Naapa kuwa sirudii tena kumsaidia Mtanzania -- never!

Wakomoro wapo tayari kufanya biashara na mkomoro mwenzao lakini sio mbongo.....

Nenda bandarini pale wanaofanya biashara comoro ni wacomoro wenyewe
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kisa nn
 
Wabongo ni watu wa ajabu saana,mwaka jana niliingia mkataba na vijana wa kazi za shamba.Nililima maharage kama hekari 12 hivi.Tumeenda nao vizuri, mpka maharage yalipo komaa na kuanza kukauka.. nilikuwa natembelea kila baada ya siku tatu..kuna siku nilipata dharula hivyo nikawa nimesafiri kama wiki nzima,ile wiki vijana walivuna maharage yote na kupiga..wakaacha kwa jirani gunia tatu tu.. zingine zote wametokomea nazo..nmewatafuta mpaka leo sijawapata..ila nmewasamehe Mungu atawalipa.
 
Habar zenu ndugu zangu. Ama baada ya salam ningependa kuendelea na kile kilichonifanya niandike uzi huu. Ndugu zangu kama ilivyo ada au kama tulivyofunzwa na misingi yetu ya Taifa kwamba watanzania popote tulipo haijalishi ni ndani au nje ya nchi, sisi ni watu wamoja. Kwahiyo kwa misingi hiyo sisi tulio nje huwa na desturi au utamaduni wa kusaidiana bila kujali tofauti zetu za kikabila, dini, rangi, jinsia au kanda ya mtu anayotokea ilimradi sote ni watanzania na tunatokea kwenye ardhi ya Tanzania basi ni ndugu.

Sasa basi miezi 3 iliyopita kuna kijana aliingia Kaburu akitokea bongo kwa lengo la kuja kutafuta maisha. Kijana anadai kuna rafiki yake wa kitaa, kwa sasa anaeishi Capetown ndio alimshawishi kuja maisha haya, lkn alipoingia tu "Kaburu" yule rafiki yake akamzimia simu na kumkosa kabisa online.

Kijana akachanganyikiwa asijue wapi pakwenda wala nini cha kufanya. Nikiwa katika mizunguko yangu mitaa ya park station Johannesburg, ghafla nikapita sehem na kumuona kijana akiwa kajiinamia na begi lake huku machozi yakimtoka. Nikamsogelea taratibu na kujaribu kumuuliza kwa lugha ya wenyeji, ghafla nikasikia jamaa akiongea kiswahili, hii ikanipa nguvu ya kumsogelea na kumuuliza zaidi baada ya kugundua kuwa naongea na mtu anaetoka nchini kwetu. Baada ya maongezi ya hapa na pale nikagundua kuwa jamaa ameingizwa cha kike na mwenyeji wake, kwahiyo nikachukua jukumu la kumsaidia.

Nikaondoka na jamaa hadi nyumban, akaoga, akala, baada ya kula nikampa sehem ya kupumzika akalala. Kwa kuwa mimi nina familia ikanibidi niende kuongea na homeboy fulan ambae ni single ili ampe hifadhi ya miezi kadhaa wakati nikiendelea na mchakato wa kumtafutia shughuli ya kufanya, mshikaji akakubali lkn kwa masharti ya kumsaidia kulipa rent.

Kwa kuwa nilikuwa nimeamua kumsaidia kijana, basi nikaona poa tu acha nimsadie kulipa rent ili aweze kuishi nae. Kijana tumekaa nae mwezi wa kwanza, wa pili na sometimes nilikuwa naenda nae kwenye mishe zangu ili kumzoesha mazingira ya nchi, na mishe za hapa na pale. Mwezi mmoja uliopita kuna rafiki angu Mkenya ambae tuliwahi kufanya nae kazi huko Gezina, Pretoria.

Mkenya alikuwa anatafuta mtu wa kumuachia saluni yake kubwa na ya kisasa iliyopo nje kidogo ya jiji la Pretoria huko Nellmapius, kwa malipo ya R600 kwa week (sawa na sh elfu 85 au elf 90) kula na kulala bure. Kwa vile nilikuwa na kijana na tayari alishanambia kuwa bongo kazi yake kubwa ilikuwa ni ukinyozi, nikaona YES maji ya mvua yameangukia juu ya mgongo wa bata. Nikampanga kijana, kesho yake mapema nikampeleka mpaka Pretoria kwa yule Mkenya na kumkabidhi.

