili tuishi kwa amani. Wafia dini watasema Mungu ana sababu zake za kumuacha shetani.
 
Una miaka mingapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…