Naapa kutomkopesha Mtanzania hela mpaka naingia kaburini

Mikopo ni changamoto sana, inakosesha sana amani na kuna namna unajawa na ugumu wa kulipa.
Muhimu ni kujitahidi sana kutokukopa au kukupa sehemu ambayo hautakuwa na udhuru wa kutolipa.
Ila kuapa na kuazimia kutokukopesha maisha yako yote ni kujidanganya, maisha hayana njia nyoofu ya moja kwa moja , kesho imebeba mengi mno.
 
Mnakopesha kwani nyie ni taasisi za kutoa mikopo? Mambo mengine ni kujitakia tu, mwambie aende taasisi za kukopa, huko kuna vigezo na masharti, akizingua wanamzingua. Unampaje mtu 1m usawa huu, unategemea nini, taasisi zipo..twende tukakope huko.
 
Achana na watanzania, wasambaa ndo nyoko, hawalipi madeni kabisa.
 
Hahaha hahaha

Ova
 
Wala sikupingi...ila huwa wanakuja huku wanalia. ( Huruma inaponza).

Hata wewe unayesoma hapa, kama unadaiwa LIPA, acha kupenda mseleleko.
 
Subiri mfugo wangu ukue ntakulipa yahe
 

Attachments

  • Screenshot_20240812-102448_1.jpg
    319.3 KB · Views: 3
Nilishasema nikija kukopesha basi dhamana ni hati ya nyumba au chochote kisichohamishika. Na mwanamke labda nimsaidie tu ila simkopeshi hata iweje.
Unachukua hati ya nyumba kwani una leseni ya kutoa mikopo? Unaweza kufanya hivyo na bado sheria ikakubana.
 
HuYo wa Ilemela nipe location nimudai,au nipe namba zake nimfuate
 
Nimepiga hesabu hapa ,unadai 1,078,000, Hongera sana kwa kuwa na moyo mzuri, watu kama nyie mko wachache sana, mnahesabika kabisa
 
Kama huna Hela usikopeshe hicho kidogo ulichonacho bora utoe damu tu unatamani watu wafe kisa mkopo uliowakopesha..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…