Kweli bwana baada ya siku mbili kijana akaanza kazi huku Mkenya akiniomba nimtafutie vijana wengine ambao wataenda kusaidizana nae, maana saluni ni kubwa ilihitaji vinyozi zaidi ya watano, lkn pia kijana lugha ni tatizo, so alitaka ambao wangeweza pia kusaidiana hata katika mambo ya lugha za wenyeji ili kuwateka vizuri wateja wa kizawa.

Nikamuahidi jamaa kumtafutia hao vijana. Wakati namuacha kwa yule Mkenya kijana wang nilimuachia sim kwa ajili ya mawasiliano yetu, au ndugu zake wa bongo, au boss wake (Mkenya). Dogo tukawa tunawasiliana ananipa taarifa za kazi na mimi nampa mpa moyo kuwa akomae ili atimize malengo ya kile kilichomleta hapa nk. Siku tatu zilizopita sikumpata online, nikajua labda simu imepata tatizo ghafla.

Sasa jana yule rafiki angu Mkenya amenipigia simu na kuniambia kuwa jamaa amemuibia kila kitu cha saluni, na hela ambazo yule Mkenya anaendaga kuzichukua kwa week jamaa katimka nazo. Simu yake haipiti na hatujui tutamtoa wapi. Nilipotaka kumlipa yule Mkenya nusu ya hasara ya vitu alivyoiba jamaa, Mkenya amkataa amesema nisijali kwa vile sio kosa langu ni kosa la mtu mungine kwahiyo mimi sistahili kumlipa na ukizingatia na rafiki yangu.

Hiki kitendo cha huyu jamaa kimenisononesha na kunivunja nguvu. Imenifanya sasa niwachukie wabongo wenzangu, maana hii ni mara pili sasa nawasaidia wabongo afu wanaharibu na kutimkia kusikojulikana, japo kwa huyu sikutegemea hata kidogo kutokana na upole na muonekano wake.

Najua binadamu tunatakiwa tusamehe, lkn kwa mikasa hii sioni sababu ya kusamehe kwa lengo la kurudi kumsaidia mungine labda yule nimjuae A to Z. Ndugu zangu wabongo tubadilike, hii dunia tunapita tu. Kumuharibia mtu anaekusaidia sio ujanja bali ni ujinga wa mwisho. Hii ni tahadhari nimetoa kwa vijana wengine kuwa makini sana. Asanteni
Mkuu pole ...mbali na Utanzania....vijana wengi was Saluni au Vinyozi wanatatizo makubwa ,waulizr wamiliki was Saluni....huyo tofauti yake n mjanja kavuka border
 
Imagine, wakenya ni mabingwa wa wizi lakini wakimwona mbongo huko Kenya hasa wachagga wanamwogopa balaa maana wanajua kupigwa ni nje nje.
wanijeria wanaosifika kwa wizi na mtandao mkubwa wa kitapeli duniani. Sehem wanayopigia mishe zao, wakiona kuna wabongo wawili watatu wamejisogeza eneo hilo basi wanajeria wanaihama hiyo sehemu ili kunusuru biashara zao.
 
Mkuu pole ...mbali na Utanzania....vijana wengi was Saluni au Vinyozi wanatatizo makubwa ,waulizr wamiliki was Saluni....huyo tofauti yake n mjanja kavuka border
Asante mkuu.. kwa kweli vijana wa saluni sikuwa nawafahamu before, lkn sasa kwa hii comment nahisi kama nimejifunza kitu.
 
