Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri tuu! , Ila...

Wangemrekebisha angewatumbua palepale kwa hiyo ilikuwa ni lazima wamshangilie tu
 
Ngoma ndio hii hapa chini.
Natumaini umeelewa, kama bado una maswali zaidi, tuendelee.
P.
 
wanashauri wanaomshauri aseme nanukuu 'kichaa kama mimi' kweli hao ni washauri kweli kweli....
 
NAONA UMEANZA KUBADILI MWANDIKO...aisee unajua kung'ata na kupuliza!!! you are talented mayalla
 
Inje ya sheria na katiba yetu turudi kwenye neno lenyewe ushauri.

Kinachotofautisha neno "ushauri" na neno "amri" ni kitu kimoja tu kuwa amri inakulazimu kufanya vile ulivyoambiwa na mtoa amri, wakati ushauri unakupa nafasi ya kupuuza, kuchukua sehemu ya ushauri mengine ukapuuza ama kufanya sawasawa na ulivyoshauliwa maamuzi ni yako, na mtoa ushauri hapaswi kunung'unika kwa hatua yoyote utakayo chukua.

Ni nani unaweza sema huyu hashauriki? Mtu asiechukua muda wake kusikiliza wengine wanasema nini, yule anaekuwa mkali kwa mtoa ushauri, anae jenga chuki kwa mtoa ushauri kisa hajapenda ushauri au ushauri haumpendelei yeye.

Ukimaliza kunishauri nenda zako niachie niamue mwenyewe likibuma ni langu, hakuna anejua ningefanya ulivyoshauri madhara yangekuwa kiasi gani so usihuzunike wewe umefanya kazi yako ya kushauri basi inatosha.

Let jpm do jpm, akifanya kama kikwete huyo ni kikwete sio jpm tena.

Lkn akivunja sheria zetu au katiba yetu tutasema.

Haya tunayoyalaumu kwake leo ndio utakuwa utambulisho wake.

Hata kwa mwalimu Nyerere yalikuwepo yasiyopendwa but leo ndio sifa na utambulisho wake. Hivi unadhani wanachuo (wakina spika sitta) walifurahia kuchapwa viboko kwa kudai haki zao vyuoni? Familia za waliowekwa kizuizini zilifurahi? Walionyimwa haki ya kugombea urais (marecela, lowasa n.k) unadhani walifurahi? Lkn hiyo ndio ilikuwa nyerere let jpm do jpm sisi tulinde katiba, sheria, Uhuru na haki zetu basi.
 
Pasco ushauri ulifuatwa????
Kwenye hoja hizi,
Naamini alishauriwa vizuri na alifuata ushauri ndio maana husikii tena lolote kuhusu US na EU resolutions on Tanzania.
P
 
Wanabodi
Bandiko hili ni kuhusu rais wetu kutoshauriwa vizuri kwenye baadhi ya maeneo.

Tukio la kukamatwa na kushikiliwa kwa ndege yetu na kuzuiliwa nchini Africa Kusini ni matokeo ya rais kutoshauriwa vizuri.

Kwanza kudaiwa sio kosa, kosa ni kushindwa kulipa madeni halali au madai halali.

Hii sio mara ya kwanza kwa sisi Tanzania kama nchi kudaiwa au mali zetu kuzuiliwa. Kama Richmond tulidaiwa na tukalipa, ndege yetu ilipozuiliwa Canada, tulilipa, huyu Beberu Steyn alipotudai tulilipa tena tumekula ng'ombe mzima tumebakisha tuu mkia, nani alimshauri rais wetu tusimalizie kulipa?. Huu ulikuwa ni ushauri sahihi?.

Naomba tukiisha ikomboa ndege yetu na ikarejea nyumbani, lazima tukae chini tuulizane nani alishauri nini, kama kuna watu wa kuwajibika, wawajibike.

Pia sasa tufanye tathmini ya madeni yetu hatarishi ya nje ya nchi na tutalipe kabla ya kuendelea na safari za nje, usikute saa hizi baada ya watu kusikia tunajipanga kutua London, watu wako tayari na makaratasi yao mezani na muhuri mkononi wakisubiri tuu itue, muhuri unagongwa na ndege yetu inadakwa!.

Nini kilichofanya tusiendelee kumlipa deni lake Beberu Steyn?.

P
 
“Niguse ninuke”
Ninawasikitikia washauri wanafiki na waoga wanaokaa kimya au kumshauri vibaya Rais wetu.
Bernard K. Membe. Mstaafu!"
Naamimi ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri.
P
 
Wanabodi, msikilizeni jinsi rais Magufuli anavyohutubia vizuri wakati anaposoma hotuba aliyoandikiwa. So far hotuba hii mpaka hapa alipofikia, is one of the best. Akisoma mwanzo mwisho bila kuchomekea, he will be the best, ila kwa vile bado anahutubia, huwezi jua atachomokea nini.

Lets hope for the best, chochote atakacho chomekea ni kuendeleza uzalendo na Umoja wa kitaifa.

Hongera sana Magufuli
Mungu Ibariki Tanzania.
P
 
Kwa leo amehutubia vizuri,,hotuba iliandaliwa vizuri,,
 
Vijembe vinawekwa mwishoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…