Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

siamini pia kama kweli kuna huo moto wa milele
Moto wa milele usichanganye sio kuungua kila siku ila ni kifo cha milele maana mshahara wa dhambi ni mauti hivo utachomwa mpaka jivu la mwisho ndugu. Mungu atuokoe na adhabu hii.
 
Binafisi siamini katika habari za moto wa milele kwamba kuna sehemu roho za binadamu zitachomwa milele.

Hizi habari za mbinguni na motoni ni aina ya reward and punishment system iliyowekwa ili kuleta hofu na kuweza kutawala watu kwa njia nyepesi. Kwamba ukifanya kama tunavyotaka utazawadiwa na ukifanya kinyume basi utaadhibiwa.

Na ili kukamata watu zaidi wakamtengeneza mungu wa kufikirika na kusema yeye ndio mwazilishi wa hayo yote, na kulazisha watu wamuani huyo mungu na kumuacha Mungu wa kweli.

Kwa kifupi Mungu hayupo kama wanavyo muelezea kwenye vitabu vingi vya kiimani.

Kuna mtu aliwahi kuniambia njia nzuri ya kujifunza mambo ya kiimani ni through experience, achana na mambo ya kusoma rundo la vitabu ambavyo vimeyumbishwa na wanadamu kwa maslai binafsi.
Lete hayo maslahi binafsi kwenye bible yanamlenga nani hapa. Maan bible inatufundisha upendo wote tuko sawa( wote hakuna cha mchungaji wa kuhani wala muinjilist) na tuko chini ya Mungu mmoja kupitia kwa kristo Yesu. Tuambie bible inamfavour nani utakuwa umechanganya maandiko bro.
 
Safi umeanza kupevuka kiakili niseme sio watu wengi hujiuliza kwa undani hivi. Mimi nami katika kujibu maswali ya watu huwajibu kulingana na level yao.

Usitetereke kiimani hata mimi naamini uwepo wa Mungu. Lakini yakupasa kujua kuwa Mungu tunayesoma habari zake vitabuni (Biblia, Quran) sio yule Mungu halisi kwani ameelezewa kulingana na jinsi mtu flani alivyoona, ndio kusema ni vigumu kumwelezea Mungu kwa utimilifu wake kwani kuna tatizo kubwa la kumwelewa Mungu (epistemological problem).

Ni kweli yeye ni mkamilifu na mweza wa vyote ameumba vyote na kuvipa uhuru ikiwa ni pamoja na shetani. Shetani au mwanadamu akitumia uhuru wake kufanya ubaya Mungu hawezi kulaumiwa.

Ubaya au uovu ni jinsi unavyoona wewe tu niseme in absolute terms hakuna kitu kama hicho! Kwani simba akila swala ni uovu? Je simba akila mtu ni uovu! Au mtu akila swala ni uovu? Mtu akila ndizi ni uovu? Na je mtu akila mtu ni uovu?

Ni “hatari “ kutaka kumjua sana Mungu na unatakiwa uwe na uelewa flani wa mambo la sivyo utaishia kuwa hovyo. Nitaachia hapo kwani kujua kunaambatana na majukumu makubwa.
Hakuna cha unavoona wew au cha nini. Nd maan kuna police pia hawa wote wanajaribu kulinda interest za watu wote. Sas unafananisha binadama na wanyama kweli. Mnyama anaweza ua kutokana na kukutana na mtu mgeni au kiumbe mgeni lakini wewe unajua kabisa nkikutana na mtu mgeni naweza kufanya hatua gani huwezi ukakutana na watu kariakoo ukaanza kupanic tu hapo na kukimbia kimbia au kuua ua tu hovyo na ndo maan binadamu unaweza ukaona kwamba hili eneo lina wanyama hatari ukaona uhame sehem nyingine una magari na misaada na mawazo ya watu unawezaje kujifananisha kimaamuzi na myama.
 
