Naapa kutomkopesha Mtanzania hela mpaka naingia kaburini

Naapa kutomkopesha Mtanzania hela mpaka naingia kaburini

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
1. Mligo wa njombe 600000/=
2. Evodi wa kibaha 100000/=
3.Elibariki wa moshi kati ya 280000/= umenirudishia 15000/=
4. Dotto wa kibaigwa 45000/=
5. Mama Thadeo wa ilemela 68000/=

Haya madeni yana miaka miwili na zaidi Mungu atanilipa. Ila mligo wa njombe ushapata adhabu yako hapahapa duniani maana nasikia u-mlevi wa kupindukia hata familia inakushinda.

Watanzania hawalipi madeni usithubutu kuwakopesha hela.
 
Sitasahau Shangazi yangu mmoja aliniambia nimpe kama 500k niitoe kwenye michango ya Harusi ya brother nilikuwa ndio mtunza fedha ili amalizie Ada atarudisha....Shangazi akatokomea na harusi hakujaga akaniachia Deni wanakamati wakanijia juu ikabidi nilipe.
 
Kuna jamaa alianza kunikopa elfu 5 jion akanirudishia baada ya siku mbili elfu 20 jion akanirudishia , baada ya wiki elfu 50 jioni akanirudishia ikaenda kwa staili hiyo hiyo hadi ikafika laki 5 jion ananirudishia kumbe bana alikua ananirudishia hela yangu ileile nayomkopesha asubuhi wala alikua hata haitumii

Mara ya mwisho akataka million 1 nikamwambia sina akanishusha hadi laki 6 nilivyompa tu akasepa nayo jumla
 
Kuna jamaa alianza kunipokopa elfu 5 jion akanirudishia baada ya siku mbili elfu 20 jion akanirudishia , baada ya wiki elfu 50 jiona akanirudishia ikaenda kwa staili hiyo hiyo hadi ikafika laki 5 jion ananirudishia kumbe bana alikua ananirudishia hela yangu ileile nayomkopesha asubuhi wala alikua hata haitumii

Mara ya mwisho akataka million 1 nikamwambia sina akanishusha hadi laki 6 nilivyompa tu akasepa nayo jumla
Alikuwa anakujaza kwenye mfumo na ukajaa kweli 😂

Ukiona mtu anaanza na utaratibu huo jua anajijengea uaminifu ili aje akulize. Wengi wanakopa ndogo hawazitumii, anakaa nayo adi siku kabla ya ahadi ya kurudisha haijafika anakurudishia hata kabla ya muda ili uone huyu ndio mtu mwaminifu, jichanganye sasa ujute.
 
Mi nawapa sana hela hadi leo nimewapa acha
Screenshot_20240812-104953.jpg
 
1. Mligo wa njombe 600000/=
2. Evodi wa kibaha 100000/=
3.Elibariki wa moshi kati ya 280000/= umenirudishia 15000/=
4. Dotto wa kibaigwa 45000/=
5. Mama Thadeo wa ilemela 68000/=

Haya madeni yana miaka miwili na zaidi Mungu atanilipa. Ila mligo wa njombe ushapata adhabu yako hapahapa duniani maana nasikia u-mlevi wa kupindukia hata familia inakushinda.
Watanzania hawalipi madeni usithubutu kuwakopesha hela.
kuna mtu nilikuwa naye utotoni, ni mtoto wa mama yangu mdogo, nyumba yao hii, inayofuata ya kwetu, alinikopa pesa kadhaa miezi kama 4 imepita, anapokopa alisema just in 10 days zinarudi, aongeze kwenye biashara yake. nilimpa, sikumkumbusha baada ya siku 10 nikampa hadi mwezi nione kama anakumbuka au la. mwezi wa kwanza nikapiga, hata simu hapokei, miezi4 sasa, hata simu hapokei itaita hadi ikatike. imebidi ninyamaze tu nikiamini pengine atakuwa amekutana na changamoto na anaona aibu kuchelewesha. zaidi sana ni ndugu yangu angenielekeza tu shida aliyokutana nayo ningemwelewa.
 
1. Mligo wa njombe 600000/=
2. Evodi wa kibaha 100000/=
3.Elibariki wa moshi kati ya 280000/= umenirudishia 15000/=
4. Dotto wa kibaigwa 45000/=
5. Mama Thadeo wa ilemela 68000/=

Haya madeni yana miaka miwili na zaidi Mungu atanilipa. Ila mligo wa njombe ushapata adhabu yako hapahapa duniani maana nasikia u-mlevi wa kupindukia hata familia inakushinda.
Watanzania hawalipi madeni usithubutu kuwakopesha hela.
Sio wote Kaka. Mimi Willy wa Gongola Mboto huwa ananikopesha hadi Milioni 5. Na huwa namrudishia ananikopesha tena...kwakweli yule jamaa huwa ananiokoa sana nikiwa na Shida.

Msitunyime msaada jamani
 
Back
Top Bottom