Naandika uzi huu kwa masikitiko makubwa sana: Kwanini mtu ufurahi kujihusisha na Shetani?

Naandika uzi huu kwa masikitiko makubwa sana: Kwanini mtu ufurahi kujihusisha na Shetani?

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Napata masikitiko makubwa moyoni ninapoona baadhi ya watu katika forum hii wakijitambulisha kwa majina ya kishetani au yanayohusiana na uchawi. Nauliza kwa unyenyekevu lakini kwa uchungu wa rohoni: Kwa nini mtu achague jina la kumtukuza shetani, ambaye ni adui wa nafsi za wanadamu wote?

Ni kweli kwamba mtu anapata amani ya kweli moyoni akiwa chini ya utambulisho unaomhusisha na ibilisi? Je, hatujui kuwa shetani hana huruma wala upendo, na kazi yake ni kuiba, kuchinja, na kuharibu?

Tumeisahau kweli ya maandiko? Si imeandikwa wazi kwamba mwisho wa shetani ni kutupwa katika ziwa la moto, yeye pamoja na wote wanaomfuata? Mtu akijiambatanisha naye, si anachagua hatima hiyo hiyo kwa hiyari yake mwenyewe? Kwanini?

Kwa nini mtu ajivunie jina au utambulisho wa kiumbe aliyelaaniwa na Mungu, badala ya kumtafuta Yesu ambaye anatoa uzima wa milele?

Jamani, shetani ni muongo, muongo, muongo. Anaweza kukushawishi uwe mfuasi wake, akakuahidi kukupa na mapesa mengi. Lakini huo ni mtego. Anataka uangamie pamoja naye milele.

Nauliza tena, kwanini mtu ajiite jina linalomtukuza shetani? Mtu anapata faida gani? Ni kutafuta umaarufu? Ni kwa mzaha? Au ni kwa kutojua tu?

Huu ni wakati wa kutafakari, kutubu, na kurudi kwa Mungu wa kweli kabla milango ya neema haijafungwa.
Mambo yanayotokea duniani nyakati hizi ni udhihirisho wa wazi kuwa Yesu amekaribia sana kuja kuwachukua watakatifu na kuwapeleka mbinguni.

Itakuwa kilio na kusaga meno kwa wale watakaoachwa. Tumkatae shetani anayetaka tuteseke duniani, halafu tena tuteseke milele motoni.
 
Yesu anasema hivi katika Ufunuo 3:20-22:
"Tazama! Nasimama mlangoni nabisha. Kama mtu yeyote akisikia sauti yangu na kufungua mlango, nitaingia ndani na kula pamoja naye, naye pamoja nami. Yeye ashindaye nitampa haki ya kuketi pamoja nami kwenye kiti changu cha enzi, kama vile mimi nilivyoshinda na nikaketi pamoja na Baba yangu kwenye kiti chake cha enzi. Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa.”
 
FB_IMG_1749134985918.jpg
 
Bro Setfree labda au kabla ya kuwa Set free, unahisi ww ungechagua/ungekuwa jina gan?

Kwahiyo na sisi tuliochagua majina ya hovyo kuna muda utafika na tutakuwa set free kama wewe.

Namuamini Mungu.

Nakusindikiza na hili neno bro wangu.
Lisome lote.

Mathayo 7 : 1-12

B2565051-C58D-4100-8658-BCE6E63E3B59.jpeg
 
Pole wenzako ila tunasikitika utekaji kwa sasa
 
Bro Setfree labda au kabla ya kuwa Set free, unahisi ww ungechagua/ungekuwa jina gan?

Kwahiyo na sisi tuliochagua majina ya hovyo kuna muda utafika na tutakuwa set free kama wewe.

Namuamini Mungu.

Nakusindikiza na hili neno bro wangu.
Lisome lote.

Mathayo 7 : 1-12

View attachment 3357426
Castle_Lite
Comment yako imenitia moyo sana. Kumbe, sababu ndiyo hiyo. Basi usikawie bro, mwambie Yesu aku set free leo leo, ili ikitokea akarudi usiku wa leo uwe miongoni mwa watakaonyakuliwa.
 
Back
Top Bottom