Naapa kuwa sirudii tena kumsaidia Mtanzania -- never!

South Africa ya siku hizi ina watu wema hivyo? Yani umkute mtu analia uende kumuuliza analia nini unamsemesha kizulu then unagunduwa ni Mtanzania unampeleka kwako.

Konda tafadhali nishushe hapahapa nimefika, mwendo wa dereva ni hatarishi.
Mkuu hata majambazi watano wakija kwako, juwa kwamba kati ya wale watano kuna mmoja au wawili ambao watakuwa na moyo wa huruma kwako. Ndio pale unapokuta unapigwa na kuelekezewa mdomo wa bunduki kichwani kwako kwa lengo la kutaka utaje zilipo hela au mali au chochote wanachohitaji ndipo hapo utashangaa kati yao anatokea mmoja au wawili kumsihi yule anaepanga kukuuwa asikuuwe

Na hii ndio husababisha mtu anaibiwa kila kitu na kuachwa hai bila kupigwa au kuuwawa, japo unakuta wenyewe walikwenda pale kwa malengo mawili ya kuiba na kuuwa ili kupoteza ushahidi, ila mmoja kati yao anazuia mauaji ya muibiwaji na kusababisha wenzake wanaondoka bila kuuwa. Kwahiyo binadamu wote hatuwezi kuwa sawa, kuna wema na wabaya. Hapo sasa utaamua mwenyewe mimi uniweke katika kundi la wema au wabaya ila nilitumia utu kumsaidia na sikujua yatakayotokea mbele.
 
Pole sana, mungu atakuongezea ulipo pungukiwa. Saudia lkn uwe unawaacha wapatane wenyewe, na lazima useme wazi , hunjui.
Shukran kwa ushauri mkuu, hii imenipa funzo ambalo sikuwahi kujifunza hapo kabla.
 
Kuna thread pia humu ya biashara Commoro naskia wakijua wewe ni mtanzania wanakuogopa maana wanajua ni tapeli tu.
Wakomoro wapo tayari kufanya biashara na mkomoro mwenzao lakini sio mbongo.....

Nenda bandarini pale wanaofanya biashara comoro ni wacomoro wenyewe
 
Dah aisee niliposoma hapa nimeshtuka kidogo maana kwa jinsi ninavyomfahamu huyu jamaa sifikirii kama anaweza kufanya biashara hiyo. Kwa hapa South Africa biashara ya aina hiyo inaweza kuwa ngumu kidogo kuifanya, ila hata hivyo nashukuru kwa ushauri wako na nitajaribu kumpeleleza jamaa ili kujiridhisha na ushauri huu.
 
Huyu dogo alinambia yeye kwao ni kijitonyama opposite na sinza, jina lake ni Frank anadai kitaani alikuwa anatumia jina la chagosi. Picha sikuweza kumpiga kwani sikufikiria kuwa atayafanya aliyoyafanya. Jamaa alishatoa taarifa police, kwahiyo anatafutwa. Na kama kweli ni mgeni ninaamini atakamatwa tu maana atafika sehem ata stuck asijue pa kuelekea.
 


Pole sana mkuu

Walimwengu ndivyo walivyo. Yaliwahi kunikuta hayo kwa cousin yangu kabisa niliyemtaftia kazi sehemu niliyokua nasimamia.

Baada ya kuwataftia na wengine ambao anawafahamu yeye alianza kutoka na na watu tofautitofauti pale na kuwaambia huyu dada kila anayemtaftia kazi hapa ni ndugu yake kasoro mimi☺☺☺

Mambo ya kijinga yakaanza, anonymous mails ziliandikwa hq kunichafua ila uzuri policy ilikua inasema wazi ajira izingatie watu wanajulikana na watu wa ndani, na walioniajiri waliniamini

Nakumbuka niliapa kutomtaftia tena mtu yoyote kazi!!! Ila baadae niligundua roho ya mtu haibadilishwi na ubaya aliotendewa

Kikubwa tenda wema uende zako

Usiache kusaidia watu10 wenye shida na wasio na ubaya sababu ya mtu mmoja aliyeamua kuwa mjinga
 
Mimi siyo mnafiki na wala simwogopi mtu.

Lazima niseme ukweli.

Mbona hapo nimesema wakenya ni wezi na hujalalamika.
Sasa angalia muktadha wa uzi.. jamaa amewashutumu watanzania wote, wewe umekimbilia moja kwa moja kwenye wachaga ni wezi.. Totaly nje ya point
 
Sijui tunakwama wapi sifa zetu ni mbaya sana
Aliyetupumbaza alikuwa ni the late mwalimu na sera zake za ujamaa na kukumbatia lugha ya kiswahili kuwa ya Taifa
Ujamaa ni sera rahisi sana kuzalisha wavivu kama Raia hawakupewa elimu.
Watanzania tuna desturi ya kuchukulua poa , ndo maana unaweza kumsaidia mtu kwa nia njema tu ,na yeye akajiaminisha kuwa msaada huo ni haki yake kupewa
 
Kusema kwamba utafikiria mara mbili mbili kabla ya kumsaidia mtu mwenye tatizo kutokana na uliyojifunza ni sawa kabisa. Lakini si sawa kuwaweka Watanzania wote kwenye kapu moja kutokana tu na Mtanzania mmoja alivyokufanyia. Huyu mmoja si kipimo cha Watanzania wote. Huko huko Kusini mwa Bara letu la Afrika niliwahi kumsaidia Mkenya (japo si vikubwa kama wewe) akanilipa kwa mabaya. Siwezi kuwasema Wakenya wote kwa sababu tu ya huyu mmoja.
 
Kuna thread pia humu ya biashara Commoro naskia wakijua wewe ni mtanzania wanakuogopa maana wanajua ni tapeli tu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dah Park Station umenikumbusha mbali sana. Nilikuwa nachukua Combi hapo ili kwenda Manzini/Swaziland kabla sijafulia.
Niliwahi kukabwa na majita hapo park station , mbele ya gari ya polisi, tena saa moja asubuhi .
Kumbe polisi wanapaki gari halafu wanaenda kulewa na kuchukua malaya diplomat bar , gari linakuwa kama boya tu na majita wanalijua hilo
 
Hakika kabisaaa yaan, naamini hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…