Wabongo ni watu wa ajabu saana,mwaka jana niliingia mkataba na vijana wa kazi za shamba.Nililima maharage kama hekari 12 hivi.Tumeenda nao vizuri, mpka maharage yalipo komaa na kuanza kukauka.. nilikuwa natembelea kila baada ya siku tatu..kuna siku nilipata dharula hivyo nikawa nimesafiri kama wiki nzima,ile wiki vijana walivuna maharage yote na kupiga..wakaacha kwa jirani gunia tatu tu.. zingine zote wametokomea nazo..nmewatafuta mpaka leo sijawapata..ila nmewasamehe Mungu atawalipa.
Bongo ilishawahi kuletwa mashine ya kumkamata mwizi ila nayo pia iliibiwa.
Wabongo kwenye kitu inaitwa uaminifu bado tupo nyuma sana.
 
Pole sana mkuu

Walimwengu ndivyo walivyo. Yaliwahi kunikuta hayo kwa cousin yangu kabisa niliyemtaftia kazi sehemu niliyokua nasimamia.

Baada ya kuwataftia na wengine ambao anawafahamu yeye alianza kutoka na na watu tofautitofauti pale na kuwaambia huyu dada kila anayemtaftia kazi hapa ni ndugu yake kasoro mimi☺☺☺

Mambo ya kijinga yakaanza, anonymous mails ziliandikwa hq kunichafua ila uzuri policy ilikua inasema wazi ajira izingatie watu wanajulikana na watu wa ndani, na walioniajiri waliniamini

Nakumbuka niliapa kutomtaftia tena mtu yoyote kazi!!! Ila baadae niligundua roho ya mtu haibadilishwi na ubaya aliotendewa

Kikubwa tenda wema uende zako

Usiache kusaidia watu10 wenye shida na wasio na ubaya sababu ya mtu mmoja aliyeamua kuwa mjinga
Pole sana mkuu.. Kwa kweli nimeshajifunza kuwa wabongo wakibebwa hawabebeki, japo kuna wale wachache kati ya wengi ambao wanaothamini wema wanaofanyiwa na wenzao.
 
Acha porojo, weka jina na pichake hapa ili akionekana kokote aogopwe kama ukoma
Hahahaha.. mkuu inamaana kila mtu unaemsaidia katika maisha yako ni lazima umpige picha! Kuna mkuu aliomba jina na address ya kijana nimeweka ila picha yake sina maana sikufikiria kama one day angefanya aliyoyafanya.
 
Kusema kwamba utafikiria mara mbili mbili kabla ya kumsaidia mtu mwenye tatizo kutokana na uliyojifunza ni sawa kabisa. Lakini si sawa kuwaweka Watanzania wote kwenye kapu moja kutokana tu na Mtanzania mmoja alivyokufanyia. Huyu mmoja si kipimo cha Watanzania wote. Huko huko Kusini mwa Bara letu la Afrika niliwahi kumsaidia Mkenya (japo si vikubwa kama wewe) akanilipa kwa mabaya. Siwezi kuwasema Wakenya wote kwa sababu tu ya huyu mmoja.
Umeongea ukweli na kunipa ushauri mzuri sana. Ila waswahili wanasema "mguu ulioumwa na nyoka, ukikanyaga jani unashtuka. Ki ukweli itanipa wakati mgumu sana kusaidia mtu nisiemfahamu, japo sijui huko baadae huenda nitasahau ni kibadili moyo kidogo.
 
Nyimyi watanganyika kazi zenu ni wizi na ujambazi ndio maana uaminifu kwenu ni zero tofauti na wazanzibar wanavoaminiwa ndani ya nchi yao mpaka njee ya nchi yao
Mzanzibar mmoja Johannesburg watu walimuamini sana maana alikua na kigari mfano wa kirikuu kwa hiyo maduka mengi anayajua walio Zambia,Tanzania wakawa wanatuma hela kwa ajili awanunulie vitu vinafungwa anapeleka kwenye maroli wanapima uzito unalipia yeye ni kuacha mzigo anachaji kazi unamlipa akafikia mpaka kununua gari yake ya kazi baadae akarudi kuoa huko Pemba akarudi SA huku gari kauza mambo ikaanzia hapo akaja na mkewe kipindi cha corona imekaza na Lockdown akamrudisha mkewe Pemba akaendelea kukaza baadae kapokea hrla za watu kadhaa akakimbia bila kununua mzigo ila kwa taarifa nilizozipata walimtafuta wamemrudisha kwa kaburu huko yupo jela kwa hiyo uaminifu ni tabia ya mtu sio pemba wala chunya...
 
