Naapa kutomkopesha Mtanzania hela mpaka naingia kaburini

daaaaah ume nikumbusha kitu
 
Naunga mkono hoja maana hata mimi silipi wanaonikopesha
 
Kama unaweza na mtu amekuja kukopa kwa sababu ana shida, hata kama atashindwa kurudishia, mshukuru Mungu kwamba uliweza kumsaidia mtu mwenye shida. Usiweke moyo wako kwenye hela, kama unaweza kumsaidia mtu (hata kumkopesha kwa vile hana) usisite kufanya hivyo. Mungu atakubariki zaidi. Mungu huwabariki zaidi wanayotoa, kuliko wanaopokea. Take note of this!
 
kama nnayo ni either nikupe kiasi kidogo au kama nina mipango hapo karibuni nakunyima. mkopo unaleta matatizo mengi sana
 
Hao wote waunge kwenye group la whatsap alafu admin mpe mfanyakazi wa pesa x utakuja kunishukuru hapa huku unabubujikwa na machozi
 
Dawa ya hawa akija kukuomba mkopo wa Laki tena mtu unaemjua
Unampa elfu 10 bure unamwambia kajazie mbele
Usikope mtu akileta umasikini zaidi mpe za uso tu
 

Naapa kutomkopesha Mtanzania hela mpaka naingia kaburini.​

Kwahiyo watu wa mataifa mengine unaweza kuwakopesha?
 
Daah.. mwenyewe nilipigwa 450,000 ya michango kwa mtindo huu huu. Mbaya zaidi alienipiga ni bwana harusi! Alikuja na gia ya kwamba anadaiwa 200k ya kumalizia suti na 250k ya gauni la bibi harusi na yeye hana kitu. Akaniambia ndani ya wiki 1 hela yake inatoka ofisini atarudisha. Mpaka tunaenda kikao cha mwisho hela hajaleta, kamati inataka mahesabu. Kulinda heshima yangu ikabidi nitoe tu.
 
elimu ya fedha inatakiwa kw mkopaji na mkopeshaji.
mtu anakopesheka kama ana dhamana(collateral),ko haina aja ya kukimbizana.

biashara ya kukopesha ni nzuri sana kama umezingatia vigezo.
 
Maskiniiini kwahiyo harusi yake suti yake deni la kwako!!!!!?
 
Mimi nampa mtu mkopo ambao asiponilipa hata sihangaika kumdai yani ile pesa ambayo haiumi sana kuanzia buku tano hadi laki. nje ya hapo ni vigumu.
 
Atakuwa mimi huyo maana ghafla wadau wote wa JF wamekuwa wakopeshaji wala si wakopeshwaji.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Wewe ndio tatizo sio wao. Ukienda Benki kukopa benki wanakopesha biashara yako sio wewe. Sasa wewe hukuangalia wadai wako shughuli zao za uchumi ukawapa kama unampa mjomba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…