Oa mwanamke uliyejiridhisha kuwa utaishi naye, hii biashara ya kuachia familia maamuzi juu ya mwanamke wa kuoa sio poa aseeeee.
Ukumbuke ni wewe utakayeishi naye. Ukifuata Kila wanalokuamulia wanafamilia ipo siku maamuzi unayotakiwa kufanya wewe kama baba wa familia yako utaachia wanafamilia wakuamulie.
Mbinu mojawapo rahisi ya kujua mwanamke wa kuoa fuatilia undani wa maisha ya pale alipolelewa /kukuzwa. Ukiona mama mkwe dishi limeyumba basi ujue bintiye ana asilimia nyingi dishi limeyumba pia.
Usioe mwanamke ambaye mnala ni wa voda halafu network inasoma tigo.
Usioe mwanamke kwa kumuonea huruma utakuja kujuta siku huruma yako juu yake ikifikia kikomo