Mkuu nataka kuja SA naomba nisaidie ila mimi nakuja na kianzio ili nisiwe mzigo kwako nimejichanga changa nmepata 1.5M ya kiTz na hela ya nauli pemben ila nmekua mzito kuja huko maana sijawahi kufika huko na sina ninae juana nae huko na nmeskia wa Tz weng wa huko unaweza ukafikiri n msaada kumbe umejipeleka kwenye mdomo wa mamba ila ww nahisi utakua tofaut kutokana na moyo wa kusaidi nataka nianzishe hata kuuza matunda tu ila nahitaji masaada wako unipe muongozo tu.
 
Mtaumiza akili na vichwa vyenu bure, South Africa ndio chimbo pekee ambalo ni rahisi kwa hawa Notorious wetu wa Bongo kukimbia Bongo na kuingia huko kwa njia za panya na wengine hufia njiani kwa kuuliwa na viboko wakati wa kuvuka mito hatari.

Haiwagharimu kiasi kikubwa cha pesa kuingia huko maana hawahitaji hata kupita official borders au airport, wao ni waruka fence ( South Africa border yote wamepiga wire fence.)

Kwahiyo chimbo hilo tegemea tabia zote za kishenzi unazozijuwa wewe Bongo utakutana nazo huko, dawa ni kukaa mbali na Wabongo kama una mishe zako na wazungu au mataifa mengine.

Hii ni tofauti na Europe na USA, process za kuingia hicho hizo zinawanyima fursa wajinga wengi kutobowa huko unless aingie kwa kuzamia meli, na kwa teknolojia inavyoshamishiri nadhani hata uzamiaji meli utafika tamati.
Lakini SA mbona hakuna complications kuingia?? Kinachowafanya hawa ndugu zetu kupita hizo njia za hatari mpaka wengine kuliwa na viboko ni nini??
 
wanijeria wanaosifika kwa wizi na mtandao mkubwa wa kitapeli duniani. Sehem wanayopigia mishe zao, wakiona kuna wabongo wawili watatu wamejisogeza eneo hilo basi wanajeria wanaihama hiyo sehemu ili kunusuru biashara zao.
😂😂wabongo nyoso
 
Habar zenu ndugu zangu. Ama baada ya salam ningependa kuendelea na kile kilichonifanya niandike uzi huu. Ndugu zangu kama ilivyo ada au kama tulivyofunzwa na misingi yetu ya Taifa kwamba watanzania popote tulipo haijalishi ni ndani au nje ya nchi, sisi ni watu wamoja. Kwahiyo kwa misingi hiyo sisi tulio nje huwa na desturi au utamaduni wa kusaidiana bila kujali tofauti zetu za kikabila, dini, rangi, jinsia au kanda ya mtu anayotokea ilimradi sote ni watanzania na tunatokea kwenye ardhi ya Tanzania basi ni ndugu.

Sasa basi miezi 3 iliyopita kuna kijana aliingia Kaburu akitokea bongo kwa lengo la kuja kutafuta maisha. Kijana anadai kuna rafiki yake wa kitaa, kwa sasa anaeishi Capetown ndio alimshawishi kuja maisha haya, lkn alipoingia tu "Kaburu" yule rafiki yake akamzimia simu na kumkosa kabisa online.

Kijana akachanganyikiwa asijue wapi pakwenda wala nini cha kufanya. Nikiwa katika mizunguko yangu mitaa ya park station Johannesburg, ghafla nikapita sehem na kumuona kijana akiwa kajiinamia na begi lake huku machozi yakimtoka. Nikamsogelea taratibu na kujaribu kumuuliza kwa lugha ya wenyeji, ghafla nikasikia jamaa akiongea kiswahili, hii ikanipa nguvu ya kumsogelea na kumuuliza zaidi baada ya kugundua kuwa naongea na mtu anaetoka nchini kwetu. Baada ya maongezi ya hapa na pale nikagundua kuwa jamaa ameingizwa cha kike na mwenyeji wake, kwahiyo nikachukua jukumu la kumsaidia.

