Naamini, Rais Samia Suluhu asingekuwa madarakani Royal Tour isingekuja Tanzania

Naamini, Rais Samia Suluhu asingekuwa madarakani Royal Tour isingekuja Tanzania

Royal tour ni tofauti na tunavyoichukulia, kama kweli maandalizi yake hadi kukamilika kwake kumegharimu zaidi ya tshs. 7bn basi kuna kitu kingine kikubwa zaidi kilichojificha nyuma ya hiki kilichobatizwa kama royal tour
 
Imani yangu inanituma kwamba, wazo la kuja na kutengeneza Royal Tour Tanzania, nimechochewa zaidi na Tanzania kuwa na Rais Mwanamke.

Licha tu ya kuwa na Rais mwanamke ambaye kwa nchi za magharibi ni kitu ambacho wanavutiwa nacho zaidi, lakini pia aina ya siasa anayofanya Rais Samia inamtafautisha sana na mtangulizi wake, John Pombe Magufuli ambapo nafasi ya Royal Tour imetumika kama njia ya kurekebisha diplomasia ya Tanzania na mataifa mengine, na ni kweli, hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Binafsi na hisi hivyo.
Ni kweli kabisa! Raisi pekee mwanamke mwenye mamlaka kamili - nafikiri Dunia nzima hakuna Raisi Mwanamke. Tanzania imepata bahati ya kuwa na mtazamo mpya, hata kwenye familia baba na mama mitazamo yao huwa inatofautiana.
 
Royal Tour(s) ni siasa (program ya kisiasa)

Zinawatangaza (brand) zaidi viongozi wa serikali kuliko vivutio vya utailii

Na Royal Tour ya TZ iko kumtangaza zaidi Samia

Dunia ijue sasa Tanzania inaongozwa na raisi mwingine, tena mwanamke, ambaye yuko tofauti kabisa na mtangulizi wake (yaani JPM)

Mama anajitangaza kwa wazungu laiti kama atapigiwa kura na wazungu 2025
 
Back
Top Bottom