Kuhusu magenius wengi..huna hizi statistics so huwezi prove hilo. Kingine huwezi fananisha maisha ya mwanamke wa dunia ya saa hivi na zama za kale, walikuwa viumbe duni ndo maana dini zote zinasema wawe dhaifu kwa wanaume kwa sababu ndo utamaduni ulivyokuwa kipindi kile. Sawa Kuna technology za hapa na pale lakini hazijaletwa na dini. Pyramids hazizajengwa na dini, wagiriki waliogundua vitu vingi walikuwa hawaamini mingu ndo maana waliweza kuwaza vitu na kufikiri. Dini Inampa binadamu majibu na inamwambia asiulize maswali. Wakati Sayansi unauliza maswali na unatafuta majibu yaliyosahihi na yanayopimika kila Mara.
Je waisrael wenye dini hawana mchango kwenye mapinduzi ya science na technlojia. Hujui kuwa hizo pyramid zilijengwa na wayahudi hujui kuwa miji mikubwa ya zamani imejengwa na wayahudi hujui kuwa mataiamfa makubwa kama marekani roman empire zote akina germany yamechangiwa sana na wayahudi. Fuatilia asilimia kubwa ya wagunduzi wa dunia wana asili ya kiyahudi. Kwann dini isianze kuwapumbaza wao wewe mwafrica sayansi nd imekucost unasingizia dini. Wewe ilitakuwa ulime umeenda kuiga techologia zinazowafaidisha watu wasio na nyenzo nyingine kwenye ardhi zao.
 
Kuhusu magenius wengi..huna hizi statistics so huwezi prove hilo. Kingine huwezi fananisha maisha ya mwanamke wa dunia ya saa hivi na zama za kale, walikuwa viumbe duni ndo maana dini zote zinasema wawe dhaifu kwa wanaume kwa sababu ndo utamaduni ulivyokuwa kipindi kile. Sawa Kuna technology za hapa na pale lakini hazijaletwa na dini. Pyramids hazizajengwa na dini, wagiriki waliogundua vitu vingi walikuwa hawaamini mingu ndo maana waliweza kuwaza vitu na kufikiri. Dini Inampa binadamu majibu na inamwambia asiulize maswali. Wakati Sayansi unauliza maswali na unatafuta majibu yaliyosahihi na yanayopimika kila Mara.
Yani tatizo wewe ndugu unachanganya mafundisho sana nd inakucost. Yani unachukua kipengele kimoja cha dini unaongezea na tabia za watu. Kwenye bible yakobo alifundishwa kuchunga na mama yake haya aliwezaje kuchunga kama alikuwa useless. Kulikuwa kuna maqueen zamani kulikuwa kuna wanawake waubiri. Hujui kuwa kwnye bible kuna kitabu cha esther na pia kuna fundisho linasema ushindi uko kwa mwanamke. Halafu mwanaume anaemcha Mungu atamuheshimu mkewe kama anavowaheshimu watu wengine. Yule bibi alietoa kipande kidogo cha fedha alitoa wapi ela kama walikuwa hawajishughulishi. Na je kwann wanawake walikuwa wanatoa sadaka hata enzi hizo. Hujui kuwa Yesu alikutana na malkia wa shiha na nd alikuwa mtawala mkuu wa ethiopia na wala Yesu hakumkemea wala nini. Sayansi iliyowaambia dada zenu wajisnap tiktok imewaletea dada zenu makalio bandia lips bandia instagram imewaletea wanaume uke bandia ndo tamu sana ila kwako wewe dini tu nd yenye tatizo. Amka kijana amka unapotea mwafrica sayansi nd imekupa umasikini wa kutisha hutaki kulima unataka ukae daslamu.
 