Nikaondoka na jamaa hadi nyumban, akaoga, akala, baada ya kula nikampa sehem ya kupumzika akalala. Kwa kuwa mimi nina familia ikanibidi niende kuongea na homeboy fulan ambae ni single ili ampe hifadhi ya miezi kadhaa wakati nikiendelea na mchakato wa kumtafutia shughuli ya kufanya, mshikaji akakubali lkn kwa masharti ya kumsaidia kulipa rent.

Kwa kuwa nilikuwa nimeamua kumsaidia kijana, basi nikaona poa tu acha nimsadie kulipa rent ili aweze kuishi nae. Kijana tumekaa nae mwezi wa kwanza, wa pili na sometimes nilikuwa naenda nae kwenye mishe zangu ili kumzoesha mazingira ya nchi, na mishe za hapa na pale. Mwezi mmoja uliopita kuna rafiki angu Mkenya ambae tuliwahi kufanya nae kazi huko Gezina, Pretoria.

Mkenya alikuwa anatafuta mtu wa kumuachia saluni yake kubwa na ya kisasa iliyopo nje kidogo ya jiji la Pretoria huko Nellmapius, kwa malipo ya R600 kwa week (sawa na sh elfu 85 au elf 90) kula na kulala bure. Kwa vile nilikuwa na kijana na tayari alishanambia kuwa bongo kazi yake kubwa ilikuwa ni ukinyozi, nikaona YES maji ya mvua yameangukia juu ya mgongo wa bata. Nikampanga kijana, kesho yake mapema nikampeleka mpaka Pretoria kwa yule Mkenya na kumkabidhi.

Kweli bwana baada ya siku mbili kijana akaanza kazi huku Mkenya akiniomba nimtafutie vijana wengine ambao wataenda kusaidizana nae, maana saluni ni kubwa ilihitaji vinyozi zaidi ya watano, lkn pia kijana lugha ni tatizo, so alitaka ambao wangeweza pia kusaidiana hata katika mambo ya lugha za wenyeji ili kuwateka vizuri wateja wa kizawa.

Nikamuahidi jamaa kumtafutia hao vijana. Wakati namuacha kwa yule Mkenya kijana wang nilimuachia sim kwa ajili ya mawasiliano yetu, au ndugu zake wa bongo, au boss wake (Mkenya). Dogo tukawa tunawasiliana ananipa taarifa za kazi na mimi nampa mpa moyo kuwa akomae ili atimize malengo ya kile kilichomleta hapa nk. Siku tatu zilizopita sikumpata online, nikajua labda simu imepata tatizo ghafla.

Sasa jana yule rafiki angu Mkenya amenipigia simu na kuniambia kuwa jamaa amemuibia kila kitu cha saluni, na hela ambazo yule Mkenya anaendaga kuzichukua kwa week jamaa katimka nazo. Simu yake haipiti na hatujui tutamtoa wapi. Nilipotaka kumlipa yule Mkenya nusu ya hasara ya vitu alivyoiba jamaa, Mkenya amkataa amesema nisijali kwa vile sio kosa langu ni kosa la mtu mungine kwahiyo mimi sistahili kumlipa na ukizingatia na rafiki yangu.

Hiki kitendo cha huyu jamaa kimenisononesha na kunivunja nguvu. Imenifanya sasa niwachukie wabongo wenzangu, maana hii ni mara pili sasa nawasaidia wabongo afu wanaharibu na kutimkia kusikojulikana, japo kwa huyu sikutegemea hata kidogo kutokana na upole na muonekano wake.

Najua binadamu tunatakiwa tusamehe, lkn kwa mikasa hii sioni sababu ya kusamehe kwa lengo la kurudi kumsaidia mungine labda yule nimjuae A to Z. Ndugu zangu wabongo tubadilike, hii dunia tunapita tu. Kumuharibia mtu anaekusaidia sio ujanja bali ni ujinga wa mwisho. Hii ni tahadhari nimetoa kwa vijana wengine kuwa makini sana. Asanteni
Pole mkuu
 
Back
Top Bottom