Naapa kuwa sirudii tena kumsaidia Mtanzania -- never!

Pole sana kwa hayo uliyopitia baada ya kutoa msaada, ila usisite kutoa msaada pindi unapokutana na mhitaji na uko kwenye nafasi nzuri ya kumsaidia. Binadamu tunatofautiana sio wote wana tabia hizo kuna wengine ni very smart!
 
😆😆😆😆
 
Nilipoandika mambo haya niliyapima maneno yangu nikayathibitisha kuwa ni kweli.

Soma hapo👇👇👇

 
Kwanini unahisi jambo hilo haliwezekani kiongozi.....mbona ni jambo la kawaida kwa wanadamu....
Anayepajuwa Park station itakuwa ngumu sana kuamini hii tamthilia.

Hizo ni sehemu tunaoijuwa vizuri Johannesburg tulikuwa tukipita huku tunakimbia kwa kujifanya kama tunapunguza winter mwilini kumbe unajilinda na majita.

Kama kuna sehemu ya mind ur business basi ni Joburg, ndio maana hii hadithi imenishangaza sana.
 
Ukweli wake ni upi?
 

Sijui tunakwama wapi sifa zetu ni mbaya sana
 
Asante kwa kutujuza kiongozi......Mungu atamlipa mleta mada kwa kadri ya dhamira ya moyo wake.....
 
Sijui tunakwama wapi sifa zetu ni mbaya sana
Mswahili hata ukifanya naye biashara akishika pesa mkononi anaona ni za kwake, Binafsi nina tabia ya kununua matunda kila siku, ninapomwambia muuzaji anichagulie, hunichagulia matunda mabovu, nikimuuliza kwanini unafanya hivi anasema "mbona haya mazima kabisa" Hili jambo hunishangaza sana! Yaani hawezi kutofautisha mazima na mabovu?

Kumbe akili ya ushwahili akuuzie yaliyochoka ili abaki na mazima ayauze kesho!!! Mtu anakuja kukukopa na ahadi ya kwamba mzigo ukitoka atalipa, weee mzigo unatoka anaanza kukuzungusha huku anajua kuwa na wewe unazungusha kama yeye.
WASHWAHILI HAWAFAI KABISA.
 
Sasa wewe tukuweke kundi la wazungu?
 
Sijui tunakwama wapi sifa zetu ni mbaya sana
Mtaumiza akili na vichwa vyenu bure, South Africa ndio chimbo pekee ambalo ni rahisi kwa hawa Notorious wetu wa Bongo kukimbia Bongo na kuingia huko kwa njia za panya na wengine hufia njiani kwa kuuliwa na viboko wakati wa kuvuka mito hatari.

Haiwagharimu kiasi kikubwa cha pesa kuingia huko maana hawahitaji hata kupita official borders au airport, wao ni waruka fence ( South Africa border yote wamepiga wire fence.)

Kwahiyo chimbo hilo tegemea tabia zote za kishenzi unazozijuwa wewe Bongo utakutana nazo huko, dawa ni kukaa mbali na Wabongo kama una mishe zako na wazungu au mataifa mengine.

Hii ni tofauti na Europe na USA, process za kuingia hicho hizo zinawanyima fursa wajinga wengi kutobowa huko unless aingie kwa kuzamia meli, na kwa teknolojia inavyoshamishiri nadhani hata uzamiaji meli utafika tamati.
 
Hakika mkuu, kila tunapojaribu kuwabeba ndugu zetu hawabebeki.
 
Pole sana Dudumizi. Ila huyo kijana ni umbwa kabisa. Hana maana. Ataishia kutangatanga tu. Na asipokuwa makini atauawa. Umbwa kabisa yeye.
Nahisi atakuwa ameshikwa masikio na yule mwenyeji wake baada ya kugundua kuwa kijana anaweza kuwa mtaji kupitia vile vifaa vya saloni. Asichofahamu kijana ni kwamba anaweza kufika kule wakauza vifaa alivyoenda navyo, afu baadae mwenyeji akambadilikia na kumtelekeza barabarani.
 
Sister.. ma gape kama haya tuna watu wana uhitaji nayo sana sana, nikuombe usikate tamaa kwa ajili ya watu wachache unaweza ukawa msaada kwa watu wengi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…