Kuhusu magenius wengi..huna hizi statistics so huwezi prove hilo. Kingine huwezi fananisha maisha ya mwanamke wa dunia ya saa hivi na zama za kale, walikuwa viumbe duni ndo maana dini zote zinasema wawe dhaifu kwa wanaume kwa sababu ndo utamaduni ulivyokuwa kipindi kile. Sawa Kuna technology za hapa na pale lakini hazijaletwa na dini. Pyramids hazizajengwa na dini, wagiriki waliogundua vitu vingi walikuwa hawaamini mingu ndo maana waliweza kuwaza vitu na kufikiri. Dini Inampa binadamu majibu na inamwambia asiulize maswali. Wakati Sayansi unauliza maswali na unatafuta majibu yaliyosahihi na yanayopimika kila Mara.
Wewe dini hujasoma vizuri unanyapia nyapia tu navoona. Maandiko yameleta uhusiano wa kiroho kati ya mwanadamu na Mungu na pia uhusiano wa kiroho na mwili kati ya mwanadamu na mwanadamu mwenzie ila kwa akili yako unahisi basi watu walikuwa hawapigi hata story wala hawacheki wala hawachezi na ndo maan unaconclude science haikuepo. Maengineer wenu wanajisifu kwa skyscrapers wakati mnara wa babeli watu waliupandisha juu sana mpaka wakachanganya lugha sababu nia yao ilikuwa ovu. Watu walivuka kwenye maji sio kwa miujiza watu walichimba dhahabu watu watengeneza silaha watu walijenga mapyramid hayo watu walitengeneza mavazi na kila kitu ila wewe unahisi watu walikuwa wanasali tu tuu hakuna maendeleo. Kama hujui maendeleo mengi yametokana na hao waliopata siri za Mungu mwanzoni watu wamefundishwa technology mpaka na akina zeus ambao walikuw ma nephilists. Ila uko kulaumu muafrica dini nd imemfirisi wakati waarabu na hao wazungu sio maskini sababu mpaka wakaleta huku it means walijifunza kwanza wao kwann wasiwe masikini kwanza wao.
 
Uwepo wa mambo wa ya ajabu ambayo yanakosa maelezo ndio chanzo cha mwanadamu kufikiri uwepo wa nguvu kubwa kuliko yeye ulipoanza.

Na naona kabisa kwenye kutafuta ama kutaka ushirikiano na nguvu hio kubwa kila mmoja alipata experience yake kama nilivosema awali.

Sasa hapo utaona kutokua na uwezo wa kueleza matukio ya aina fulani watu hao wakakabidhisha uwezo huo kwa kitu kingine Tunaita MuNGu na wakaanza kuhalalisha mambo mengine humo ndani, ambayo hayana uhusiano na uwezo wa mungu kuumba na kufanya mambo makubwa.

Mfano; unaweza kuta kundi fulani la watu wanawachukia watu fulani kwa sababu zai binafsi tu ili waeneze hio chuki kwa watu wengine watasema, watu wenye tabia fulani ni chukizi kwa mungu muumba mbingu. Sasa chuki yako na uumbaji wa mungu wapi na wapi.

Kutoka 20:7 Inasema usilitaje jina la bwana mungu wako bure.
Ukisoma biblia tafsiri ya KJV inasema
"You shall not take the name of the LORD your GOD in vain"

Biblia tafsiri ya J.B ROTHERHAM
"Thou shall not utter the name of the yahweh your GOD for falsehood"
Akimaanisha usitumie jina la mungu kuhalalisha mambo yako ya kipimbavu.

Ukiangalia history biblia ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali ambavyo watu fulani waliona mafundisho yake yanafanana fanana ama lengo la waandishi hao tofauti tofauti ni kama lilikua moja.

Ndio maana unakuta kuna matoleo mbalimbali ya biblia na yote waandaaji watakuambia waliongozwa na roho mtakatifu ili kukusanya vitabu hivyo.

Na je kama roho ni mmoja mbona awaongoze makusanyo yalio tofauti?, mbona waprotestanti wawe na vitabu kiasi fulani kwa biblia zao, mbona mayaudi wa kanisa la orthodox maybe wakubali mafundisho ya vitabu mfano vitabu vya enoch lakini waprotestant waseme vitabu hivyo havijavuviwa na roho mtakatifu, ni roho mtakatifu gani aliwavuvia waorthodox.

Ukiangalia fact kwa umakini hapo utakuta kuna interest za watu kwenye kuupata ukweli ndio maana ukweli halisi huwezi upata kwenye hivyo vitabu zaidi ya kuongeza maarifa juu ya mambo fulani tu.

Hata kristo alitoa onyo juu ya maandiko
Yohana 5:39-40....
Maandiko pekee hayatoshi bali kumtazama yeye kuutazama ukweli, ukweli ndio utatuweka huru. Na tukubaliane labda tungekua na toleo la kwanza la biblia huenda tungefahamu uhalisia wa mambo yalivyo lakini kwa hii tuliyonayo sasa imechezewa sana, kuna interest ya makundi ya watu fulani sana na wamehalalisha mambo kwa mgongo wa MUNGU.

Nimeegamia upande wa biblia sina ufahamu sana kwenye quran. Tuna mengi ya kujifunza sana mkuu.

Na kuegamia sana vitabu vya dini kujifunza ukweli ni kuishia kua mfia dini.
Msingi wa ukristo ni matendo mema kumuelekea Mungu muumba mbingu na nchi hivo na sio kujua kama mti uliota upande wa kulia wa mto au upande wa kushoto. Inatakiwa uje hapa usema hii bible imesema kuzini ni dhambi ila hii imesema kuzini ni sawa. Halafu huo mfano uliotoa una tafsiri yake hasa kwenye kuapa pale nd moja ya mifano kutaja jina la Mungu bure kama ni ndiyo semeni ndiyo kama ni hapana semeni hapana dhamira yenu nd iwe mwanga. Na hii imeepusha wale wa kutumia haki ya Mungu na kumbe ni waongo halafu wanawaamisha wenzao vitu vya uongo.
 
Mabaya ni adhabu kwa kuasi kwasababu mabaya yote adhabu yake ni kifo.
Wakati Mungu ana muumba mwanadamu, Hakujua kwamba ipo siku mwanadamu atamuasi na kufanya mabaya?

Kama alijua uasi utakuja kutokea kwa nini alisubiri hadi utokee asi uzuie tangu mwanzo??
 
Hakupanga tujue mema na mabaya ndugu. Mema na mabaya ni adhabu ya uasi wa kwanza kuwa usile tunda la katikati ya mti.
Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Hakujua kwamba Uasi utakuja kutokea?

Yeye si hujua yote?

Alishindwaje kujua kwamba ipo siku binadamu atakula tunda la katikati amzuie asile, Badala yake ali acha hadi binadamu akala???
 
mimi nipo mwanza but i've got your point. Mkuu naongelea hatima ya mtu either jehanamu au peponi na kwa mfano wako umeongelea kupajua tu kwa majina na sio kufika au kupapitia


Kumbuka mungu ndio muumba sio tupo under him kabla hajakuumba anajua wewe ni wa jehanamu tu so huwezi change na ikitokea yeye alijua kuwa ni wa jehanamu ila ulipozaliwa ukatumia maombi kama ulivyodai ukaenda peponi hapo tunaiterm kama alikuwa hajui maana yeye kabla haujazaliwa alijua wewe ni wa jehanamu but umebadilisha ukawa wa peponi kwa maamuzi yako but something that's impossible


Hauwezi kuchange hatima anayoijua mungu since he is your designer you can never go beyond his expectations buddy!
Kwaiyo unafikiri Mungu ni rigid hawezi kubadili hatma yako sababu unaamini anajua hatma yako, yaani kiufupi unaamini Mungu hafanyi reasoning kwenye maamuzi yake?

Yaani hata kama umetenda mema basi yeye atakupa tu adhabu ili atimize hatma yake juu yako?

Em fikiria kama wewe binadamu aliekuumba you can make reasoning na kubadili maamuzi yako au hatma yako, je yeye si zaidi yako?
 
S
Hayo mabaya kama hayapendi yeye si Mungu muweza wa vyote, Alishindwaje Kuto kuumba Dunia isiyo na mabaya??

Mabaya ambayo humsababisha mwanadamu ayafanye...
Sasa hayo ya kutokuumba au kuumba hakushindwa ila ni mapenzi yake na sio yako na hakuna wa kumpangia kama ambavyo hukumpangia wewe uzaliwe au usizaliwe, uwe na jinsia me au ke hayo yote ni mapenzi yake ambayo yapo nje ya uwezo wako,

Ndio maana kakupa nawewe uhuru wa kufanya mapenzi yako hapa duniani but at your own cost, kwamba ukitenda mema utalipwa na ukitenda mabaya utalipwa.
 
Kwani mwalimu akijua kuna kilaza darasani akatoa mtihani na akajua fulani atafeli hyo ina tafsiri gani na influence ya mwalimu juu ya mwanafunzi huyo?
ni either teacher alitoa mtihani mgumu ambao wenye uwezo mdogo hawawezi japo kuna maswali mengine angeyaleta au mwalimu hajui kufundisha ndio maana sio wote walioelewa


Nb: mimi sijaongelea mitihani mungu aliyotupa mimi naongelea kutuumba sisi bila uwezo ya kufaulu mitihani yake na mbaya zaidi anajua hata kabla hataumba na bado anakuumba ili uje ukosee tu
 
Hapana wala haipo hivyo, nimesema ni uongo kwasababu hata wewe unajua hilo sio jibu sahihi.
Lakini we pia huna jibu sahihi so unaassume..Ni Kama walivyoassume mvua Ni madirisha ya mbinguni kumwaga maji kabla hawajajua mvua Ni natural process.
 
Lakini hamna kitu ambacho binadamu atafanya kinachostahili kuungua milele. Hii adhabu imewekwa na dini ili kuendesha watu. Hazikuwepo katika agano la kale. Ndo maana wanajua kwa hii adhabu wote mtakubali kuendeshwa na wanaosema dini imewafata wao
Mimi vitu vingi navyoongea hapa ni kutokana na uelewa wangu binafsi sija quote maandiko ya dini japo yamenisaidia kuwa na uelewa huu nilionao.

Kuhusu adhabu hata mimi kuna muda huwa najiuliza kwanini Mungu ahangaike kuumba kitu ambacho kina mapungufu alafu aje akiteketeze. Lakini pia pengine maandiko sio makamilifu kutokana yaliandikwa na mwanadamu.

So kuna muda naona kufuata nafsi yako kunasadia ndio maana kuna msemo unasema matendo mema ndio dini ya kweli.
 
Msilaumu wengine kwa matokeo yenu. Kama dini ililetwa kwanini hamkuwa matajiri miaka yote wala hamkuwa na technology kubwa kuwazidi wenzenu. Mmekuja kudanganywa na sukari na sabuni kweli nyinyi nd mngetoboa hata kujua kuna kujenga nyumba kweli au barabara au madaraja au hata kujua kusoma na kuandika tu. Vyoo vyenyewe mmefundishwa kutumia mgeweza kutengeneza fedha au baishara au ndege spaceships kwelii? Ichukieni dini kwa mambo mengine ila sio kwenye failures zenu. Kwanza dini gani inakataza watu kuendelea binafsi tuanzie hapo lete na vifungu.
Dini inakupa majibu. We mwafrika si alijua mbingu Ni mawinguni According to bible. Haya mzungu kaenda mwezini. That's just one example out of all, wazungu wanaweka dini pembeni kwamba kila kitu kinawezekana na majibu yanapatikana kwa utafiti sio maneno ya watu wa zamani.
 
Je wazungu hawana makanisa? Hayo makanisa ya africa mangap yamejengwa na wazungu? Je nyinyi ambao hamuhamini dini tuonesheni viwanda vyenu. Waafrica tunafeli mambo mengine ila tunatafuta kichaka cha kujifichia mara siasa mara dini na tusipoacha kulaumu watu au dini tutakaa hivi hivi miaka yote.
Nchi nyingi za Ulaya na marekani Zina population kubwa ambao haiamini dini, na wanasayansi wengi hawaamini dini na ndo wameleta maendeleo. Fuatilia sawa
 
Kuna stori tofauti kutokana na uasi shetani kuvuruga mambo ila sasa dini nzuri ni ile yenye matokeo chanya kwa wanadamu. Kukataza dhambi kama vile uzinzi na uasherati uuaji uongo kutokuheshimu wazazi kutamani mali za wengine( haya nd mambo muhimu ya kuangalia kwenye matokeo ya dini zilizopo)
Nieleze kwa Nini uzinzi Ni kosa? Kwa akili isiyo ya dini.. niambie why.
 
Back
Top Bottom